Vitasa kila mahaliMi pesa zangu sikuiz natunza kupitia lipa namba ya TIGO.
Kuweka pesa Bank ni risky mno.. nimewah zinguana sana na CRDB kipindi flani ilikua kila nikideposit hela baada ya muda nikicheki balance nakuta over 200k imekuwa deducted. Sitaki tena kuskia habari za Bank
Voda wameishapita na hiyo 10m..tafuta pesa nyingineWakuu kwema?
Line yangu ya Vodacom inasoma mtandao vizuri lakini haifai kupiga namba yoyote, iwe ya kawaida au Mpesa au kununua vifurushi
Nilipoenda kwenye Vodashop nikidhani kuwa nilifungiwa sababu sikuhakiki namba vizuri
Lakini Vodashop walipoicheki wakasema niliihakiki vizuri na imetokea error tu yaani imefungwa kwa bahati mbaya na nisubiri kwa saa 24 itakuwa imefunguliwa, hiyo ilikuwa ni wiki iliyopita
Saa 24 zilipopita bado ikawa imefungiwa, nikaenda Vodacom makao makuu kuwaelezea
Makao makuu wakaniambia mbona line yako inaonekana imeshafunguliwa? Nikawaonyesha kwa kupiga simu pale kuwa haifai kupiga
Ndipo wakaniambia watashughulikia ndani ya saa 24 itakuwa tayari
Nikasubiri saa 24 zikapita bado ikawa haifai, nikawapigia huduma kwa wateja kupitia namba nyingine, huduma kwa wateja wakasema namba inaonyesha imeshafunguliwa nikate simu niijaribu tena, tukabishana pale maana nilijua haitaweza kupiga
Nikarudi tena makao makuu, wakaniambia wameishughulikia na ndani ya masaa 3 itakuwa tayari, masaa 3 yakipita ikawa haifai kupiga vilevile
Kesho yake nikarudi tena makao makuu nikawaeleza kuwa line haikufaa kupiga na sasa ninachotaka ni kupata hela zangu kwenye M Pesa hata kwa njia nyingine maana sina imani na mifumo yao tena (kumbuka siwezi kuingia M Pesa wala kufanya chochote)
Makao Makuu wakasema haiwezekani kupata hizo hela kwa njia nyingine, ni kupitia menu ya M Pesa tu,
Ila wakaniambia waliofunga line sio wao ni TCRA ila wanaipigania sana na kesho yake (leo) itakuwa tayari, jamaa akanipa na namba yake binafsi nimpigie kama haiatakuwa tayari
Sasa leo line haijawa tayari, na jamaa hapokei Simu
Wakuu hapa nafanyaje, maana hela zimekwama na sina uhakika kama nitazipata lini au ndio zitapotea moja kwa moja
CC Vodacom Tanzania
Kufanya miamala kwa line ya kawaida ndio 5 million, ila ukiiongezea uwezo unaweka hadi 100 million kutoa hadi 50 million kwa sikuSheria za Benki Kuu ya Tanzania haziruhusu mtu kuwa na million 10 kwa wakati mmoja kwa siku kwenye line ya simu; maximum amount ni million 5 kwa siku. Wewe uliwezaje kuweka million 10 kwa wakati mmoja kwenye line ya simu, na wakati huo huo ukashindwa tena kuwa mwangalifu na laini yako hadi ikafungiwa ikiwa na kiasi kikubwa hicho cha fedha?
Ndiyo maana mimi kati ya kazi ambazo nilitamani sana kufanya nchi hii, ni u-Polisi, ila basi tu sikubahatika
Ukiwapa Leseni na Tin namba inafika mil 50Hiv unaruhusiwa kuweka ela nyingi hivo kwa wakat mmoja kwenye mitandao ya simu, navojua mwisho million tano
Huwa naweka hadi 7mHiv unaruhusiwa kuweka ela nyingi hivo kwa wakat mmoja kwenye mitandao ya simu, navojua mwisho million tano
Wanaangalia mzee nani mnyonge mtu mwenye wadhifa hapo angeshawapeleka mahakamani mkuuJe wanaoweka hadi 50 million
Kutakuwa na sababu tu! Aende TCRA akajuzwe!Kuna kitu utakipata kupitia pesa zako. Inaonesha miamala yako kuna pesa ilifanyika jambo ndio zikakufikia wewe
Una uhakika kama hizo ni pesa zake mwenyewe?Bora ufanye kwenda huko TCRA ili upate ushahidi na vigezo vya kuwaburuza mahakamani wote Voda na TCRA, tafuta wakili mzuri umfahamishe hiyo kadhia yako.
Huoni wamekupa shida juu ya pesa yako mwenyewe??.
Haha umesahau kwenye makabatiBenki bado inabaki kuwa sehemu salama na rahisi kuweka na kutoa fedha
Endelea kuwasisitiza bila kuchoka
Kupanga ni kuchagua mkuu, kuweka mil 10 mpesa haimaanishi jamaa hayuko serious na uchumi wake. Yamkini ana akaunti nyingine mbalimbali na hiyo 10M kwake ni 'petty amount of money' kwa ajili ya matumizi madogomadogo ya dharura.Duh! 10ml unahifadhi m-pesa! Haupo serious na uchumi wako. Anyway nenda TCRA.
Ikishindikana nenda kwa waziri wa habari na mawasiliano.
Duniani kote, haipo kazi yenye sifa ulizozitaja wewe hapa. Kazi ambazo zinaongoza kwa kuonekana kuwa zina baraka, ni za watumishi wa Mungu pamoja na zile za dharula, zinazohusiana na uhai wa mwanadamu moja kwa moja, mojawapo zikiwa ni za udaktari na za usalama, uPolisi ikiwa ni mojawapo ya kazi hizo.Ulitamani kazi ya laana Sana Bora hujapata tu
Ndiyo, kama ulivyo wewe!
Kutamani kuwa polisi Ni kukosa hekima...Duniani kote, haipo kazi yenye sifa ulizozitaja wewe hapa. Kazi ambazo zinaongoza kwa kuonekana kuwa zina baraka, ni za watumishi wa Mungu pamoja na zile za dharula, zinazohusiana na uhai wa mwanadamu moja kwa moja, mojawapo zikiwa ni za udaktari na za usalama, uPolisi ikiwa ni mojawapo ya kazi hizo.
Ni kwa sababu watu wote wanaofanya kazi hizi wanaonekana kuwa ni immediate surbodinates wa Mungu moja kwa moja kwa sababu Mungu ndiyo chanzo cha uhai!