Vyama vinavyong'ang'ania madaraka kama CCM ndiyo huleta machafuko na mapinduzi Afrika

Vyama vinavyong'ang'ania madaraka kama CCM ndiyo huleta machafuko na mapinduzi Afrika

Wizi wa kura unaofanywa na CCM wakisaidiana na vyombo vya usalama ndio sababu hatuna uchaguzi huru,JPM aliiba kura za wabunge nchi nzima, wapinzani wanashinda sana na sio siri
Hizo ni propaganda tu zinazofanywa na walioshindwa. Kama ni kweli kura zimeibiwa unaenda mahakamani. Hata hivyo katika nchi zote zinazofanya Uchaguzi, Afrika, Ulaya, Asia na kwingineko, suala hili la kuibiwa kura huwa linaibuka. Na walioshindwa.

JPM ameikuta CCM. na Ameiacha.Wachaneni na siasa za majitope na kufukuzana na makaburi.

Wapinzani Tanzania wapo toka 1990's Magufuli alikuwepo kuwaibia kura huko nyuma. Narudia, kampeni zenu za kumlalamikia mtu mmoja ambaye hakuwa na moja ama mbili za siasa ni Uwenawazimu.

Fanyeni utafiti. Hizi lalama kuwa ni Afrika pekee ndimo kunapovurugwa kwa Uchaguzi ni Upotoshaji wa hali ya Juu.

Nani anajua Ujerumani na CDU wamekuwa huko tangia 1945? Merkel amekaa miaka mingapi?

Nani anajua Democrats wamekuwa na Uraisi kwa miaka mingapi kablabya Republicans kuchukua Urais?

Hawa wakina Allen Kilewella wanafanya Propaganda hasi za Kisaikilojia. Wanapandikiza uwongo na wakati huo huo wanakuza Ukuu wa Mzungu.

Fanyeni critical analysis.

Kama Faiza anavyouliza. Shuleni mlienda kusoma nini?
 
digba sowey umeona wenye matendo ya ki-CCM kama SYLLOGIST! alivyoandika???

Hivi kweli ukiwa na akili timamu unaweza kuuliza ni lini CCM ilikataa kushindwa!?
Mkuu, hakuna pahali nimesema CCM ilikataa kushindwa. Hata hivyo huo nao ni Upotoshaji.

Katika chaguzi za nyuma wapinzani walijaa Bungeni na katiik serikali za mitaa. Nikuulize CCM ilikataa kushindwa?
==============

Nikuambie hivi. Usichezee himaya yangu, utaumia mwenyewe. Haijalishi.

Nasema hivi, hamnitetereshi. Nitasema ukweli siku zote.
 
CCM haiwezi kutoka madarakani ikiwa wananchi bado wanaipigia kura,kutoka madarakni kwa ccm pale wananchi wataikataa
Imekataliwa mara nyingi na mara ya mwisho ni 2020.
Acha kujitoa akili ingawa huna akili,2020 tuliona mambo ya kutisha na ya aibu.
Vituo vingi vya kupigia kura vilikuwa na takwimu kama ifuatavyo
Waliokiandikisha mfano 179
Waliopiga kura 238
Kura zilizo haribika 2
Kura halali 573
Ccm kura 1596
Sasa huko ndiyo kukataliwa kwa ccm.
 
Imekataliwa mara nyingi na mara ya mwisho ni 2020.
Acha kujitoa akili ingawa huna akili,2020 tuliona mambo ya kutisha na ya aibu.
Vituo vingi vya kupigia kura vilikuwa na takwimu kama ifuatavyo
Waliokiandikisha mfano 179
Waliopiga kura 238
Kura zilizo haribika 2
Kura halali 573
Ccm kura 1596
Sasa huko ndiyo kukataliwa kwa ccm.
Asante sana mwanachaduma mwenzangu kwa taarifa sahih,kazi nzuri
 
Pikipiki za kampeni zinagawiwa kabla ya muda, fedha zinatapanywa kwenye kunyanyua mabango
Sawa Mkuu.

CHADEMA mna mabilionea kede kede. Kila mgombea aliyeshinda chaguzi, tumetaarifiwa na Erythrocyte kuwa ni BILIONEA. Hata mbowe ni BILIONEA l, itoshe mna TShs 2.7 bilion za ruzuku.

Mmekatazwa kununua piki piki. (Vifukuza upepo🤭)?

Mmekatazwa kuweka mabango? Kweli hayo?

Msitafute visingizio. Hela mnayo nankama CCM imetumia sheria zilizopwaya, mnashindwa nini?
 
Wewe hujui siasa za RSA unazisikia kwenye TV tu.

Hivi ni lini DA ilitawala South Africa. Au kwako ukiona chama cha wazungu tu assumption zako ndiyo chama kile kile cha De clark....!?

