Kwani unawapangia mwelekeo wao wa kiuchumi? Wewe ulitaka wahamishe lini kwa deadline yako.
China kunufaika ni matokeo ya jitihada zake na wawekezaji. Unadhani wazungu wana roho nyeusi ya wivu kwamba kwa kuwa tumemsaidia akifanikiwa basi tuache kufanya naye kazi. Ni sababu tu ya sera za uchumi, sio mambo personal.
Kama wangekuwa hivyo Marekani isingetoa lend lease kwa USSR, wala isingezijenga Japan, South Korea na kuikopesha Ujerumani kurudi juu kiuchumi baada ya WW2. Na zote hizo nchi 3 hazikosi miongoni mwa nchi kubwa 10 kiuchumi duniani.
Wanabaki Beijing sababu ni mabepari, capitalists siku zote wanatazama faida. Kama China faida ipo watabaki lakini kwa kuwa mazingira ya China kuwa na faida sio exceptional kwa China peke yake bali yalitengenezwa basi yanaweza tengenezwa kwingine.
Unless utueleze ni advantage gani ipo China na haiwezi kuwepo India, Vietnam na Mexico nilizotaja.