JaxenDL
JF-Expert Member
- May 17, 2022
- 1,118
- 2,581
Kuna yule jamaa alijitutumua mbele ya kadamnasi bila haya akasema vyombo hivyo ni mali ya CCM.Umesema "vyombo vya dola ni vyombo dola huvitumia ku-assert mamlaka". Sawa, matumizi tumekubali. Lakini swali letu sio vinatumikaje, swali ni NI MALI YA NANI? Kutumia si kumiliki. Dereva anaitumia gari la kampuni, lakini gari sio mali yake.
Umesema "Vyombo vya Scott ni vya kupikia". Tofauti ni hii: Sufuria ya Scott umeinunua kwa pesa yako. Bunduki ya JWTZ na gari la Polisi vimenunuliwa kwa KODI YA WANANCHI. Mshahara wa askari analipwa na wananchi. Ndio maana Katiba Ibara ya 8 inasema mamlaka yote na rasilimali zote ni mali ya wananchi.
Umesema "Oktoba 29 vyombo viliilinda dola". Hapo umejifunga mwenyewe. Kikatiba Ibara 147, kazi ya vyombo ni KULINDA WANANCHI na mipaka ya nchi, sio kulinda dola dhidi ya wananchi. Kama Oktoba 29 vililinda dola dhidi ya wananchi, basi ndio tatizo lenyewe - vimetumika kinyume na Katiba. Vinatakiwa vilinde wananchi, sio vitawale wananchi.
uwezo mdogo wa kifikra wa Gen Z". Hiyo inaitwa Ad Hominem - ukishindwa kujibu hoja, unaanza kumshambulia mtu. Mjadala wetu sio wa Gen Z vs wazee, mjadala ni Katiba inasema nini? Na Katiba inasema ni mali ya wananchi, sio mali ya dola wala mali ya CCM.
Bila woga bila aibu.