Yeye mwenyewe kazungukwa na jamii inayomfanya ajione mnyonge, ndiyo maana hata kaona jambo hilo si la kawaida na linahitaji kuomba ushauri.
Mwanamke akiwa hana bwana watu wanampa pressure bwana wako nani? Akiwa na bwana watu wanampa pressure, anakuoa lini? Akiolewa anapewa pressure, utazaa lini? Akizaa anapewa pressure mtoto wa pili lini? Mtoto anatakiwa kuwa na mwenzake, asiwe peke yake, wa pili utazaa lini? It is ridiculous.
Yani tumemfanya mwanamke ambaye hana mtoto wala mahusiano awe mtu wa ajabu sana, wakati hayo nayo ni maisha tu.