Iran haijawahi kuivamia nchi yoyote jirani yake, ila yenyewe ndio imevamiwa na kushambuliwa na maadui zake mf Iraq ya Saddam, Israel na Marekani....
Iran inafadhili proxies katika Nchi jirani na kufadhili instabilities. Inataka kusambaza mapinduzi yake katika Nchi jirani za Kisunni.
Na vita kati ya Iraq na Iran (1980-1988) vilisababishwa na provocations za Iran dhidi ya Iraq ikiwemo kutaka kusambaza mapinduzi yao na kutaka kumpindua Saddam Hussein.
Tofauti na Saud Arabia iliyoishambulia Yemen na kuua maelfu ya raia wasio na hatia.
Saudia ilianza mashambulizi dhidi ya MaHouthi mwaka 2015 kuwasaidia WaYemen WaSunni waliokuwa wakiuawa na MaHouthi vibaraka wa Iran na pia kuitetea Serikali halali inayotambulika kimataifa. Ahlus Sunnah walikuwa wanauawa Yemen na hakukuwa na Makelele, ila Saudia na Baadhi ya Nchi za Kiislam zilipoingilia kuwatetea WaSunni wa Yemen ndio makelele yakaanza. Wale Waislam Wa Sunni waliokuwa wanauawa bila ya hatia sio watu au?
Halafu Saudia wakawa wanalaumiwa kusababisha Starvation Yemen, wakati maHouthi ndio walikuwa wanapora misaada ya kibinadamu iliyokuwa ikienda Yemen na kusababisha Starvation.
Mazayuni wameua Wapalestina wanaofikia 75,000 ila wewe unawaona afadhali kuliko Iran?....
Iran ikishirikiana na yule kafiri Bashar al Assad na Ma Hezbo wameua malaki ya Waislam, MALAKI YA WAISLAM, huko Syria. Na hiyo ni Syria tu. Sikuambii waliouawa Yemen, Iraq na Lebanon na kwengineko.
Mashia kila walipopata fursa ya kuua Waislam wameifanya kikatili mno.
Idadi ya Waislam waliouawa na Mashia katika Nchi za Kiislam huwezi kuilinganisha na mazayuni ijapokuwa wote ni mashetani.
Mazayuni hawajawahi kuishambulia Makkah wala Madinah, ila Mashia wamefanya hivyo.
Mashia wameua mpaka mahujaji, kitu ambacho mazayuni hawajakifanya.
Na zaidi mazayuni ni maadui wa wazi wa Uislam, ilhali mashia wanajificha nyuma ya Uislam.
Waliopaswa kuwa mstari wa kuwatetea Wapalestina (Misri na nchi nyingine za Ghuba) zote ni vibaraka wa Israel na Marekani...Labda kidogo Uturuki ndio angalau inatetea Wapalestina.
Nchi za Kiislam zilizoingia katika mahusiano ya kidiplomasia na Mazayuni sio vibaraka wa mazayuni. Kuwa na diplomatic relations na mikataba ya Amani na nchi maadui sio kuwa kibaraka.
Kuwa na mahusiano ya kidiplomasia na Nchi za kikafiri kwa Maslahi ya Ummah wa Kiislam kwa kufuata misingi ya Shari'ah sio jambo baya. Na wala sio kuwa kibaraka.
Na ndio maana hizo nchi zina mahusiano ya kidiplomasia na mpaka China ama Urusi.
Mbona dola ya Kishia ya Iran ina mahusiano tena ya karibu sana na Urusi licha ya kuwa Urusi imeua Waislam Chechnya na imeua Waislam ikimsaidia kafiri Assad na Iran na Hezbo huko Syria? Mbona ina mahusiano mazuri sana na China inayocommit genocide dhidi ya Uyghurs na inai occupy East Turkestan?
Mbona ina mahusiano mazuri sana na India inayowakandamiza Wakashmiri na ina uadui wa wazi na Nchi ya Kiislam ya Pakistan?
Ni kibaraka wao?
Na Nchi za Ghuba, ukiitoa Bahrain na UAE, ni nani mwengine Ana mahusiano rasmi na dola ya Kizayuni?
Hata kuitambua dola ya kizayuni hawaitambui, ikiwemo Saudi Arabia ambao hawaitambui kabisa dola ya kizayuni na suala la kuitambua tu dola ya kizayuni wamelifungamanisha suala hilo na kuanzishwa kwa Taifa huru la Palestina. Hivyo hakuna recognition bila kuanzishwa kwa Taifa huru la Palestina na nadhani unaijua Sera hii ya wazi kabisa ya Saudi Arabia.
