Vyama vinavyong'ang'ania madaraka kama CCM ndiyo huleta machafuko na mapinduzi Afrika

Vyama vinavyong'ang'ania madaraka kama CCM ndiyo huleta machafuko na mapinduzi Afrika

Yaani kwa sera CCM ni bora kuliko ANC!?

hebu weka hapa sera hata moja ya CCM ambayo wewe unaona Bora!!
Mlinganisho wako ni mlinganisho mfu.ANC wanakumbana na upinzani uliojipanga.DA waliwahi kutawala South Afrika,Zuma na Malema ni zao la ANC wanajua kujenga hoja za kufanya wachaguliwe licha ya kutoshinda.
Hapa Tanzania tuna wapinzani waganga njaa tu na kusema eti walishinda Urais 2020 ni wishful thinking.
Wapinzani wa Tanzania ni wakosoaji wa matukio bila sera mbadala za kiuchumi,mazingira na uhusiano wa kimataifa.
Lini ulisikia wame table bajeti mbadala na jinsi watakavyo finance hayo matumizi.
Hawa ni wafukuzia ruzuku tu ili kushibisha matumbo yao.Na hawana utamaduni wa kukubali kushindwa. Mfano Msigwa kashindwa lakini anadai kashinda.
 
Leo nimeunganisha matukio ya vyama vikongwe vya siasa Afrika ambavyo vimeonesha weledi wake na kufanya nchi zao ziwe za kupigiwa mfano Afrika.

Chama cha kwanza ni chama cha United National Independency Party (UNIP) Cha Zambia ambacho kilitawala Zambia tangu mwaka 1964 hadi mwaka 1991.

Mwaka 1991 UNIP walishindwa uchaguzi dhidi ya chama cha Movement for Multparty Democracy (MMD) kilichokuwa kinaongozwa na Fredrick Chiluba.
Mpaka Leo Zambia kumetulia na UNIP wamekubaliana na matokeo.

Chama cha pili ni Kenya Africans National Union (KANU). Mwaka 2002 Muungano wa vyama vya siasa uliojulikana kwa jina la National Rainbow Coalition (NARC) ulishinda uchaguzi.

KANU wala hawakushughulika kupindua matokeo kama tabia ya CCM ilivyo wanaposhindwa uchaguzi. Maisha ya KANU huko Kenya yanaendelea na siasa zinasonga mbele.

Chama cha mwisho ni African National Congress (ANC) cha Afrika ya kusini.

Kwenye uchaguzi wa mwaka huu ANC imekataliwa na waafrika ya kusini. ANC wamepata asilimia arobaini (40%) wakati vyama vingine vimepata Asilimia sitini (60%).

ANC wala hawajifaragui kukubali matokeo badala yake wanatafuta kuunda Serikali na vyama vya siasa vingine walivyoshindana navyo kwenye uchaguzi.

Afrika nzima kwenye purukushani za mapinduzi na machafuko ni kule ambako vyama vilivyoko madarakani hukataa matokeo au mabadiliko.

CCM tabia yake ya kupora matokeo imewanogea hadi kwa Sasa hawaoni tena aibu kupora uchaguzi.

Walianza mwaka 1995 kule Zanzibar na baadae mwaka 2019/2020 wakaiba uchaguzi mzima.

Iko siku tabia hii ya kukataa kushindwa ya CCM italiletea Taifa letu madhara.
Hao wapinzani washinde kwenye sanduku la kura, hakuna ushindi wa zawadi
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Bila vyama vya upinzani kuungana basi sahau sisiemu kutoka madarakani.
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Bado CCM ni chama Cha grassroots...CHADEMA ilianzishwa vibaya kwahiyo memory za watu Bado zinaikumbuka historia hiyo. Mpaka sasa kama ni CCM basi imefanikiwa kuifanya nchi ikose mpinzani wa kweli. Hii ingekuwa nzuri kama yenyewe itasimamia maslahi ya wananchi, lakini wachache wetu tumeamua kukiweka kwapani Ili tule matunda ya nchi peke yetu...Hii ni hatari sana Kwa CCM chama changu, please let us go back to our values
Mkuu 'Ame'... "please, let us go back to our roots" IMPOSSIBLE under the current circumstances. You're asking fo too much! Nani huko CCM mwenye uwezo wa kufanya kazi kubwa na ngumu kama hiyo?
Listen, I stand with you for the sake of Tanzania; but the reality is that CCM in its current form is beyond repair. Sorry! to both of us and to our beloved Tanzania

Inaonesha huna ulijualo kuhusu siasa... CPC haitawali kama CCM
Ukweli mtupu, hata sijui kwa nini alitoa mlinganisho wa namna hiyo.

