Wewe ni coward kwani sasa hivi familia ngapi zinateseka,Ben wa saanane, aquilina,azory gwanda,mwangosi, watu 21 Pemba, mawazo, kinondoni uchaguzi mdogo ,makamanda kibao wameuliwa na greengurd, miili Coco beach,kibiti,na wengine wengi waliofilisiwa na kesi za uchumi kwenye jasho Lao hiyo Amani unayohubiri ipo wapi? WA kina kabendera? Tatizo bado hayajakufika ndo mana unaongea huo upuuzi wako tulia dawa ikuingie#anaitwaroma#tumehuruyauchaguzi#katibampyayawarioba
COWARD? NOT ME.
Labda neno "coward" lipotoshwe; mimi siyo coward. Hoja yangu ni AMANI badala ya Vurugu. Sote (pamoja na wewe) ni wadau na wanufaika wa amani. Unaandika na kutoa mawazo kwa kuwa uko hai. Wafu huwa hawaongei!
Umemtaja Acquilina na wengineo kama wahanga. Unataka tuwe na vurugu ili idadi ya wahanga iongezeke? Mimi nasema HAPANA. Na nitaendelea kutetea hoja ya amani hata kama kwa kufanya hivyo utanibatiza majina ya kebehi.
Watanzania tuna nchi moja (TANZANIA) ya kuishi na kuendesha maisha yetu kama raia.
Usijidanganye kwa hoja potofu kwamba njia ya vurugu itatupeleka kwenye amani zaidi na maisha bora zaidi ya haya tuliyo nayo. Mwenyezi Mungu Atuepushe na njia unayoihubiri.