Uchaguzi 2020 Vyama vya upinzani msipogomea uchaguzi 2020 bila tume huru tutawashinikiza sisi wanachama


Muhimu ni hiyo katiba mpya ya warioba
 
Kweli kabisa
 
Hakuna bora hapo kuchakachua ni kuchakachua tu.Wakijitokeza wengi itatengenezwa propaganda kwamba si unaona wananchi wanaunga mkono juhudi,ndo maana wamejitokeza kwa wingi kupiga kura.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana, hujanielewa nimeandika nini. Na kwa kuwa wewe ni "TruthLover" ni matumaini yangu utatulia na unisome kwa makini.

Wanaojitokeza kwa wingi kupiga kura ni kwamba wamehamasishwa na wanatambua maana ya kura zao.

Hawa hawakubali kuporwa haki yao ya kuwachagua viongozi wao. Watasimama kidete kutetea haki hiyo.

Hili halitokei/halijatokea kwa sababu watu hawajahamasishwa kukataa kunyang'anywa haki hiyo. Na wakiwa wengi hakuna mwenye uthubutu wa kuwazuia wasiidai haki hiyo.

Tume haiwezi kuwa na uthubutu wa kuchezea kura za watu (wengi) wenye hamasa ya kuilinda haki yao.

Sasa kama bado hunielewi, sina njia ya kukuelewesha.

Labda uje na swali jingine, ambalo ni hao watu hamasa hiyo wataitoa wapi? Jibu pia nimekwishaligusia kwenye yale niliyoandika mwanzo.
 
Kudai tume huru ya uchaguzi sio kosa kudai mabadiliko ya katiba sio kosa baada ya maumivu ya jiwe na CCM yake kwa miaka 5/10 hatuko tayari kabisa kumpata jiwe mwingine kwa miaka kumi ijayo !! Never shall that be allowed to happen!!! It is an oath!!!

Naunga mkono hoja post yako namba moja. Upinzani kushiriki uchaguzi huu wenye mazingira ya kishenzi ni kupoteza muda. Mimi nilipendekeza waanze hilo mwezi machi, ila hata wakianza sasa hawana la kupoteza. Na hata wakisema watashiriki, sisi wapiga kura wao hatutajuandikisha kupiga kura. Sasa ni wakati sahihi, hatuko tayari tena kwa chaguzi za kishenzi.
 

Ni hivi kalamu 1, kwenda kushiriki chaguzi ambazo hujuma ziko wazi ni kupoteza muda. Tudai tume huru kwa nguvu zote, na tuonyeshe taifa na dunia hakuna uchaguzi bali ubatili. Ni bora kutokushiriki uchaguzi kuliko kushiriki uchaguzi ambao watu wataishia kupata vilema.
 
Hili ni swala tofauti, kama nakuelewa.

Na kama ni hivyo ninavyokuelewa ulichoandika, sina shaka ya kuunga mkono hoja yako. Nitakubaliana nawe kama hivyo unavyopendekeza ndivyo itakavyokuwa.

Mimi ninavyokuelewa ni hivi. Nisahihishe kama nakosea.

Hakuna uchaguzi wa aina yoyote utakaofanyika bila ya kuwepo "Tume Huru."

Je, hiyo ndiyo maana yake?
Utekelezaji/uzuiaji wa uchaguzi wa aina yoyote ya uchaguzi usifanyike unawezekana?


Nitashukuru sana ukiyajibu haya.

Niseme wazi, yote mawili, yaani:
1) kuhimiza wananchi wakapige kura kwa wingi; na
2) hili la "kuzuia uchaguzi usifanyike bila ya kuwepo Tume Huru,)
Yote ni kazi ngumu sana inayowakabila vyama vya upinzani na asasi zote zinazopigania haki kuyatimiza. Ni kazi ngumu ambayo nimekuwa nikiihimiza CHADEMA waifanye kwa bidii huko mitaani, mtu kwa mtu, na mlango kwa mlango.

Hii sio kazi rahisi tu ya kukurupukia siku/miezi kadhaa kabla ya kufanyika uchaguzi.

Ni kazi ngumu, lakini ni kazi inayofanyika kwa viongozi walio na 'determination' ya kuifanya kwa ufanisi.
 
Hata sijui tatizo lipo wapi. Kwamba inakuwa vigumu sana kulieleza hili jambo lieleweke vizuri.

Aina yoyote ya uchaguzi utakaofanyika chini ya 'Tume ya Uchaguzi' iliyopo sasa uchaguzi huo unakabiriwa na uchakachuaji. Hili sote tunakubaliana juu yake.

"Uchakachuaji" utakuwa rahisi zaidi kuufanya kwa wapiga kura wengi kutojitokeza kwenda kupiga kura kwa hiari yao wenyewe.
Hii ni faida kubwa sana kwa CCM.

Na kama wapiga kura wamesusa kwenda kupiga kura, wakabaki tu wanapiga makelele huko nje ya utaratibu wa kupiga kura, hizi kelele hazina maana yoyote kwa mshindi wa uchaguzi huo wa kuchakachua.

Tofautisha hali hiyo na hii hapa chini:

"Uchakachuaji" utakuwa mgumu kufanywa na "Tume ya Uchakachuaji" kama mamilioni ya wapiga kura watajitokeza na kupiga kura zao, na huku wakionya bila ya kificho, kwamba kura zao zikichakachuliwa hapatatosha.

Hawa wengi waliojitokeza kupiga kura, kura zao ushahidi upo, unaonekana hata kama uchakachuaji utafanyika. Na wakikataa kunyang'anywa haki yao, suluhu ipo wazi kwa kuangalia tu kura zilizopo, na sio zisizokuwepo ambazo walizisusia wenyewe.

Sijaandika mahali popote kutowashirikisha watu wengine, mashirika mbalimbali na hata Jumuia za Kimataifa kuunga juhudi za wananchi hawa wakiongozwa na viongozi wao kukataa kuporwa haki yao ya msingi; haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka wao wenyewe.

Sasa, unapoweka na vitisho vya "kupewa vilema", hapo ndipo unapomaliza kabisa na kuwakatisha tamaa hata hao ambao wako tayari kutetea haki zao!
 
mada za kumkashf magu zmetosha sasa: haiwezekan kila kuamka na kulala ni negatives tu kwan hakuna mazuri yamefanyika? kwan kua upinzani inamaanisha unatakiwa kuangalia upande wa negatives tu?


cha ajab zaidi upinzani bado sana kushika nchi, jamaaa anawekeza nguvu kubwa vijijini maaana ndo kwenye watu wengi nyie mnawekeza nguvu online! this is purely bullshit
 
Cha kusikitisha si Chadema wala chama chochote kinachoonyesha kuwa na mikakati ya kudai tume huru let alone katiba mpya. Vyama havina political strategists, wanafanya tu vitu kwa mazoea.
Bila tume huru, na mimi nasisitiza sitasimama juani eti kusubiri kupiga kupiga kura. Siwezi kuwapa legitimacy wapuuzi wanaotutesa miaka na miaka.Wafanye uhalifu wao but not under my name.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…