Vodacom Premier League 'VPL' Simba SC dhidi ya Polisi Tanzania, Rekodi Ya Alama 50 Kuwekwa Leo

90+5' Kuelekea kumalizika kwa mchezo huu wa VPL

Simba wapo eneo la katikati, kwake Chama, Boco kwake Ajibu...Faulo kuelekea PT
 
90+5' Ajibuuuuuuuu....Goooooooooooooooooooaaal Goooooooooooooooooooaaal

Ibrahimu Ajibu Migomba anawainua Simba kwa kuandika bao la pili muda mchache kabla ya kumalizika kwa mchezo huu

Simba SC 2-1 Polisi TZ
 
90+5' Naaaaaaaaaaaaaaam mpira Umee Umeeeeeeeeeeee Umekwishaaaaaaaaaaa

ambapo Simba wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Polisi TZ yakiwekwa kimiani na Bocco 57' na Ajibu 90+5' huku la Polisi likifungwa Sabilo Sixtus 22'

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha alama 50 kwa michezo 19 na kujikita kileleni huku akiwa amemaliza mzunguko wa kwanza

VPL, FT: Simba SC 2-1 Polisi Tanzania
 
Siku hizi Simba ni mpaka jioniiiiiii.
Inabidi vyura wakate rufaa maana Mnyama anaongezewa dakika nyingi na anafunga magoli ya ushindi. . Dakika 5 zote hizo za nini kama si upendeleo
 
Daah hii Simba hii, poleni Sana vyura fc najua inawauma sana
 
Inabidi vyura wakate rufaa maana Mnyama anaongezewa dakika nyingi na anafunga magoli ya ushindi. . Dakika 5 zote hizo za nini kama si upendeleo
Uliona maafadhe walivyokuwa walala ovyo Kama wanadegedege?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…