saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,683
- 7,222
Kichwa cha habari chahusika.
Vyuo vikuu binafsi nchi hii ambavyo vingi vinamilikiwa na taasisi za dini wanalipa wahadhiri wao mishahara midogo sana. Huwezi amini mishahara ni midogo kuliko hata walimu wa shule za sekondari. Kwa mfano Mhadhiri msaidizi analipwa Tsh Milioni moja kabla ya makato.
Mbaya zaidi wengine wamekaa na mishahara hii kwa miaka zaidi ya 20, wengine 15 na wengine 10. Waajiri wa hivi vyuo hawajui kitu kinaitwa nyogeza ya mshahara.Hata hii nyogeza ya mama Samia hawataongeza maana nyogeza nyingi zilishapita hasa kipindi cha JK lakini wao haikuwahusu.
Kiukweli wafanyakazi wanaishi kama watoto yatima hakuna wa kuwasemea, Siyo idara ya kazi wala Wizara yenyewe. Wafanyakazi wa umma wao wana wazazi hawa hawana. Lakini tukumbuke wanaofanya kazi kule ni watanzania na wanafunzi wanosoma vile vyuo ni watoto wetu wa kitanzania. Kwanini Serikali kupitia vyombo vyake haifuatilii hivi vyuo?
Naomba serikali itembele hivi vyuo ikaone hali halisi na iwasaidie wahadhiri wale ktk unyanyasaji huu mkubwa. Ifuatilie ipate ukweli wahadhiri wamekaa miaka zaidi ya 20 bila nyongeza yoyote.
Hata THTU haina habari maana haina matawi ktk vyuo vingi. Jamani wahusika timizeni wajibu wenu kuwasaidia watanzania wenzenu.