Uchaguzi 2020 Vurugu zatawala ofisi za CCM Dodoma baada ya walioshinda kura za maoni Udiwani kukatwa

Uchaguzi 2020 Vurugu zatawala ofisi za CCM Dodoma baada ya walioshinda kura za maoni Udiwani kukatwa

18 Aug 2020
Dodoma, Tanzania

WanaCCM waandamana kupinga maamuzi



Vurugu zinaendelea leo 18 agosti 2020 katika ofisi za CCM Wilaya ya Dodoma mjini baada ya kupokea majina ya wagombea udiwani ambao wamekatwa licha ya kuongoza.

Jana halmashauri ya CCM mkoa wa Dodoma walirudisha majina ya madiwani waliogombea kupitia chama hicho ambapo kata 7 Kati ya 41 za jiji la Dodoma walioongoza walikatwa na kurudishwa wengine ndipo wakaandamana ofisi za wilaya.

Mmoja wa diwani aliyeshinda CCM lakini jina lake lililokatwa amewaomba wanaCCM wa kata ya Changombe kuwa watulivu wasifanye maandamano wasubiri maamuzi ya Halmshauri ya wilaya CCM watakapotafuta ufumbuzi wa sintofahamu hiyo ndani ya CCM .

Chanzo: Mwananchi digital

Mtu huyu anabembelelezwa kupanda karandinga lakini ingekuwa wa upande mwingine angeshakula mitama kibao
 
Mambo Ni Moto..alhamisi patanoga zaidi..
IMG-20200817-WA0002.jpeg
 
Katika hali isiyo ya kawaida tofauti kabisa na wanavyofanyiwa wafuasi wa vyama vya upinzani polisi jijini Dodoma wamemkamata kistaarabu mno huku wakimbembeleza kwa maneno matamu mfuasi wa CCM aliyefanya vurugu na kuhatarisha amani ya nchi kwa kushiriki maandamano bila kibali na kuvamia ofisi za CCM wilaya ya Dodoma kupinga uteuzi wa mgombea udiwani.

Walisikika polisi wakimsihi na kumbembeleza kwa maneno matamu, "njoo bwana!" "Panda twende basi". Huku jamaa akikataa akisema " kwanini mtumie dola?" " kwani mimi ni mpinzani".

Huu ni upendeleo wa wazi wa jeshi la polisi nchini, ukilinganisha na tukio la karibuni mathalani jinsi alivyopigwa Tanganyika jeki Mheshimiwa Joseph Mbilinyi kule Mbeya kuna tofauti kubwa sana.

Tafashali mods huu uzi usiunganishwe na wowote tujadili upendeleo huu wa jeshi la polisi.View attachment 1541192
Vumilieni kidogo maana October 2020 Lissu anakuwa rais na Salum Mwalimu anakuwa makamu wa rais wa JMT mnafanya mnavyotaka.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Kamati kuu waliwahi kuandamana na kuimba wanaimani na Lowasa lakini bado huyo Lowasa akakatwaa!
Lowasa akahamia upinzani wale waliondamana wakahama nae na kauli mbiu ya UlipoTupo nako akafeli
Msingi wa CCM uko imara sana bado, muda utatoa majibu

Hiyo ndio ccm tuijuayo ambayo ni chama dola. Mwl JK alisema, Bila CCM imara hatuna taifa imara. Huyu aliye kusanya watu na kuwa shawishi kufanya vurugu lazima aadhibiwe kwa mujibu wa taratibu za katiba ya chama. Awe fundisho kwa wengine wanaotarajia kufanya hivyo. Asitake kuuaminisha umma kuwa chama nguli Afrka CCM hakina taratibu za kushughulikia tatizo lake.
 
Walialia kwanini sasa wakati taratibu za chama zao ndivyo zinavyosema kwamba hata kama umeshinda kuna vikao vingine vya chama ndivyo vyenye mamlaka ya kukamilisha zoezi la uteuzi ambapo kuna kukatwa ama kuendelea kama wajumbe walivyotaka
 
UJANJA AMBAO CCM WAMEUFANYA MWAKA HUU, WANATAKA WATANGAZE MAJINA TAREHE ZA MWISHO WA KUCHUKUA FORM ILI UKIKATWA HATA UKIKIMBILIA UPINZANI UNAKUTA FORM HAZITOLEWI TENA SABABU MWISHO WA KUCHUKUA FORM NI TAREHE 25/08/2020.
Kwani huko upinzani hakuna wagombea Hadi mlalamike kuwa waliokatwa CCM hawana muda wa kuja kwenu? Mpayukaji Hana watu wa kumfaa huko Hadi mmuletee waliokatwa CCM?

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom