Vurugu ya middle east imekuwa kubwa sana

Vurugu ya middle east imekuwa kubwa sana

Mkuu marekani hajapeleka Meli zake moja kwa moja kupambana meli za Mafuta zisizuiwe sababu kubwa ni moja tu,akifanya hivyo itakua direct war Hormuz means Mafuta hayatapita kabisa hata haya kidogo ambayo yanapita.

Iran nayeye hawezi kuruhusu hilo litokee sababu uchumi wake unategemea zaidi njia hiyo,anauza China 90% ya mafuta yake,mlango ukifungwa completely bei ya mafuta itakua ya maafa kwao,kwetu,kwa marekani, China na dunia nzima..

Marekani anachofanya sasa ni kufanya Doria gulf of Oman,Arabian Sea,na Bab al Mandab,badala ya kujaza meli za kivita ndani ya Mlango wa Hormuz wenyewe,na Huo Mlango wa Hormuz una ukubwa Kiasi gani??Geographical marekani akipeleka Meli kujaza Hormuz kwake itakua rahisi kupoteza zaidi ya anavyopigana sasa

So nimalize kwa kusema Iran kawashika Pazuri US kuzuia Mlango wa Hormuz(strategically)
Marekani waliwahi kupeleka meli zao kusindikiza meli za mafuta za Kuwait hapo Hormuz miaka hiyo, ile experience waliyoipata ndio maana hawarudii. Jiografia ya Hormuz ni changamoto aisee.
 
Niliona video wanamgambo wanaotumiwa na Saud Arabia wakiondoka, wanasema hawana Ari wala hamu ya kupigana, watu wamevaa yebo yebo wanakatisha jangwani wakikimbia na Machine gun zao...Vita zisizo na mwisho huwa zinachosha Sana hasa Kipindi hiki cha uwazi, sayansi na Teknolojia. Middle East imetengenezwa kuwa Chaos Hotbed.
 
Marekani waliwahi kupeleka meli zao kusindikiza meli za mafuta za Kuwait hapo Hormuz miaka hiyo, ile experience waliyoipata ndio maana hawarudii. Jiografia ya Hormuz ni changamoto aisee.
Yes sio kwamba hawezi au muoga but wanajua Risk,watapigwa hadi wachanganyikiwe bora eneo lingekua kubwa but eneo lisilozidi Km 39 unapeleka vipi meli za kivita??
 
Kinachoendelea ndio original plan ya Trump na matajiri wa Wall Street, vuruga oil and gas businesses za Middle East ili wamiliki soko lote duniani,US ndio number one kwa uzalishaji wa mafuta na gas,sasa wamekamata soko lote na dunia nzima tunawalipa wamarekani sasa, ni kama kwenye gas tuu,kabla ya vita ya Russia na Ukraine, 90% ya European gas ilikuwa inatoka Russia,sasa ni less than 10% na US kachukua soko lote la ulaya sasa,Hakuna cha amani wala nuclear ni oil na gas tuu na mpaka vita ziishe oil infrastructure zote za waarabu zitakuwa kwisha habari yake,na atakayekuja kuzitengeneza upya mnamjua
 
Hakupoi
Ukikimbia nchale na ukichimama nchale

Japo tunaumia na bei ya mafuta, lakini wacha dunia ichangamke
Trump kawa mdogo kama piriton, Juzi nchi za Ulaya na UK zimeiwekea vikwazo Israel, kashindwa hata kulopoka kitu

Hapa wa Houthi wamekabia kwa juu sana kushinda hata Hormuz

View attachment 3668816
Mbona kama sasa waasi wa Houth wamecharuka wanataka kuichukua Yemen yote! Aisee! Wakati ukuta! Saud Arabia amezidiwa nguvu za kuisaidia serikali ya Yemen
 
Hatari sana aisee, hilo eneo linazidi kuwa Tete.

US angekuwa na Allies (NATO) bega kwa bega huenda wangepeleka meli na manowari zao Ili kupambana na hawa Houthi ila naona wapo kimya tu.

