Vodacom, tiGO wapandisha tena bei za vifurushi vya Internet. Nape unafanya kazi gani?

Vodacom, tiGO wapandisha tena bei za vifurushi vya Internet. Nape unafanya kazi gani?

SABABU ZILIZOPELEKEA VIFURUSHI KUPANDA NI:-
1. VITA VYA UKRAINE
2. KUPANDA KWA MAFUTA SOKO LA DUNIA.
3. UGONJWA WA CORONA NA EBOLA.
4. UKAME NA KUCHELEWA KWA MVUA...

Sasa hapo waziri wetu anahusikaje na HAIEPUKIKI GHARAMA KUPANDA...

Miongoni mwa majibu wa Amos Makala KUHUSU CHANGAMOTO MBALIMBALI.
 
Haya ya kusema eti achia ngazi ni kelele tu
Sio kwa Africa baba
Mwingine jirani anautaka Urais kwa nguvu na amesema ni zawadi kwa mama yake [emoji1]
Yule ana mental illness mkuu... Tena dingi awe macho asije akamharakisha ili awahi kumfurahisha mama yake
 
JPM alikataa wahuni na Wezi. Mama yeye ana warudisha kwa ajili tu ya mikakati yake.

1000 GB1. siku hizi 2000 GB 1. Tena mitandao ya simu ime chakachua jinsi ya kutafuna bando. Dk 30, ume tumia 75% ya bando lako la wiki.
Nape na Makamba Waji uzuru tu. Pamoja na huyo maneno Mengi Juma Aweso-wa Maji.
Hivi itachukua miaka mingapi kuacha kumzungumzia mwendazake? Jamani he is no more and will never come back to help you. Can't you think alternative way out without him?
 
Sipendagi hii tabia ya viongozi ku compare hali ya nchi yetu na nchi nyingine ......bas tu

Hii inakuwa dalili ya kushindwa kuongoza
Kama nchi nyingine wanaumia, ndio iwe sababu ya sisi kuumia pia??
Halafu huwa wanachagua ya ku compare, yale mengine wasiyoyapenda utawasikia hao ni wakoloni na mabeberu wana mambo yao na sisi tuna ya kwetu...
 
nchi ina viongozi hii kwani au tunajiongoza wenyewe, Ingetokea nafasi ya kuhama hii nchi ningehama... sijivunii walah
Huna nasikia wakisema ni rahisi sana kuwatawala wabongo [emoji23] [emoji23]
 
Hivi itachukua miaka mingapi kuacha kumzungumzia mwendazake? Jamani he is no more and will never come back to help you. Can't you think alternative way out without him?
Serikali hadi leo imeshindwa kumsahau Nyerere wa 1961. Itakuwa ww maskini usahau JPM. Miaka 5 tu JPM; Inter change bridges Dar nzima, Meli, Mwanza-Busisi Brigde, Wami Bridge, Roads, SGR, Nyerere HEP, Stendi zote Tz, Umeme bila mgao, Ufisadi 0.05%, Vyeti feki 17,000, Uwajibikaji 80%, nk.
JPM ni SI Unit ya kumpima Kama ana faa au hafai coz alikuwa makamu wa Rais. Hizi Arguments zetu kwa Watawala ndio Alternative Ways zetu za ku Air our Voices. Hatuwataki.
 
Vifurushi vya Data kila siku vinaongezwa gharama na hawa Providers kama wapendavyo na Nape na wizara yake pamoja na TCRA wako kimya.

Leo asubuhi TIGO wamekuja na menu mpya. Nape atupishe maana hata Rais hamuondoi kama vile anafanya kazi katika kampuni binafsi ya Rais.

View attachment 2400109
Wote waliofukuzwa na Magufuli kwa sababu yoyote ile, kuanzia vyeti feki na hao Mawaziri mizigo, hawakustahili hata kidogo kurejeshwa kwenye nyadhifa hizo tena wakati damu changa zikiendelea kuzaliwa kila uchao.

Yeyote aliyetumbuliwa kisha kurejeshwa, wamekuwa na hasira na Taifa kwa kula bila kunawa midomo, ama kutoa maamuzi ya maangamizi!

Chunguza mawaziri wote waliofukuzwa na kurejeshwa uone "impact" yao kwa Taifa ipoje!

Tunabaki kujiuliza, hivi mwenye nchi anakuwa haoni huu uozo ama kuna ukuta umejengwa katikati yake na hili genge ili kumfanya asione yanayoendelea ya kuumiza watu?
 
Back
Top Bottom