Tetesi: Vyombo vya habari vya kimataifa vyaanza kuwasili Tanzania kuelekea Sep 1(UKUTA)

Halafu kwa taarifa yenu hao wamekuja shuhudia kupatwa kwa jua wapate cha kuandika kwao sio hayo mnayofikiri yatatokea Not in Tanzania God bless us
 
Yani mtu unaota ICC hii iliyomgwaya Kinyata? Ndio unataka kutwambia Magu ataenda icc? Kwa lipi?

Kuweni wakweli jamani!
 
wenzako wanakuja kuangalia TUKIO LA KIHISTORIA LA KUPATWA KWA JUA ama wenyewe wanaita SOLAR ECLIPSE
 
Mfumo wa kuongoza Nchi usiufananishe na mfumo wa kuongoza Familia ...
Logically the child analogy has similar syllogism to CDM political behaviour; thus requiring similar shaping approach.

Uwezi kupata kila kitu kila saa its simple; na tabia hizo zikiendekezwa uwafanya watu waamini mambo ndio yanavyofanyika someone has to make a stop.
 
Sasa siasa ni hoja, je wapinzani waitolee wapi kama mikutano yote imepigwa marufuku? Mtafutano wooote huu ni kuwa watu wamezuiwa kutoa hoja na wameamriwa kuwa mazezeta hadi 2020.
Si kweli kinachopingwa ni campaign type of politics watu awawezi zunguka nchi nzima kupinga serikari iliyoko madarakani halafu wakaachwa sio Tanzania tu nchi yoyote siasa hizo uisha baada ya uchaguzi au kulazimisha kuonyeshwa kwa bunge live wakati hayo ni maamuzi ya serikari wasubiri washinde warudishe lakini si kulazimisha ni haki yao.
 
H
Nafikiri huwajui wazungu na hufikiri sawa sawa hujaona waandishi kwenye maeneo yenye vita kali kuliko hii nchi km Syria, Iraq, Libya.. japo sina uthibtisho wa ujio huo wa waandishi
 
fikirieni nje ya box tarehe 1 sept kuna kupatwa kwa jua kwanini msiseme wanakuja ili kuchuku tukio hilo??hivo vyombo vya kimataifa vilishindwa kuweka kambi yao zanzibar ambako hali mpaka sasa ni tete ndo waje leo kisa tu ya ukuta??acheni upuuzi nyie...........
 
wakifukuzwa mgogoro utakuwa mkubwa zaidi
Hivi kuna mgogoro gani
na nani hasa
ni yupi wa kukaa naye Meza moja ?
CUF wamesambaratika
UKAWA wamewaondoa CUF katika umoja wao
waliobaki ni CHADEMA
kwa hiyo CHADEMA ndio UKUTA?
basi waandamane wao km wanatikisa kiberiti cha gesi
wasitusingizie Watanzania wengine
wao wanataka tu kutawala kabla ya 2025 kabla fedha ua UFISADI haijaisha
 
Reactions: bdo

Wangeruhusiwa kupanda majukwwani wananchi wachuje kati ya pumba na mchele. Pili serikali ingeweza kuwakamata na kuwafungulia mashtaka ya kuikashifu serikali na uchochezi. Hili lingeruhusiwa, wala hakuna mwananchi yeyote ambaye angepoteza muda wake kuandamana kwa ajili ya watu walioshtakiwa kwa mujubu wa sheria za nchi. Kinachogomba kwa sasa ni makatazo ya jumla bila kufuata sheria.
 
Chadema tunapita kwenye tanaru la moto,
Lakini Mungu haijawah kuliacha kundi lake lunaloshikilia ukweli liaibike mbele ya wadhalimu/ccm
 
Mfumo wa kuongoza Nchi usiufananishe na mfumo wa kuongoza Familia ...[/QUOTE
si majuzi mulikiwa unatumia mfano wa nchi kama familia mlipokuwa mnamkosoa Rais Kikwete?
 
Hao wanaofikiri Tanzania ni Yemen wameptea. Waende Iraq na Syria kwa matukio yao walikofanikiwa kupandikiza chuki. Uzuri hapa vyama vyote vimegoma kuunga uhuni wa chadema wa kutumiwa na walewale wanaotaka tuendelee kuwa masikini.
 
Watu wanafanya uchaguzi kwa sababu ya kupata 'political mandate' ya kuongoza nchi kutokana na namna sahihi kwao wao, mbinu zao, ilani yao etc. Na kufanikisha hilo inataka kuongoza jamii iliyo na amani na mshikamano.

Sasa aina maana kila maamuzi yatawapendezea watu wote lakini aiondoi uhalali waliopata kidemokrasia kufanya yale waliyodhamiria katika muda waliopewa na katiba. Kama ukubali kuna njia halali za kuponda sera za serikari yes kipindi hiki upinzani kazi yao ni kukosoa tu sio kuzuia maamuzi ya serikari iliyo namamlaka halali.

Kwa dhana hizi mikutano ya hadhara, au campaign za kutaka watu waandamane kuishinikiza serikari ni siasa ambazo azikubaliki duniani kwa mtindo wa demokrasia. Uamini subiri tarehe 1 uone kama kuna mtu atashutumiwa; wewe uwezi kugoma, utoke bungeni halafu utunge uongo wako utake kuusambaza kwenye mikutano ya hadhara huko sasa ndio kuchekeana na kukubali watu wakuaribie kazi uliyoipata kikatiba.
 
Hao wazungu wanataka kumjaribu wambie hajaribiwi
 
Wacha waje hakuna shida.. mbona 2015 October 25 walikuja tele pia kwa matumaini hayo hayo waliokuja nayo sasa na mwisho wa siku wakaishia kuripoti mastaajabu yao ya hali ilivyokuwa kinyume na matarajio yao...
Tutaendelea kuwashangaza tena kama ilivyo ada na watarudi kama walivyokuja, sana sana watakua wamekuja kutalii kwa bajeti ya mabosi wao..

TZ yetu watuachie wenyewe... hatuendeshwi kwa hisia wala vichwa vya wendawazimu...
Non of the unthinkable will ever happen on this mother land..
 
H
Nafikiri huwajui wazungu na hufikiri sawa sawa hujaona waandishi kwenye maeneo yenye vita kali kuliko hii nchi km Syria, Iraq, Libya.. japo sina uthibtisho wa ujio huo wa waandishi
UKUTA sio global news, ukilinganisha na kupatwa kwa jua. Kupatwa kwa jua kunako tarajiwa has been covered kwenye hivyo media na makala kibao duniani ili hali huo UKUTA unaandikwa na Tanzania Daima, Mtanzania labda kidogo sana na Mwananchi.

Hizo criss za Libya and et al huwezi ukaringanisha na huu upupu wa akina nanilio, hadi mtu apewe DSA ya kuja kuandika kitu ambacho hakina maana, sawa na maigizo.

In fact sioni kama kutakuwa na maandamano, never hayatakuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…