Kenya 2022 Vurugu zanukia Kenya, mawakala wa Odinga waishtumu tume kufanya uhalifu

Kenya 2022 Vurugu zanukia Kenya, mawakala wa Odinga waishtumu tume kufanya uhalifu

Kenya 2022 General Election
Mnatamkatamka kila wakati hadi asiyejua anaona ni shida hasa.Kwa Raila na kwa Martha Karua kura nyingi kachukua Samoei Ruto.Huo ukabila mnaoung'ang'aniza unatoka wapi kwa mfano huo mdogo tu?
Wewe hili hulijui?

Hujui kwa nini Uhuru Kenyatta kakataliwa katakata na hao nduguzake wanaomkataa Odinga sasa hivi?

Kama hujui maana yake, itakuwa huelewi chochote kinachoendelea nchini humo..
 
Ukabila upo Kenya.Si kwamba haupo.Ila si kama mnavyoukuza.Mnavyoueleza kana kwamba akifika mgeni leo basi atachinjwa au ataishi kipweke sana.Siyo hivyo!
Sasa wewe unataka kuwepo ukabila kuonekane vipi? Hebu tueleze wewe!

Kama mtu hawezi kumchagua kiongozi kwa sababu tu ni kabila fulani, na si kwa sababu ya anayoyasimamia kuyatimiza; kama huo siyo ukabila ni kitu gani?
 
Wabongo wanashobokea tu mambo kwa mihemko kama ilivyo jadi yao.

Saitabao yumo BOMAS na haoni huo UWAZI ila mbumbumbu mmoja yupo Namtumbo huko anakubania pua.

Mbona hamzungumzii tena kuhusu uwazi wa fomu za 34A uliositishwa na IEBC? 24hr+ just two forms uploaded.

Mtu anayefuatilia kwa karibu kabisa hawezi kuona upekee wowote wa uchaguzi huu na hata reports za waangalizi zimesema dosari ndogondogo zimejitokeza.

Hata hiyo internet yenyewe inaenda kuzimwa,subirieni kesho!
 
Wewe hili hulijui?

Hujui kwa nini Uhuru Kenyatta kakataliwa katakata na hao nduguzake wanaomkataa Odinga sasa hivi?

Kama hujui maana yake, itakuwa huelewi chochote kinachoendelea nchini humo..
Hiyo ni tabia ya kibinadamu.Uchoyo.Self-centeredness.Mawazo yao waliona kama Uhuru anawaondolea "Urais" katika himaya yao ya ukabila.Hiyo ni tabia tu ya kibinadamu kutaka kumiliki vitu vizuri vyote peke yake,au famili yake,au ukoo wake au kabila lake.Misingi ya Wakenya kumuona kila aliyezaliwa ndani ya mipaka ya Kenya achukuliwe kama Mkenya ni jambo la kwenda nao polepole.Huwezi kuamka tu likawa sawa.Au ukaamuru tu likaisha hapohapo.Ni kama ujinga ulivyosambaa Tanzania.
 
Akili mgando ndio hizi, tume ina siku 7 kutangaza matokeo na wapo ndani ya wakati.

Kuhesabu kura manual ndio utaratibu sahihi na hakuna computer hackers wanaweza kuuingilia.
Hili siyo tatizo kubwa, na wako ndani ya muda wao wa kufanya kazi. Sidhani kwamba kuna yeyote kati ya wagombea anayelalamikia ucheleweshaji. Kuna ya ziada yanayoendana na ucheleweshaji huo, na makosa yasiyo na msingi wa kuwepo yanayoweka hali ya wasiwasi kwa baadhi ya wagombea.
 
Sasa wewe unataka kuwepo ukabila kuonekane vipi? Hebu tueleze wewe!

Kama mtu hawezi kumchagua kiongozi kwa sababu tu ni kabila fulani, na si kwa sababu ya anayoyasimamia kuyatimiza; kama huo siyo ukabila ni kitu gani?
Usijidanganye ndugu yangu.Ukabila na ubaguzi upo sana hata Tanzania.Muulize Jesca Msambatavangu au hata Joseph Mbilinyi walivyopata tabu hadi kukubalika majimboni mwao.Jesca alikuwa akibaguliwa na wenyeji wa Iringa(Wahehe na Wamanyema)kwa sababu ya Ubena na uanamke wake.Baada ya CCM kuzidiwa na kukosa mbadala wa kupambana na Msigwa ndiyo Jesca akakubaliwa kwa shingo upande.Vivyo hivyo kwa Sugu.Ukinga wa Sugu ulikuwa ni changamoto kwa Wanyakyusa na wenye asili ya Mbeya.Nguvu ya CHADEMA ilimbeba Sugu kwa nguvu.Hiyo ni mifano tu ya ubaguzi iliyopo hata Tanzania.
 
Hiyo ni tabia ya kibinadamu.Uchoyo.Self-centeredness.Mawazo yao waliona kama Uhuru anawaondolea "Urais" katika himaya yao ya ukabila.Hiyo ni tabia tu ya kibinadamu kutaka kumiliki vitu vizuri vyote peke yake,au famili yake,au ukoo wake au kabila lake.Misingi ya Wakenya kumuona kila aliyezaliwa ndani ya mipaka ya Kenya achukuliwe kama Mkenya ni jambo la kwenda nao polepole.Huwezi kuamka tu likawa sawa.Au ukaamuru tu likaisha hapohapo.Ni kama ujinga ulivyosambaa Tanzania.
Duh!

