Vyombo vya habari Tanzania vimethibitisha aliyoyasema Lissu

Vyombo vyetu vya habari vingekuwa huru, Wewe ilibidi uwe Mwandishi na mtangazaji nguli nchini.

Yaani mtu wa kufukunyua yaliyonyuma ya pazia kwa maslahi ya Taifa.

Sema ndio hivyo njaa haina baunsa.
 
Kulialia nako kunachosha.

Inaeleweka kwa kila mwenye akili, kwamba nchi yetu ipo chini ya utawala wa kidikteta usiovumilia ushindani wa aina yoyote.

Kama unatambua hilo kwa nini uendelee kulialia na kulalamikia hivyo vyombo unavyojua havina uhuru wala utashi wa kufanya unayoyategemea?

Jambo mhimu la kufanya katika hali inayoeleweka hivyo ni kufanya kila juhudi za kufikisha ujumbe kwa walengwa kupitia njia mbadala ambazo dikteta hana uwezo wa kuzizuia.

Kitu mhimu hapa ni ujumbe ufike kwa walengwa, sio aina ya njia ujumbe huo utakavyofika huko.

CHADEMA wanajua wazi wamefungiwa hivyo vyombo wasiwafikie wananchi; waache kulialia na kutafuta huruma. Ni kazi yao kutafuta njia za kuufikisha ujumbe.
 
Nani anaetaka kuwa airtime kikundi Cha wahuni?
 
Unataka watangaze Ushoga??
 
Wakati mmoja rais wa sasa wa Zimbabwe alikuwa makamu wa Rais hivyo akafutwa kazi na mh Mugabe na kuundiwa zengwe ili afungwe na wammalize.Usiku uliooangwa tukio lifanyike alidokezwana baadhi yawatuwa usalama ikabidiatoroke kwa kutaka kukodi ndege ya private lakini wahindi waliokuwa wanaimiliki ile ndege walikataa kwa madai kuwa wanamuogopa Mugabe na uhusiano wao utateteleka.Basi Mh Mnangagwa ambae ni Rais wa sasa akavalishwa baibui na kutoroka kwa shida akipitia safari ngumu ya taabu Hadi msumbiji na baadae South Africa.Hivi sasa ndiye Rais wa Zimbabwe kwa sasa sijui itakuaje kwa wale wahindi waliomnyanyasa wakati alipokuwa na shida.
 
Kijana angaika na maisha yako achana na maisha ya wanasiasa ambao wakishapata madaraka wanawafikria ndugu zao kwanza.
 
Tutatoa eyataymu kesho kuanzia magazeti yetu na tv. Habari za msingi kwa leo zilikuwa zimejaa.
 
Kwani mbowe ni CCM mbona anaitaga waandish wa habari na wanakuja wa vyombo vyote tatizo tundulisu akipewa maiki anaanza kutukana na kutaja watu majina badala ya kuongea kilicho mpelekea waandish wa habari hawawez kupoteza muda wao kumsikiliza chizi alifikir atakiki maskin ujinga wake umezid kufika mbali
 
Hilo la Lissu kushinda halimo kabisa katika akili zao, ndio maana ya haya yote wanayofanya.

Wao wamejipa uhakika kwamba hawawezi 'kushindwa' kwa njia yoyote.

Ndio maana huko unakokusema "...wataanzaje kumuomba msamaha" hawakufikirii, kwa sababu wanajua haitatokea washindwe, na iwalazimu kuomba msamaha.

Hata ikitokea kwamba iwalazimu kusalimu amri kwa matakwa ya wananchi, sioni kamwe mtu wa kuomba mwingine msamaha hapo.

Sioni jinsi anayoweza Magufuli kuanza kumwomba Lissu msamaha. Huyu sio mtu wa kuomba msamaha, yeye ni mtu wa kuombwa msamaha tu kwa kulazimisha, hata ambao hawana sababu ya kuomba msamaha kwake, na hata aliowakosea yeye mwenyewe, analazimisha wamwombe yeye msamaha. Huyo sio mtu wa kuomba asamehewe.

Itabidi alazimishwe kufanya hivyo kwa aibu kubwa sana mbele za jamii.
 
That's why nilishaacha kuangalia tv zote nchini bora nimfuatilie kigooooo
 
Hivyo ni viidara tu vya kipropaganda kwa madhumuni maalum vya kiswahili (kiingereza kwa VOA) vya hao BBC, VOA na DW ambazo hurushwa kwa nchi walengwa na siyo dunia nzima.
 
Maccm hawajafanya tambiko lao (Mwenge)wamekwishaa
 
Ndugu's sometime mue mnatumia ubongo, hivi ITv na vyombo vingine vikipigwa faini hua mnavisaidia kulipa?? Vikifungiwa leseni hua mnafanya nn??
Watz sio watu wakuwapigania kwasababu hawajitambui so acha kulaumu vyombo laumu raia wasiojali kile kinachoendelea
 
We'll said Bro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vyombo vyetu vya habari vingekuwa huru, Wewe ilibidi uwe Mwandishi na mtangazaji nguli nchini.

Yaani mtu wa kufukunyua yaliyonyuma ya pazia kwa maslahi ya Taifa.

Sema ndio hivyo njaa haina baunsa.
Mkuu ebu acha kejeri aisee
 
Wanaogopa bill za tra
Kodi walikwepa huko nyuma
 
Mleta mada hujielewi Wala Huelewi utaratibu unaotakiwa kuufuata ili uwe mbashara kwenye TV. Na nilichogundua unasumbuliwa na stress za Chama+familia na ndo Maana unabwabwaja tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…