Pakistan na Uturuki nao wapo kimya japo wana defense agreement na Saud Arabia, US Navy ndio hiyo imekwama hapo Iran.

Meli za China na Urusi zinapita bila kizuizi chochote hapo hapo Red Sea.

Kiufupi ni kama vile nguvu za Marekani kudhibiti hali na siasa za kikanda eneo hilo zimepungua.

Utawala wa Trump ulikosea sana kuanzisha vita na Iran.

Kichuguu zitto junior Kiranga T14 Armata
Alichojiroga Trump na Saudi ni wao kufanya uvamizi. Security pact za Mekkah na NATO ni defensive sio offensive. Hata Mohammed bin Salman aliambiwa na Assam Munir vita umeanzisha wewe na huu muungano wa kujilinda sio wa kushambulia.
 
We ndio hujielewi, yaani Iran inazuia meli za kutoka Hormuz kupita alafu unasema US inadhibiti Hormuz? Kwanini Marekani isipeleke meli zake ili kuhakikisha hakuna meli za mafuta zinazuiwa?

Unajitambua kweli?
Danganya Wafuga Midevu na Majini wenzako!! Hormuz kuna Naval Blockade ya Marekani!! Wajinga tu kama wewe wanajifanya hawaoni hiyo Blockade!¡
 
Iranian kama hamuogopi MAREKANI

Vip uyu Pakistan au Uturuki
Kwake si wachumba tu

Pakistan zaidi zaidi yupo na Nuclear

Lkn tukumbuke na Marekani kuna Viwanda vya Nuclear elfu 3000
Nabado Iranian anampelekea MOTO 💥💥💥 Iranian ni Mkuu wa lile eneo kwasasa🤠🤠
Wacha, mambo ya Allah hayo. 😂😂
 
Kama umeelewa Pakistan na uyu Pesa ipo Bank hawana tofauti

Saudi Arabia kawasha MOTO
Mwenyewe
kwa kutegemea Mkataba wa magumashi
Usitegemee cha jirani 🤠
Mbs alimpgia simu mara mbili trump kuomba awashambulie but trump kagoma anasema watatoa taarifa za kiintelijensia. Middle east haitatulia wamelianzisha moaka kieleweke
 
Wahouthi wameuteka mlango bahari wa Bab al Mandab unaotenganisha Afrika na Asia na kupitisha asilimia 7 ya mafuta duniani. Bei imepanda kufikia dola 105 kwa pipa? Wahouthi wanasema meli za SA hakuna kupita.

Wahouthi hao hao wameipiga mabomu Saudi Arabia. Saudi Arabia kaomba msaada US, Trump kagoma maana naye kabanwa. Saudi ana mkataba wa Ulinzi na Uturuki na Pakistan. Wametulia wanasikilizia kumsaidia maana Iran anaweza kuwasaidia Wahouthi kwa njia itakayowaumiza sana.

So Iran ni kama anacontrol Milango ya Hormuz na Bab al Mandab na huku bado anawapiga mabomu waarabu. Turkey na Pakistan wanaweza kuingia ulingoni.

Vurugu zimekuwa kubwa sana.

Acha yapigane mashenzi mashenzi wamedanganya watu na kuanza kubaguana na kuchinjana
 
Na bado wanaendelea na Vita wanataka kuendelea kuchukua miji ya Taizz na Aden na maeneo yenye Mafuta nk.



Marekani UK Israel lazima watasaidia Saudi Arabia japo

Kwasasa Iranian inaonekana inanguvu kubwa kuamua chochote mbele yao✍️

USA washir

iirika wa karibu wa Saudia wametamka kutopeleka wanajeshi wake labda watasaidia kutoa taarifa za kijasusi tu
 
Uwanja wa kishabiki , siasa za kijiopolitiki , Vita vya rasilimali na Ushawishi .

Kupigania Utaifa na utambulisho.

Utamaduni mila na desturi .
 
Aisee kweli trump amenyooka, angalia alivyokuwa muoga 😂
Leo US wanaogopa Houthi 🤣


1789219383195.png
 
Back
Top Bottom