Kwa hiyo hii ndiyo kiwe kisingizio cha eneo zima kufanya uamizi wa kumchagua kiongozi? Hapa huoni kasoro yoyote?
 
Ukiona hivyo ujue wameshaona kuwa kura za mzee hazijatosha!! Uwazi uliowekwa na tume ya uchaguzi ya kenya iliyo huru kweli kweli unamwezesha kila mgombea kuweza kuhesabu kura zake kwa usahihi kabisa!! Anachozuiwa tu ni kujitangaza kuwa mshindi kitu ambacho Raila amekikiuka baada ya kutangaza kuwa ndiye kashinda uchaguzi. Ukweli ni kwamba huenda uchaguzi ukarudiwa kwa wagombea kushindwa kupata 50%+1 ya kura halali!!
 
Usijidanganye ndugu yangu.Ukabila na ubaguzi upo sana hata Tanzania.Muulize Jesca Msambatavangu au hata Joseph Mbilinyi walivyopata tabu hadi kukubalika majimboni mwao.Jesca alikuwa akibaguliwa na wenyeji wa Iringa(Wahehe na Wamanyema)kwa sababu ya Ubena na uanamke wake.Baada ya CCM kuzidiwa na kukosa mbadala wa kupambana na Msigwa ndiyo Jesca akakubaliwa kwa shingo upande.Vivyo hivyo kwa Sugu.Ukinga wa Sugu ulikuwa ni changamoto kwa Wanyakyusa na wenye asili ya Mbeya.Nguvu ya CHADEMA ilimbeba Sugu kwa nguvu.Hiyo ni mifano tu ya ubaguzi iliyopo hata Tanzania.
Naona unazidi kujichanganya. Nimekwisha kueleza wazi, hali ya hivi karibuni ndani ya Tanzania, siwezi kuitoa kama mfano mahali pengine popote, lakini hutaki kuelewa.

Kwa hiyo kwa kuwa Tanzania wanakwenda huko waliko wakenya, unataka tuache kuisema hali mbovu iliyoko huko Kenya?
 
Sikuchanganyi.Labda weye ndiye unashindwa kunyakua kinachotakiwa kwa wakati gani.
 
Hakuna u-perfect!Changamoto zipo ila tusizipe sura ngumu kiasi hicho.
Hakuna anayetafuta u'perfect' kwa yeyote. Kenya wanayo mifumo mizuri kabisa ya kufanya mambo yao, lakini bado wanakwama, kwa sababu ya mambo ya msingi kabisa, kama ukabila. Hili liko wazi kabisa.
 
Mzee Odinga sijui kanusa kushindwa sijui
Mawakala wake wamekuwa wakilalamikiwa na Tume kuzua vurugu kila mara kwenye ukumbi wa kuhesabia kura Bomas

Wakala Mkuu wa odinga anasema Bomas imekuwa chumba cha uhalifu akimaanisha haamini mchakato wa uhakiki
View attachment 2323329
Ruto/Luwasa style , mzee baba keshashituka , baba anachukuwa nchi.
 
Attachments

  • VID-20220814-WA0017.mp4
    14.8 MB

  • VID-20220812-WA0111.mp4
    5.3 MB
Nakubaliana na wewe kabisa. Tatizo ni tume. Kwa sababunwalikuwabwatangaze matokeo kwa kutumia zile karatasi zilizowekwa kwenye mtandao wa tume. Sasa kama kuna mtu angelalamika ndio angeenda mahakamani ili ukaguzi wa karatasi halisi ufanyike. Wamejibebesha mzigo mzito bila sababu. Na kuifanya matokeo yaliyowekwa kwenye tovuti yako kutokuwa na maana.
Unajua kwa nini wanalazimika kufanya verification? Ni kwa sababu Supreme Court chini ya Judge David Maraga walitengua matokeo ya Urais kwa sababu ya kasoro hizi za kutokuhakiki matokeo.Sasa unataka Tume warudie kosa lile lile walilofanya kwa uchaguzi uliopita?
 
Chebukati 2017 alizingua sana hadi ikabidi mahakama kutengua uchaguzi. Naona hukumbuki!

Safari hii, isingekuwa haya makosa madogo madogo, na ucheleweshaji usiostahili angejizolea sifa nyingi sana bila kujali nani kashinda.
Sasa huu ucheleweshaji, na funikafunika hii inaharibu jambo ambalo lingekuwa zuri sana.
Makosa madogo kama yepi?
 
Ndio najua mana yake lakini hapa wewe ndio hujui wala matumizi yake kwenye sentensi huyafahamu hayo kwamba wewe unafanya biashara ni yakwako mwenyewe.

Soma sentensi yako uone ujinga ulioandika.
Sijui unajua English au umeishia la ngapi
Najua nimesema Kenya ndio importer wetu mkuu, au Kenya is our leading importer kwa English, sasa hapo kuna shida gani?
Au Kenya ndio exporter wetu mkuu ndio ingekuwa sahihi?
 
Hujielewi wewe.
 
Back
Top Bottom