Vodacom: Mamilioni wameacha kutumia M-Mpesa hasa vijijini, ni hatari kwa biashara yetu

Vodacom: Mamilioni wameacha kutumia M-Mpesa hasa vijijini, ni hatari kwa biashara yetu

Kosa kubwa la Rais na wasaidizi wake ni kufanya maamuzi bila kutafiti na kuwashirikisha wadau kuwa waelewe wanataka kukatwa nini na kwa ajili ya nini...
Kuna kampuni naona kabisa zikifungasha virago kutoka na huu uhuni wa Mwigulu. Kama Zantel waliondoka nini kitawashinda wengine kuondoka?

Tutabaki na TTCL watutese mpaka tushangae.

Akili ikiturudia watakaribishwa Safaricom kuja kutunyonya mpaka tushangae.
 
Huku ndiko KUKURUPUKA unaamuaje jambo serious kama hili bila kuwashirikisha stake holders km hawa
 
Siyo chonde chonde ila ni hopeless kabisa huyu jamaa. Huwa namfananisha na wale manamba wa kwenye mashamba ya katani zamani. Akili ndogo sana huyu jamaa.
Huwa sielewi alipataje PhD ingali mambo madogo kama haya ambayo hata mtu wa darasa la Saba anatoa analysis nzuri ya effect ya hii tozo especially Kiwango wallichoweka na makato mara mbilimbili wanatotoza.

Halafu amekaaga mshamba sana nahisi hii ndio tatizo atakuwa shule ndio ilimleta mjini.
 
Haya wale manowaita Mabeberu wameamua kuwateteeni maana serikali yenu chini ya Mkurupukaji Daktari Mwigulu imeamua kugombana na sisi wananchi.

Basically wao na matajiri hawatumii sana hii huduma kama sisi, nalazimika kusafiri kwenda makambako tokea Morogoro kumpa mama hela ya matumizi kwa kupanda Lori nabaki na chenji.
 
Masuala ya kiuchumi hayataki siasa tupu zisizo utafiti.

Ukitaka kumkamua maziwa ng'ombe ambaye hujamlisha, utapata damu na kumuua ng'ombe.

Kidi na tozo zina "point of diminishing returns".

Serikali ilifanya utafiti kujua hii "point of diminishing returns" iko wapi?

Ili consult na wataalam wa haya mambo kwenye sekta binafsi?
 
Huwa sielewi alipataje PhD ingali mambo madogo kama haya ambayo hata mtu wa darasa la Saba anatoa analysis nzuri ya effect ya hii tozo especially Kiwango wallichoweka na makato mara mbilimbili wanatotoza.

Halafu amekaaga mshamba sana nahisi hii ndio tatizo atakuwa shule ndio ilimleta mjini.
PhD za wanasiasa walio madarakani tena walizozipata katika vyuo vya ndani, zote zinawalakini.

Ben alihoji akapotea/potezwa
 
Bunge lote alilo liteua jiwe lijihudhulu halina faida kwa RAIA na Mali zake, na katiba mpya itaondoa huu uporaji wa aina mpya ambao umebuniwa na MUUZA drug a.k.a zungu
 
Back
Top Bottom