Anyway, hivi katika vyama EFF au MK unaviona ni vyama ....!? Jaribu kutofautisha movement na chama. Kwa RSA vyama ni ANC, IFP, DA may be na UDM. Vingine ni waganga njaa tu. Ndiyo maana kuna vyama zaidi ya 100. Kudai kuwa RSA wana vyama bora vya upinzani kuliko Bongo ni kukosa ufahamu tu kudharau Watanzania. Syestem yao ilikuwa designed in a way haisupport ukuaj wa vyama. Actually, itachukua muda mrefu sana huko mbeleni chama kimoja kutawala peke yake.


Mkuu, wewe hujui siasa za RSA unazisikia kwenye TV tu na kuzisoma kwenye magazeti tu. Yaani hii EFF inayoambulia 8 to 10 % kila uchaguzi unataka uilinganisha na vyama vya Tanzania!? EFF ambayo kila mwaka Wabunge wake wanatolewa kwa nguvu Bungeni kwa utovu wa nidhamu. EFF hawa wanaomtukana Rais wao Bungeni live kwenye Television ya Taifa. .... Au unazungumzia EFF ipi ... labda ya Namibia!!?

Halafu, ni lini DA ilitawala South Africa. Au kwako ukiona chama cha wazungu tu assumption zako ndiyo chama kile kile cha De clark....!?

Anyway, hivi katika vyama EFF au MK unaviona ni vyama ....!? Jaribu kutofautisha movements na vyama. Kwa RSA vyama ni ANC, IFP, DA may be na UDM. Vingine ni waganga njaa tu kuliko hata hivi vya Tanzania. Ndiyo maana kuna vyama zaidi ya 100. Kudai kuwa RSA wana vyama bora vya upinzani kuliko Bongo ni kukosa ufahamu tu kudharau Watanzania. Tatizo la Tanzania ni system mbovu ya uchaguzi na wizi wa kura wa chama tawala. kama uchaguzi ungeendeshwa kama RSA .... mbona CCM tayari ingelishakuwa history Bongo.

Kwa RSA, System yao ilikuwa designed in a way haisupport ukuaji wa vyama. Actually, itachukua muda mrefu sana huko mbeleni chama kimoja kutawala peke yake. Wazungu alitaka hiyo system ya PROPORTIONAL REPRESENTATION ili wajihakikishie kuwa wanakuwa represented Bungeni. Kama wangekuchua hii system kama yetu Tanzania Wazungu wasingonekana Bungeni na pia ingekuwa ni vigumu sana kuiangusha ANC.
Dah. Upo sawa Mkuu.

Mlinanganisho upo Sawa na CHADEMA. Just a movement!

Unaona CHADEMA kama chama?
 
CHADEMA. Just a movement!
Sometimes circumstances decide the fate. If you are in the banana republic country, what do you expect to come out of the jungle law system!??

So CHADEMA to be a movement organisation is just the situational fact. TANU and ASP was a movement Parties that's why today we have the historical event of Zanzibar revolution.
 
Leo nimeunganisha matukio ya vyama vikongwe vya siasa Afrika ambavyo vimeonesha weledi wake na kufanya nchi zao ziwe za kupigiwa mfano Afrika.

Chama cha kwanza ni chama cha United National Independency Party (UNIP) Cha Zambia ambacho kilitawala Zambia tangu mwaka 1964 hadi mwaka 1991.

Mwaka 1991 UNIP walishindwa uchaguzi dhidi ya chama cha Movement for Multparty Democracy (MMD) kilichokuwa kinaongozwa na Fredrick Chiluba.
Mpaka Leo Zambia kumetulia na UNIP wamekubaliana na matokeo.

Chama cha pili ni Kenya Africans National Union (KANU). Mwaka 2002 Muungano wa vyama vya siasa uliojulikana kwa jina la National Rainbow Coalition (NARC) ulishinda uchaguzi.

KANU wala hawakushughulika kupindua matokeo kama tabia ya CCM ilivyo wanaposhindwa uchaguzi. Maisha ya KANU huko Kenya yanaendelea na siasa zinasonga mbele.

Chama cha mwisho ni African National Congress (ANC) cha Afrika ya kusini.

Kwenye uchaguzi wa mwaka huu ANC imekataliwa na waafrika ya kusini. ANC wamepata asilimia arobaini (40%) wakati vyama vingine vimepata Asilimia sitini (60%).

ANC wala hawajifaragui kukubali matokeo badala yake wanatafuta kuunda Serikali na vyama vya siasa vingine walivyoshindana navyo kwenye uchaguzi.

Afrika nzima kwenye purukushani za mapinduzi na machafuko ni kule ambako vyama vilivyoko madarakani hukataa matokeo au mabadiliko.

CCM tabia yake ya kupora matokeo imewanogea hadi kwa Sasa hawaoni tena aibu kupora uchaguzi.

Walianza mwaka 1995 kule Zanzibar na baadae mwaka 2019/2020 wakaiba uchaguzi mzima.

Iko siku tabia hii ya kukataa kushindwa ya CCM italiletea Taifa letu madhara.

View: https://youtu.be/93uf0cMvExU?si=5UEY483BrEdOCs02
 
Screenshot_2024-11-12_205045.jpg
 
Hakuna namna. Si unaona CCM inavofanya uhuni kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa?
 
Back
Top Bottom