Vyama vya Siasa nchini huu ndio wakati sahihi wa kutafuta ushindi wa kura za Uchaguzi wa Mkuu wa 2025, amkeni!

Vyama vya Siasa nchini huu ndio wakati sahihi wa kutafuta ushindi wa kura za Uchaguzi wa Mkuu wa 2025, amkeni!

Tunaitoa kwani iko madarakani kwa chaguzi halali? Labda tuwe na vikundi vya msituni maana yenyewe inawekwa madarakani na vyombo vya dola. Hivyo machafuko au mapinduzi ndio yataitoa maana hakuna uchaguzi Tanzania. Uchaguzi upo Kenya.

Basi waambieni wanaopinzana watulie wasipoteze muda
 
Hiyo ni ndoto ya wengi ila huwezi kuitoa CCM kwa vikaratasi.... Anayeuandaa Uchaguzi, Anayeusimamia na Anayetoa Matokea ndo huyo huyo mtu mmoja...

Ni kweli, vikaratasi haviwezi watoa CCM madarakani
Nguvu ya CCM ni kuwa na viongozi imara na wafuasi watiifu
Wakati udhaifu wa wapinzani ni uongozi dhaifu na wafuasi wa lazima

ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI
 
Ni kweli, vikaratasi haviwezi watoa CCM madarakani
Nguvu ya CCM ni kuwa na viongozi imara na wafuasi watiifu
Wakati udhaifu wa wapinzani ni uongozi dhaifu na wafuasi wa lazima

ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI
Kama kuna udhaifu kwenye hoja ni namna ile ile ya kupindisha ukweli kuwa uongo.Unahalalisha Uongo wa CCM katika taifa hili uonekane una uhalali katika ulimwengu wa sasa.Mlisema mikutano ya siasa inachelewesha maendeleo mkafanya kwa nguvu zote tena kubwa mkafunga watu,mkaua baadhi ya watu,mkatembeza vichapo kwa wabishi na mwisho wa yote mkatapeli Chaguzi za 2019 na 2020 ili uongo wenu uendelee kufanya kazi.Leo baada ya Uongo wenu kuonekana hauna faida kwa Watanzania mmeamuamua kuruhusu mikutano huku mkijipanga na Ushauri wa pumba pumba kama unavyofanya wewe na Paschal Mayala.
Ukweli utabaki pale pale kuwa hoja za Wapinzani zina nguvu kuliko za ccm.
 
Habari za asubuhi

Siku zinakwenda, mambo mengi yanabadilika, watanzania wanabadilika lakini hatari ni kwamba mifumo na miongozo ya vyama vingi vya siasa inabaki ileile ya kufanya mambo kwa mazoea.

Hivi, viongozi wa vyama vya siasa pinzani mlishawahi kujiuliza ni nini kipya mnaweza ambia wananchi au kufanya ili kuongeza thamani ya vyama vyenu huku mitaani? Mlishawahi kufanya tafiti kujua ni vitu gani wananchi wakipata watakua loyal kiasi cha kusimama kidedea na kuwalinda viongozi wao kwa hali na gharama yoyote na kuhakikisha msukumo wa kushinda uchaguzi unatoka kwao na sio kwenu?

Badala ya kutenga budget ya kwenda kutembea na kuwapa wananchi maneno matupu huko majimboni ili mjinufaishe nyie na familia zenu kwa hizo per diem, nufaikeni kidogo na wananchi mnaowatembelea wanaufaike kidogo. Mkono mtupu haulambwi. Watanzania wala hawataki mambo makuuuubwa, wnataka mambo madogomadogo yenye muendelezo

Msikurupuke makaendelea kufanya vitu vilivyokwishafanyika, sera zenu zinaweza kuwa nzuri sana ila sasa wekeni mipango itakayowapa wananchi imani kwamba sera zenu zinatekelezeka either kwa kuwashirikisha kwa vitendo au kuwapa connections muhimu au miongozo itakayogusa maisha yao.

Hakuna nchi nyepesi kuongoza na ngumu kuongoza kama Tanzania, ila kizuri na rahisi ni kwamba wepesi wa kuwaongoza watanzania unatokana na mahusiano ya kidugu mtakayokuwa mmeyajenga .

Msikurupuke mkawageza chama tawala CCM. Wenzangu hawa wana pa kusimamia tena sio padogo.... hawa wana cha kusemea sababu ndio wenye serikali na ndio watekelezaji wa mipango ya serikali.
Ingieni gharama kujenga vyama vyenu leo na baadae vyama hivi vitawajenga ninyi.

Halafu msilalamike kwamba hamna pesa ya kufanya mambo ya msingi sababu hata hayati Mwalimu Nyerere na Karume hawakuwa na pesa lakini walieweza kujenga vyama imara vilivyowaondoa wakoloni na vinavyowasumbua wapinzani hadi leo

Kama kweli mko kwaajili ya maendeleo ya taifa Amkeni ndugu zangu. Mkiendelea kufanya kilekile kinachowakoseshaga kila uchaguzi mtaendelea kukosa ushindi milele.

