Vodacom Kulikoni? TCRA hebu tuokoeni na hizi gharama za Data

Vodacom Kulikoni? TCRA hebu tuokoeni na hizi gharama za Data

Niliwahi kumsikia bosi mmoja wa mtandao flani akisemezana na staff wenzake. Nanukuu, "Jamani tuwe wa kweli tu, hivi sisi kama staff tukivaa viatu vya wateja wetu je tutaweza hata kununua hata kifurushi cha wiki!?"
Nilichomuelewa mimi ni kwamba;
  • wao kama stafff wanamenu yao tofauti na wateja wao
  • wanapewa muda wa hewani kila mwezi kila staff kulingana na position yake
  • consumption ya Data kati ya staff na mteja ni tofauti kabisa. Eg. Wote wakinunua 2gb itumike ndani ya wiki, data ya mteja itakata siku moja tu baadae. Lakini staff anaweza kutoboa nayo wiki nzima.
  • mishahara ya stafg ni mikubwa, that means mteja ndie anaeumia kwa kunyonywa.
  • serikali inakusanya mapato makubwa kupitia mitandao hii, hivyo mteja lazma aumie na asitegemee kushuka kwa ghalama za Data.
 
Hawa mbwa ile system ya vifurushi wameichezea. Ukipewa 1GB ya Voda ni kuwa umepewa 500MB za kikweli, hio 1GB ni Code tu imeeditiwa ikuletee hayo maneno kwenye SMS ila utashangaa inawahi kuisha balaa.😁😁😁

Ila wao wanapeana GB halisi
 
Bro ni kusogeza tatizo mbele tu, Watu wanahama mitandao ukihama baada ya muda huko nako mambo yanabadirika
Kaka nina mwaka wa 3 natumia Zantel. Same vifurushi vilivyonileta vipo intact mpaka leo. Ulaji wa Data ni same same hamna wizi hata chembe. Nikuulize tu ushawahi sikia Zantel wametajwa katika zile fine za ajabu ajabu?

Nitajie offer moja nzuri ambayo ishawahi kumaliza japo mwaka mmoja tu toka iwe launched kwenye mitandao yenu pendwa ya Tigo, Voda au Halotel?
 
TCRA wanakusanya kodi..usikute ndo wamekodineti hizi garama

TRA pia wanakusanya

PolisTZ wanakusanya

Migambo wanakusanya

Mjumbe wa nyumba kumi

Nawengineeeee
 
Voda Pamoja na Gharama zao kuwa juu nilikuwa najitutumua kwenda nao hivyo hivyo lakini imefika hatua sasa naona sitaweza kabisa
Hahahahahah endelea kujimwambafied mkuu mpaka mtapouziwa 1GB kw 20,000 for 24hrs time 😂😂😂😂
 
Yaani hii mitandao changamoto sana haswa tigo tz ndo hatari zaidi,mimi niliacha kutumia muda tu bora hata halotel
Halotel napo ni sawa na kujificha nyuma ya ua kwenye uwanja wa vita. Utapopolewa very soon 😂😂😂 tafta chaka jengine hapo sio safe
 
Halotel wana lipi la maana spidi ya konokono na unakuwa na miGB kibaoo haina kazii
Hahahahah halotel toka walivyojifunza wizi kwa tigo nilikimbilia Zantel na sijutii, mwaka wa 3 huu!
 
Muda si mrefu hata zile mb's wanazotoa kwa free basic data zitatoweka muda si mrefu.
Hahahah kule wakigusa tutaandamana. Wafanye vurugu zao huku ila kule wasiguse kabisaa.

Ile ni emergency door ya wanyonge kuingilia JF 😂😂😂
 
Halotel pia waduwanzi kichizi. Royal bundle walikuwa wanatoa 4Gb plus 2Gb bonus ikiwa na speed kali. Ukimaliza hizo, wanaaza kukupa 500Mb daily kwa speed ya kawaida hadi mwezi unaisha. Ila sasa hivi wanatoa 7Gb tu, after that bundle linakata.

Pia upande wa dakika kwa royal bundle wamepunguza pia.

Ukija vifurushi vya usiku pia ni vile vile tu. Wanafanya badariko, ila wanayaita maboresho.
Hamia Zantel acha uzembe mkuu, utakuja kunishukuru. Ndio sehemu pekee ambako wanyonge tunatamba kwa sasa 😂😂😂 utajilaumu kwanini hukujoin mapema
 
Mimi nina 30k ya muda wa maongezi wa voda kila nikiangalia kifurushi sioni kinacho suite....nadhani ninahama by kesho nitamuuzia wakala huo muda wa maongezi anibadiliahie wa halotel..... siwezi kuendelea na huu ujinga ambao wameamua kuufanya... Rubbish vodacom
 
Nahisi mitandao ya simu kuna muda huwa wanakaa vikao wanapanga mikakati ya kuwatesa wateja. Mimi voda na airtel wameniondolea ofa maalum kwa siku moja.
Hahahahahah nimecheka kinoma mkuu, eti kuwatesa wateja 😂😂😂!!! Mkuu hamteswi ila mnaeleweshwa mitano Tena kwa vitendo.😂😂😂😂😂

Mpaka kufikia 2024 vifurushi Voda, Tigo na Halotel vitakuwa:
250MB @5,000 Tshs
500MB @ 10,000 Tshs
1GB @ 15,000 Tshs

Kwa sasa ndio kwanza mko kwenye dibaji hapo 😁😁😁
 
Mimi nina 30k ya muda wa maongezi wa voda kila nikiangalia kifurushi sioni kinacho suite....nadhani ninahama by kesho nitamuuzia wakala huo muda wa maongezi anibadiliahie wa halotel..... siwezi kuendelea na huu ujinga ambao wameamua kuufanya... Rubbish vodacom
Hahahah Halotel pia sio pa kudumu, upumbavu huu soon utawafikia huko. Hamia Zantel mzee utakuja kunishukuru huku hakuna uswahili wa kubadilishiana vifurushi kila kukicha.
 
Mie voda imebaki ya kupokelea hela tu.
Naona wameamua kuigeuza line yangu ya matangazo maana kila wakati ni msg tu za matangazo yao.
 
Mie voda imebaki ya kupokelea hela tu.
Naona wameamua kuigeuza line yangu ya matangazo maana kila wakati ni msg tu za matangazo yao.
Mi pia ni line ya miamala 😂😂😂 na ni vile hela zinatoka nje ya nchi ila za hapa hapa ndani ningeua line kabisa ya hawa masheitwani😝
 
Back
Top Bottom