Mkuu, 'Allen Kilewella', umetoa bonge la mada hapa; lakini kama ujuavyo huwezi kupata mjadala wa kukidhi ubora/umuhimu wa mada yenyewe. Tutagusagusa tu na kukuachia mipasho ya hapa na pale, kama unavyoona mwenyewe hapa.

Lakini ukweli ni kuwa CCM ipo njiani kuondoka madarakani, iwe kwa kukubali au kwa kuondolewa kwa nguvu.
 
Its a zero sum game.

Dola sio peremende unamega halafu unampatia mwenzio amalizie, hilo hakuna.
================

CHADEMA uzeni sera na sio vitisho.

Hakuna aliyesema CHADEMA wamegewe dola kama peremende na wenyewe watafune.

Watu wanadai fair play, mashindano ya haki kwenye kutafuta dola.

CCM wanavunja sheria za ushindani, wanashika dola kinguvu.

Pikipiki za kampeni zinagawiwa kabla ya muda, fedha zinatapanywa kwenye kunyanyua mabango ya kumtangaza Samia kabla ya muda. Msemaji wa CCM Amos Makala katapika hadharani kwamba CCM inagawa pikipiki kwa ajili ya kampeni, hata hajui kama ni kuvunja sheria, upeo mdogo masikini ya Mungu.

Nchi ilifanya sherehe kubwa siku Kikwete lipopitisha sheria ya kuthibiti campaign financing. Yako wapi ? Mnakumbuka ? Wafuatiliaji wa mambo ya kitaifa ya nchi hii, mnakumbuka ?????

Sasa CCM tuambieni, mbona mnazivunja, mnanajisi, mnatemea mate sheria za campaign financing ????
 
Kupigiwaje kura!?

Unataka kusema kuwa hujui mwaka 2015 Jecha Salim Jecha alivyofuta uchaguzi wa Zanzibar kiharamu!!??

Umesahau vipi jinsi watendaji wa mitaa mwaka 2019 walivyosema eti wagombea wa CHADEMA nchi nzima kuwa hawajui kusoma na kuandika!?
Hapo sasa.
 
Ila hiki Chama Chetu pendwa cha CCM .....mmmmh. Jamii moja na ZANU PF ... wananchi maisha magumu Zimbabwe, pesa hakuna kila mwezi wanazibadili lakini majaa yamekomalia hapo hapo. Yaani ZANU PF na CCM ni kama Mapacha vile. Tabia zao zinashabihiana sana.
Uko sahihi.
 
Hakuna aliyesema CHADEMA wamegewe dola kama peremende na wenyewe watafune.

Wananchi wanadai fair play, mashindano ya haki, kwenye kutafuta dola.

CCM wanavunja sheria za ushindani, wanashika dola kinguvu.

Pikipiki za kampeni zinagawiwa kabla ya muda, fedha zinatapanywa kwenye kunyanyua mabango ya kumtangaza Samia kabla ya muda. Msemaji wa CCM Amos Makala katapika hadharani kwamba CCM inagawa pikipiki kwa ajili ya kampeni, hata hajui kama ni kuvunja sheria, upeo mdogo masikini ya Mungu.

Nchi ilifanya sherehe kubwa siku Kikwete lipopitisha sheria ya kuthibiti campaign financing. Yako wapi ? Mnakumbuka ? Wafuatiliaji wenzangu wa mambo ya kitaifa ya nchi hii, mnakumbuka ?????

Sasa CCM tuambieni, mbona mnazivunja, mnanajisi, mnatemea mate sheria za campaign financing ????
Yaani CCM wameamua kuiweka Rushwa ya Uchaguzi bila aibu.
 
Mlinganisho wako ni mlinganisho mfu.ANC wanakumbana na upinzani uliojipanga.DA waliwahi kutawala South Afrika,Zuma na Malema ni zao la ANC wanajua kujenga hoja za kufanya wachaguliwe licha ya kutoshinda.
Hapa Tanzania tuna wapinzani waganga njaa tu na kusema eti walishinda Urais 2020 ni wishful thinking.
Wapinzani wa Tanzania ni wakosoaji wa matukio bila sera mbadala za kiuchumi,mazingira na uhusiano wa kimataifa.
Lini ulisikia wame table bajeti mbadala na jinsi watakavyo finance hayo matumizi.
Hawa ni wafukuzia ruzuku tu ili kushibisha matumbo yao.Na hawana utamaduni wa kukubali kushindwa. Mfano Msigwa kashindwa lakini anadai kashinda.

Wewe hujui siasa za RSA unazisikia kwenye TV tu.

Hivi ni lini DA ilitawala South Africa. Au kwako ukiona chama cha wazungu tu assumption zako ndiyo chama kile kile cha De clark....!?