Rais wetu na mwenyekiti wa chama tawala ameshawaambia msisubirie msisubirie 2025 anzeni sasa. Mkumbuke pia na yeye ameshaanza kutetea kiti

Upinzani kwa afya ya taifa[emoji95]

Mungu ibariki Tanzania[emoji7][emoji1241][emoji1666]
USHAURI GANI HUU?

.............Ingieni gharama kujenga vyama vyenu leo na baadae vyama hivi vitawajenga ninyi............
 
Ni kweli, vikaratasi haviwezi watoa CCM madarakani
Nguvu ya CCM ni kuwa na viongozi imara na wafuasi watiifu
Wakati udhaifu wa wapinzani ni uongozi dhaifu na wafuasi wa lazima

ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI
Mwenyekiti aliona mbali sana, baada ya Uhuru aliona kabisa kuwa hizi kenge zitanisumbua akaamua kufuta MFUMO WA VYAMA VINGI akabaki kutuimbusha hilo PAMBIO ...

HALAFU baadaye anajifanya steringi wa picha 🤣🤣🤣 anafosi wenzake wauruhusu MFUMO WA VYAMA VINGI wakati ye ndo alifanya tuwe mazezeta kwa miaka 30..

Haya mambo ya KATIBA yanayoulizwa na akina MBOWE na Chama Cha Mkwewe katika Karne hii ya 21 ilibidi yaulizwe na akina ZUBERI MTEMVU wa ANC na wenzake katika Karne iliyopita 20.. Infact UPINZANI upo miaka 60 nyuma...

OfcoZ CCM ni suala lililo wazi kuwa wana UONGOZI ulio bora na IMARA ndo maana kwa miaka zaidi ya 40 hawajatetereka, ila bahati mbaya sana UIMARA wa huu UONGOZI umejikita kwenye kutaka kushika Dola kwa njia za kulaghai UMMA na si KUTATUA shida za WANACHI, hata MWENYEKITI naye kipaumbele chake kilikuwa ni KUKUZA chama na si ELIMU kwa WADANGANYIKA ili wasiamke kifikra...
 
Nini kinashindikana kuondoa hicho unachokiita " maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. " kama kipo kweli????

Kama kweli CCM haifai itoeni. Vinginevyo acheni kujiita wapinzani kumbe ni wanaSACCOs

Wanaume Mkwawa aliwaweza kwa wajerumani, Karume akiweza, Nyerere aliweza tena bila kulialia kama nyie mnalialia kutafuta excuses za kitoto mnooo

Sio ajabu hata hamjui mnachotaka

ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI

..natofautiana na wewe unapolinganisha changamoto alizopitia Mwalimu Nyerere na Tanu, na changamoto wanazopitia viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani.

..kwa kufupi ni kwamba Ccm na serikali yake ni MAKATILI kuliko wakoloni wa Kiingereza na vyombo vyao.

..Mfano mdogo chukulia idadi ya wafungwa na mahabusu wa kisiasa wakati huu wa utawala wa Ccm dhidi ya wakati wa mkoloni.

..Pia sijasikia au kusoma mahala popote kwamba Mwalimu Nyerere au viongozi wenzake wa Tanu walishambuliwa, au kudhalilishwa, na vyombo vya serikali ya mkoloni.

..Pamoja na kusema hayo, nakubaliana na hoja yako kwamba maadam mikutano imeruhusiwa basi vyama vya upinzani VIJIPANGE vilivyo kwa kuja na sera na kutoa elimu itakayoongeza hamasa kwa wananchi kuwaunga mkono.

..Na ushauri huu ili ufanikiwe ni lazima serikali na vyombo vyake iweke mazingira ya HAKI kwa vyama vyote vya siasa.
 
.......

Huwezi kulinganisha idadi ya wafungwa na mahabusu wa 1950s na 2020s bila kutupatia population za hivyo vipindi, bila kukokotoa hizi number huna uhalali wa kulinganisha

Mbinu za kudai uhuru 1950s hazina ulazima wa kufanana na za 2020s

Wacha niishie hapo😂😂😂😂
 
..hakuna ulazima wa kulinganisha population ya 1950s na sasa hivi kwasababu hakukuwa na wafungwa au mahabusu wa kisiasa kipindi cha mkoloni.
 
Uzi wa hovyo zaidi tangu mwaka huu uanze
 
..hakuna ulazima wa kulinganisha population ya 1950s na sasa hivi kwasababu hakukuwa na wafungwa au mahabusu wa kisiasa kipindi cha mkoloni.
Wapinzani wa sasa wengi ni wachumia tumbo na ili tupate mazingira sawa itabidi wapinzani wasubiri miaka 30 au50 ijayo hata Zambia,Malawi,Kenya nk awakusubiri Serikali iwawekee mazingira yaliosawa
 
Back
Top Bottom