Vyama vinavyong'ang'ania madaraka kama CCM ndiyo huleta machafuko na mapinduzi Afrika

Napenda kukuhakikishia ya kuwa CCM itaendelea kusalia madarakani na kuongoza Taifa letu kwa kadri ya uhai wa Taifa hili. Hii ni kutokana na ubora wa sera zake zinazogusa maisha ya watu na kuwa na ajenda zinazoendana na mahitaji ya kila kundi pamoja na wakati.
 
Yaani kwa sera CCM ni bora kuliko ANC!?

hebu weka hapa sera hata moja ya CCM ambayo wewe unaona Bora!!
 
Yaani kwa sera CCM ni bora kuliko ANC!?

hebu weka hapa sera ya CCM ambayo wewe unaona Bora!!
CCM ndio chama kiongozi Barani Afrika.ndio chama kilichobeba matumaini ya watanzania na waafrika.ndio maana watu wengi sana huja kujifunza masuala mbalimbali hapa Nchini juu yakuendesha chama katika mfumo wa kitaasisi.angalia vyama dhaifu kama CHADEMA ambavyo uchaguzi tu wa ndani unawagawa na kuwasambaratisha.ona namna Msingwa alivyokuja hadharani kuongea mambo yaliyopaswa kuzungumzwa katika vikao.
 
🤣 🤣 🤣
 
🤣 🤣 🤣
 
Mjibu swali lake na siyo kuruka ruka hapa.Kwanini Mbowe yupo madarakani Muda wote? Huko CHADEMA hakuna watu wengine wenye uwezo wa kuongoza?
Hii siyo mada ya bandiko hili na wala haishabihiani na hoja yangu Kwa CCM.

Mifano nimetoa ya vyama vya siasa ila jamaa yako analeta mambo ya mtu binafsi

Kama ningekuwa nimetolea mfano wa Stephen Wasira badala ya CCM hapo ndipo ingekuwa sawa kuleta hoja ya Mbowe.
 
Jibu swali kwanini Mbowe amekaa muda mrefu kwenye uwenyekiti wake? Kwanini hamjambadilisha kwa kuchagua mwingine?
 
Mwaka 2025 CCM itashinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu. Hakuna chama cha kuiondoa CCM madarakani na Wajinga eti wataleta machafuko nchi hii watashughulikiwa ipasavyo!
 
Jibu swali kwanini Mbowe amekaa muda mrefu kwenye uwenyekiti wake? Kwanini hamjambadilisha kwa kuchagua mwingine?
Uelewa wako umeuweka ki-CCM Sana.

Ni sawa mtu aseme Yanga kwenye ligi ya mwaka 2023/2024 iliifunga Simba 5-1, halafu wewe useme "mbona Saido Ntibanzokiza amewahi kufunga goli 5 kwenye mechi moja!!??".

Sasa Yanga kuifunga Simba 5-1 kuna husiana vipi na Saido kufunga goli 5 kwenye mechi moja!!!

Au mnataka kumaanisha kuwa Mbowe ni sawa na CCM yote!!?
 
Acha kimalezi isiyo na sababu .wewe jibu swali kwanini Mbowe amekaa muda mrefu sana kwenye Uwenyekiti? Hakuna watu wengine wenye uwezo wa kuongoza huko CHADEMA?
 
Acha kimalezi isiyo na sababu .wewe jibu swali kwanini Mbowe amekaa muda mrefu sana kwenye Uwenyekiti? Hakuna watu wengine wenye uwezo wa kuongoza huko CHADEMA?
Nawezaje kujibu swali lisilo na mahusiano na bandiko hili!??

Kujibu ni kujiabisha kuonesha sijui nilichoandika.

Mabandiko kuhusu Mbowe humu Jf yapo mengi ya kutosha nendeni huko mkajadili.
 
Hizo nchi ulizozitaja zina vijana wanaojielewa si kama Tz ya akina mwashambwa ambao wanaongea kiurahisi tu.kenya huwezi kumrubuni mtu,wala Zambia au Malawi.Tz watu wanagongwa hadi bia moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…