Anyway, hivi katika vyama EFF au MK unaviona ni vyama ....!? Jaribu kutofautisha movement na chama. Kwa RSA vyama ni ANC, IFP, DA may be na UDM. Vingine ni waganga njaa tu. Ndiyo maana kuna vyama zaidi ya 100. Kudai kuwa RSA wana vyama bora vya upinzani kuliko Bongo ni kukosa ufahamu tu kudharau Watanzania. Syestem yao ilikuwa designed in a way haisupport ukuaj wa vyama. Actually, itachukua muda mrefu sana huko mbeleni chama kimoja kutawala peke yake.
Mlinganisho wako ni mlinganisho mfu.ANC wanakumbana na upinzani uliojipanga.DA waliwahi kutawala South Afrika,Zuma na Malema ni zao la ANC wanajua kujenga hoja za kufanya wachaguliwe licha ya kutoshinda.
Hapa Tanzania tuna wapinzani waganga njaa tu na kusema eti walishinda Urais 2020 ni wishful thinking.
Wapinzani wa Tanzania ni wakosoaji wa matukio bila sera mbadala za kiuchumi,mazingira na uhusiano wa kimataifa.
Lini ulisikia wame table bajeti mbadala na jinsi watakavyo finance hayo matumizi.
Hawa ni wafukuzia ruzuku tu ili kushibisha matumbo yao.Na hawana utamaduni wa kukubali kushindwa. Mfano Msigwa kashindwa lakini anadai kashinda.

Mkuu, wewe hujui siasa za RSA unazisikia kwenye TV tu na kuzisoma kwenye magazeti tu. Yaani hii EFF inayoambulia 8 to 10 % kila uchaguzi unataka uilinganisha na vyama vya Tanzania!? EFF ambayo kila mwaka Wabunge wake wanatolewa kwa nguvu Bungeni kwa utovu wa nidhamu. EFF hawa wanaomtukana Rais wao Bungeni live kwenye Television ya Taifa. .... Au unazungumzia EFF ipi ... labda ya Namibia!!?

Halafu, ni lini DA ilitawala South Africa. Au kwako ukiona chama cha wazungu tu assumption zako ndiyo chama kile kile cha De clark....!?

Anyway, hivi katika vyama EFF au MK unaviona ni vyama ....!? Jaribu kutofautisha movements na vyama. Kwa RSA vyama ni ANC, IFP, DA may be na UDM. Vingine ni waganga njaa tu kuliko hata hivi vya Tanzania. Ndiyo maana kuna vyama zaidi ya 100. Kudai kuwa RSA wana vyama bora vya upinzani kuliko Bongo ni kukosa ufahamu tu kudharau Watanzania. Tatizo la Tanzania ni system mbovu ya uchaguzi na wizi wa kura wa chama tawala. kama uchaguzi ungeendeshwa kama RSA .... mbona CCM tayari ingelishakuwa history Bongo.

Kwa RSA, System yao ilikuwa designed in a way haisupport ukuaji wa vyama. Actually, itachukua muda mrefu sana huko mbeleni chama kimoja kutawala peke yake. Wazungu alitaka hiyo system ya PROPORTIONAL REPRESENTATION ili wajihakikishie kuwa wanakuwa represented Bungeni. Kama wangekuchua hii system kama yetu Tanzania Wazungu wasingonekana Bungeni na pia ingekuwa ni vigumu sana kuiangusha ANC.
 
Democratic Alliance pamoja na ku merge na vyama vingine kama Inkatha bado ni chama kile kile cha kulinda privileges za wazungu.Same old wine in a new bottle.
Hujagundua hivyo wewe ni naive na wishful thinker.
 
Wewe mtu unashida,nilini upinzani ulishinda CCM ikakataa kukabidhi madaraka!?,au unataka CCm isisimamishe kabisa mgombea ili isionekane imekatalia madarakani?
Mnasema hivi lakini kwa katiba hii ya kipuuzi mtakuja kuichoma hii nchi halafu katiba lenu la kipuuzi linazuia kupeleka mahakamani matokeo ya urais yaliyoibiwa ccm ndio italeta machafuko kwenye hii nchi kizazi cha wajinga wa vijijini kinaondoka wanabaki vijana wasiopenda upuuzi wenu wa kusifiana kijinga.
 
Ccm haichaguliwi ila mazingira yafuatayo ndio yanaifanya ijione inashinda ila hapana.
1. Kutumia dola ku supress upinzani.
2. Kutumia dola kuiba kura.
3.Kutumia wakurugenzi kama wasimamizi wa uchaguzi ambao ni makada wa ccm (rejea kauli ya magufuli nikulipe mshahara umtangaze mpinzani.
4. Katiba mbovu mfano kifungu kinachozuia matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani.
Juu ya hayo kuna mambo mengi ya ushetani yanafanywa na serikali ya ccm ili iendelee kubaki madarakani.
 
Back
Top Bottom