Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Hata sijui tatizo lipo wapi. Kwamba inakuwa vigumu sana kulieleza hili jambo lieleweke vizuri.
Aina yoyote ya uchaguzi utakaofanyika chini ya 'Tume ya Uchaguzi' iliyopo sasa uchaguzi huo unakabiriwa na uchakachuaji. Hili sote tunakubaliana juu yake.
"Uchakachuaji" utakuwa rahisi zaidi kuufanya kwa wapiga kura wengi kutojitokeza kwenda kupiga kura kwa hiari yao wenyewe.
Hii ni faida kubwa sana kwa CCM.
Na kama wapiga kura wamesusa kwenda kupiga kura, wakabaki tu wanapiga makelele huko nje ya utaratibu wa kupiga kura, hizi kelele hazina maana yoyote kwa mshindi wa uchaguzi huo wa kuchakachua.
Tofautisha hali hiyo na hii hapa chini:
"Uchakachuaji" utakuwa mgumu kufanywa na "Tume ya Uchakachuaji" kama mamilioni ya wapiga kura watajitokeza na kupiga kura zao, na huku wakionya bila ya kificho, kwamba kura zao zikichakachuliwa hapatatosha.
Hawa wengi waliojitokeza kupiga kura, kura zao ushahidi upo, unaonekana hata kama uchakachuaji utafanyika. Na wakikataa kunyang'anywa haki yao, suluhu ipo wazi kwa kuangalia tu kura zilizopo, na sio zisizokuwepo ambazo walizisusia wenyewe.
Sijaandika mahali popote kutowashirikisha watu wengine, mashirika mbalimbali na hata Jumuia za Kimataifa kuunga juhudi za wananchi hawa wakiongozwa na viongozi wao kukataa kuporwa haki yao ya msingi; haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka wao wenyewe.
Sasa, unapoweka na vitisho vya "kupewa vilema", hapo ndipo unapomaliza kabisa na kuwakatisha tamaa hata hao ambao wako tayari kutetea haki zao!
Narudia tena kalamu1, kuliko wananchi kuendelea kupata vilema huku tume ikiendelea kuwa ile ile, huko ni kupoteza wakati, bora tume iwe huru kisha watu walinde kura zao kutoka mashinikizo mengine nje ya tume. Sio watu wapige kura kwa wingi, kisha tume imtangaze waliyeagizwa na mwenyekiti wa ccm, halafu vyombo vya dola vipokee amri ya kuwaua na kuwatia vilema wasiokubali kuporwa kura. Tume ikiwa huru tutahamasisha watu kupiga kura, na sio kinyume chake.