Hizo nguvu za US unazozitaja hapa ndio udhaifu umeonekana hapo hapo.Kukosea alikosea pakubwa, lakini Bora alivamia Ili kujipima. Hii vita imepita somo America, umuhimu wa Drone, na kutovamia hovyo nchi za watu.
Lakini huwezi beza nguvu ya US kijeshi, jamaa kapiga Naval blockade Kwa Iran, na hakuna takataka ya Iran inapita kwa nguvu za Iran, sioni nchi tofauti na US yenye ball za kupiga Naval blockade.
Lakini America kwenye Air force ni Dunia nyingine, jamaa analeta jambajamba Kwa kutumia Aircraft carriers tu
Tokea 1980s Iran imesafirisha mafuta na bidhaa zingine kwa magendo kutumia shadow fleet/ghost ships. Mtindo ni huo huo hata sasa Iran inasafirisha na kuuza mafuta kutumia false flags, smuggling kupitia bandari za Pakistan, Bahari ya caspian na pia reli ya kutoka Iran mpaka China!!Lakini huwezi beza nguvu ya US kijeshi, jamaa kapiga Naval blockade Kwa Iran, na hakuna takataka ya Iran inapita. Kwa nguvu za Iran, sioni nchi tofauti na US yenye ball za kupiga Naval blockade.
Trump na Hegseth wameongelea sana kuhusu Iran kushindwa ila uhalisia unakataa.Marekani bado iko vizuri sana kijeshi. Tatizo ni kwamba, serikali ilianzisha vita bila kuwa na mikakati, halafu makamanda walipowaambia kuwa vita haianzishwi kiholela namna hiyo, wote wakafukuzwa kazi. Makamanda waliopokea majukumu leo wanajifunza wakati vita inaendela: pakubwa sana hapo. Leo nimejaza mafuta nikalipa $4:29 kwa galloni.
😁Bei ya mafuta itarudi kule kule hao Ewura wazee wa kupandisha Tsh 1000 kwa lita na kushusha Tsh 90 nawaona wakikaa vikao tena.
US navy ipo bize Iran..Wahuthi ni wa kuwekwa tanji wahuni hao. Marekani inashindwa nini kuwasambaratisha? wanaleta uhuni mashariki ya kati wapigwe tu
Nguvu kubwa ya Marekani ni kuchapisha DOLLAR.Kwao Jeshi ilikuwa kama fashion tu
Wakitegemea pakubwa Propaganda Kwamba wao wanajeshi kubwa Duniani
Lkn Iranian kaja kutupa Somo jipya kuiyusu Marekani na Jeshi lake
Kwanza waoga sana
Vita yao ilikuwa ni Angani tu
Wakishakutwanga ndio wanashuka
Kuteka maeneo yako
Sasa Iranian inakabia juu
uko uko 👀‼️
ndiomana
Trump kila siku anatokwa na maneno yasiomwisha🤠🤠
Reli kutoka Iran hadi China imepita nchi ngapi?huoni kwa hoja hii mafuta yanaweza kua gharama mara mbili zaidi ya mafuta wanayosafirisha kwa meli(Evasion)Tokea 1980s Iran imesafirisha mafuta na bidhaa zingine kwa magendo kutumia shadow fleet/ghost ships. Mtindo ni huo huo hata sasa Iran inasafirisha na kuuza mafuta kutumia false flags, smuggling kupitia bandari za Pakistan, Bahari ya caspian na pia reli ya kutoka Iran mpaka China!!
Kama Marekani wana hizo confidence waingie Hormuz kabisa ili meli zipite kwa urahisi kuliko kuwasifia kuwazuia Iran ilihali Iran nao wamezuia meli za kibiashara kuvuka Hormuz. Its illogical
Unaongea kishabiki sana Hormuz hakipiti kitu bila idhini ya kiranja wa dunia,!!!!Wahouthi wameuteka mlango bahari wa Bab al Mandab unaotenganisha Afrika na Asia na kupitisha asilimia 7 ya mafuta duniani. Bei imepanda kufikia dola 105 kwa pipa? Wahouthi wanasema meli za SA hakuna kupita.
Wahouthi hao hao wameipiga mabomu Saudi Arabia. Saudi Arabia kaomba msaada US, Trump kagoma maana naye kabanwa. Saudi ana mkataba wa Ulinzi na Uturuki na Pakistan. Wametulia wanasikilizia kumsaidia maana Iran anaweza kuwasaidia Wahouthi kwa njia itakayowaumiza sana.
So Iran ni kama anacontrol Milango ya Hormuz na Bab al Mandab na huku bado anawapiga mabomu waarabu. Turkey na Pakistan wanaweza kuingia ulingoni.
Vurugu zimekuwa kubwa sana.
Hivi kuna mbunge hana kituo cha mafuta kweli?Hao wahuni walioweka bei ya mafuta tofauti kila Mkoa kupitia Bunge lao ila bei ya Pepsi ni sawa kwa Nchi nzima ndio unawasaidia aisee hao wahuni wamejaa hapo sio mmoja inawezekana Ewura yote ni yao.
Mafuta ya Iran yanayoingia Pakistan yanamfanya Pakistan afikirie mara mbili mbili kwenda kumsaidia SA dhidi ya wahouthi.Tokea 1980s Iran imesafirisha mafuta na bidhaa zingine kwa magendo kutumia shadow fleet/ghost ships. Mtindo ni huo huo hata sasa Iran inasafirisha na kuuza mafuta kutumia false flags, smuggling kupitia bandari za Pakistan, Bahari ya caspian na pia reli ya kutoka Iran mpaka China!!
