Tatizo linatokana na wabunge wanaodhani wanaweza kuwaamulia wananchi kila jambo bila kuwashirikisha na kupokea mawazo yao kabla ya kufanya majumuisho bungeni.
Hii tozo waliyoweka ilikuwa ni wazo na mbunge mmoja ambaye alisuggest kiujumla. Wazo hilo lingeweza kuwa na manufaa kama wangeshirikisha wananchi, wafanyabiashara na wadau wa uchumi especially micro economy.
Sikutarajia kuona Mwigulu kama PhD holder wa mambo ya uchumi analichukua wazo la mbunge na kuweka tozo kwa haraka bila kuangalia tozo iwe wapi, kwa Kiwango gani na viwango viwekwe kwa kuangalia Hali halisi ya uchumi na mzunguko wa pesa kiujumla.
Pia nilitarajia Mwigulu angetoa maelezo ya sababu zilizowafanya kuweka viwango vya tozo na kwa nini mtumaji na mpokeaji wakatwe ingali hii ni levy tu hapo kodi imekatwa pia tena kwa wote.
Haiingii akilini mtu anayetoa 5000 akatwe pesa yote hiyo, wamekokotoa vipi kufikia hicho Kiwango? Wamemshirikisha nani? Laiti wangeangalia record ya viwango vya miamala wangetambua kwamba watu wengi wanatumia na kutoa pesa chini ya 50,000. Hii ukimkata hayo makato plus Kodi anabaki na na pesa ndogo sana ambayo unakuwa umemuonea sana.
Mie naona Mwigulu ameshindwa kusimamia na kumshauri Rais kwenye masuala ya uchumi, ni wakati sahihi aenguliwe kwenye hiyo nafasi amefamya mengi ya hovyo kwa muda mfupi sana.
Mwigulu akiachwa hapo atakuwa kama Kabudi alivyokuwa anamuingiza chaka Magufuli. Huyu sio wa kumchekea.