Na pia Nchi za Kiarabu zimeongoza mpaka 1970's kuipigania Palestina kwa vita vya kisilaha. Waarabu wamepigana vita Nne na mazayuni. Ni kuanzia miaka ya 70, hasa baada ya mapinduzi ya Iran ya kina Khomeini na akina Khomeini wakatangaza kuyasambaza mapinduzi yao kwa Nchi za Kiarabu na Kiislam ndio Nchi za Kiarabu nyingi zikaanza kubadilisha approach yao ya kudeal na mazayuni.
Na pia Nchi za Kiarabu hazijaacha kuwapigania Wapalestina, ila hazipigani tena na mazayuni kwa vita za silaha kwa sababu ya kuchunga maslahi mapana ya Waislam ikiwemo Wapalestina wenyewe. Wana experience ya kupigana vita nne na mazayuni, wanawajua, hivyo wamebadilisha mbinu ya kudili nao. Ukizingatia sasa hivi wana adui mwengine, dola ya kishia ya Iran, ambaye ametangaza kuwapiga vita wazi, hivyo lazima wapige hesabu zao vizuri. Geopolitics na mambo ya kimataifa sio masuala ya kuyachukulia kishabiki shabiki na kitoto.
Nchi za Gulf wanaipigania Palestine, ndio wapelekaji wakubwa wa misaada ya kibinadamu, ndio wanaongoza ku lobby kwa ajili ya recognition yao Palestine kwa kutumia diplomasia, hata mpango wa kui rebuild Gaza utaona ni akina Saudi Arabia ndio wanaipanga na kupanga mabilioni kwa ajili ya kuijenga upya Gaza.
Ila hawapigani na mazayuni kwa sababu ya kuepusha madhara makubwa zaidi na wanataka kuchunga maslahi mapana ya Waislam ikiwemo waPalestine wenyewe.
Wewe mwenyewe unaona Iran yenyewe haiwezi kuwakomboa Wapalestina kwa kupigana na mazayuni (bali hawana hata huo mpango bali wanafanya propaganda tu). Wala hawajawahi kuingia vitani na mazayuni kwa ajili ya Palestine licha ya rhetoric zao na slogans zao, wanajitutumia pale tu wanapoanza kupigwa wao.
Israel imeshajitanua kwa kumega ardhi za Gaza, Lebanon, Syria na bado wana ndoto za kuongeza maeneo zaidi ila Iran mpaka Sasa haijamega ardhi yoyote ya jirani yake
Iran ina mpango wa kujitanua kwa kuwatumia proxies wao. Na imejaribu hilo na ina mpango huo bado. Inataka ku export mapinduzi yao na kujitanua.
Vibaraka wa mazayuni wanafahamika (Fuatilia Abram Accords)...Iran haipo hilo kundi
Abraham Accords sio ushahidi kuwa Nchi zinazoshiriki mazungumzo ya hayo makubaliano ni vibaraka, Nchi za Kiarabu kufanya mazungumzo kwa ajili ya mikataba ya Amani kwa maslahi mapana ya Nchi zao na Waislam kwa ujumla sio ukibaraka.
Na Iran sio adui wa mazayuni kwa sababu ya Wapalestina, huwa wanashirikiana na mazayuni kila pale maslahi yao yanapoendana na mazayuni katika ukanda ule, uadui wao na mkinzano wao ni kugombania kuidhibiti Mashariki ya kati ndio kuna kupishana na wanajikuta approach zao zinagongana na kukinzana, ila hushirikiana kila maslahi yao yanapoendana. Na ndio maana Waarabu wenyewe wako chonjo kwa sababu dola ya kishia ya Iran kuwa backstab ni sekunde tu.
Iran kusema wanawapiga vita mazayuni kwa sababu ya Wapalestina ni propaganda ambayo wamekuja nayo kujaribu kujipatia ushawishi kwa MaSunni, na wakati huo huo kueneza influence yao. Ila sio kweli kuwa wanawapigania Wapalestina.
Iran inashirikiana na mazayuni pale maslahi yao yanapokutana, ila hilo hilo linafanywa ni kosa lisilosameheka kwa Waarabu.