Kama Marekani wana hizo confidence waingie Hormuz kabisa ili meli zipite kwa urahisi kuliko kuwasifia kuwazuia Iran ilihali Iran nao wamezuia meli za kibiashara kuvuka Hormuz. Its illogical
Walijua wataiangusha Iran kama walivyoiangusha Libya. Kwamba watayapiga mabomu majeshi ya serikali kisha wananchi na waasi wa ndani watachukua nchi. Mambo yamekuwa tofauti.Nguvu kubwa ya Marekani ni kuchapisha DOLLAR.
Na akaitumia hiyo Dollar, kwamba ndio sarafu ya mafuta, kwa kuingia mkataa na Gulf Nations.
Jeshi la Marekni halipgligani kwa moraki, bali watu wanaajiriwa kwa pesa tu, na silaha ni biashara.
Ndio maana wanatymiaghrama.kunwa kuwalinda Israel, Gulf nations na wao wenyewe kiasi kwamba wanaonekana kuzidiwa.
Kitu pekee ambacho wangeweza kufanikowa ni kama wangekuwa na uwezo wa kupeleka askari wa ardhini kitu ambacjo kwa jipgrafia ya Iran, hawawezi.
Hapana in fact kwa meli inachukua siku 40 kufika china ila kwa reli ni siku 15 pekee kwahiyo hata kma mzigo unaoenda ni mchache kuliko meli ila spidi ni kubwa.Reli kutoka Iran hadi China imepita nchi ngapi?huoni kwa hoja hii mafuta yanaweza kua gharama mara mbili zaidi ya mafuta wanayosafirisha kwa meli(Evasion)
Wahouth wamepata nguvu, kutokana na kuharibiwa kwa kambi nyingi za marekani, kwa hiyo kwa SASA US hana backupLengo kuu kubana shingo ya Uchumi wa Marekani
Marekani inategemewa pakubwa uwekezaji wake maeneo ya Gulf States
Na Rasilimali zake kama Mafuta na Gas
Wahouthii wamepata nguvu kupitia Makombora madogo madogo Utayali wa kupigana ✅️
tofauti na Majeshi yanayoungwa mkono na Saudi Arabia ✍️
Pia volume ya mzigo kwa reli ni ndogo sana. Meli inabeba hadi mapipa 2m. Train haizidi laki moja.Reli kutoka Iran hadi China imepita nchi ngapi?huoni kwa hoja hii mafuta yanaweza kua gharama mara mbili zaidi ya mafuta wanayosafirisha kwa meli(Evasion)
Hao wahouthi watu walishajaribu kupambana nao mkuu,ila kuwasambaratisha inahitaji sio tu nguvu za kijeshi bali na mbinu nyingine ambazo sio za kijeshi. Hizo nchi za middle east baadhi yao mfano Yemen kuna mambo ya ukabila sana, hapo unakuta wahouthi wanatafuta ushawishi wa viongozi wa hayo makabila. Viongozi wanawashawishi wanajamii ili wahouthi wakubalike kwenye jamii na wachanganyikane nao. So unaweza kwenda kupigana halafu unakuta wahouthi wamejichanganya na wanajamii wengine,utamuua nani sasa hapo maana hujui yupi ni mhouthi na yupi sio mhouthi. Hata kule Iraq wanajeshi wa Marekani walivyovamia walisumbuliwa na hii issue ya ushawishi wa viongozi wa makabila,kuna vitabu vya wanajeshi walioenda kule niliwahi kusoma kimojawapo, yule mwanajeshi alisema kuna sehemu wanajeshi walikuwa wanauawa sana na haikujulikana anaewauwa ni nani maana walikuwa wanajificha kwenye milima,ikabidi serikali ya Marekani iombe baadhi ya viongozi wa Saudia wakawahonge viongozi wa kikabila wa hayo maeneo ya Iraq,ili wawapooze raia waache kuua wanajeshi wa Marekani. Ndio vifo vikapungua. Kupigana sio nguvu za kijeshi pekee,ni zaidi ya hicho.Hatari sana aisee, hilo eneo linazidi kuwa Tete.
US angekuwa na Allies (NATO) bega kwa bega huenda wangepeleka meli na manowari zao Ili kupambana na hawa Houthi ila naona wapo kimya tu.
Pakistan na Uturuki nao wapo kimya japo wana defense agreement na Saud Arabia, US Navy ndio hiyo imekwama hapo Iran.
Meli za China na Urusi zinapita bila kizuizi chochote hapo hapo Red Sea.
Kiufupi ni kama vile nguvu za Marekani kudhibiti hali na siasa za kikanda eneo hilo zimepungua.
Utawala wa Trump ulikosea sana kuanzisha vita na Iran.
Kichuguu zitto junior Kiranga T14 Armata
We ndio hujielewi, yaani Iran inazuia meli za kutoka Hormuz kupita alafu unasema US inadhibiti Hormuz? Kwanini Marekani isipeleke meli zake ili kuhakikisha hakuna meli za mafuta zinazuiwa?Unaongea kishabiki sana Hormuz hakipiti kitu bila idhini ya kiranja wa dunia,!!!!
Ni jambo la kufurahisha sana waarabu wafuga midevu na majini wakipigana na kuuana wao kwa wao na kumuacha adui yao Israel akiwashughulikia magaidi wenzako wa Hamas na Hezbollah!!!
Mkuu marekani hajapeleka Meli zake moja kwa moja kupambana meli za Mafuta zisizuiwe sababu kubwa ni moja tu,akifanya hivyo itakua direct war Hormuz means Mafuta hayatapita kabisa hata haya kidogo ambayo yanapita.We ndio hujielewi, yaani Iran inazuia meli za kutoka Hormuz kupita alafu unasema US inadhibiti Hormuz? Kwanini Marekani isipeleke meli zake ili kuhakikisha hakuna meli za mafuta zinazuiwa?
Unajitambua kweli?