Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Leo nimeunganisha matukio ya vyama vikongwe vya siasa Afrika ambavyo vimeonesha weledi wake na kufanya nchi zao ziwe za kupigiwa mfano Afrika.
Chama cha kwanza ni chama cha United National Independency Party (UNIP) Cha Zambia ambacho kilitawala Zambia tangu mwaka 1964 hadi mwaka 1991.
Mwaka 1991 UNIP walishindwa uchaguzi dhidi ya chama cha Movement for Multparty Democracy (MMD) kilichokuwa kinaongozwa na Fredrick Chiluba.
Mpaka Leo Zambia kumetulia na UNIP wamekubaliana na matokeo.
Chama cha pili ni Kenya Africans National Union (KANU). Mwaka 2002 Muungano wa vyama vya siasa uliojulikana kwa jina la National Rainbow Coalition (NARC) ulishinda uchaguzi.
KANU wala hawakushughulika kupindua matokeo kama tabia ya CCM ilivyo wanaposhindwa uchaguzi. Maisha ya KANU huko Kenya yanaendelea na siasa zinasonga mbele.
Chama cha mwisho ni African National Congress (ANC) cha Afrika ya kusini.
Kwenye uchaguzi wa mwaka huu ANC imekataliwa na waafrika ya kusini. ANC wamepata asilimia arobaini (40%) wakati vyama vingine vimepata Asilimia sitini (60%).
ANC wala hawajifaragui kukubali matokeo badala yake wanatafuta kuunda Serikali na vyama vya siasa vingine walivyoshindana navyo kwenye uchaguzi.
Afrika nzima kwenye purukushani za mapinduzi na machafuko ni kule ambako vyama vilivyoko madarakani hukataa matokeo au mabadiliko.
CCM tabia yake ya kupora matokeo imewanogea hadi kwa Sasa hawaoni tena aibu kupora uchaguzi.
Walianza mwaka 1995 kule Zanzibar na baadae mwaka 2019/2020 wakaiba uchaguzi mzima.
Iko siku tabia hii ya kukataa kushindwa ya CCM italiletea Taifa letu madhara.