Vyuo vikuu vyote jirekebisheni kuna namna mmepotoka kidogo.

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
16,911
Reaction score
28,469
I salute you kinsmen.

Kuna kasumba imekuwa kubwa taratibu sana, nahisi hali hii TCU ndio wameleta

Sikuhizi wanafunzi wamekuwa wengi na ufaulu nao umeongezeka sana
Maelfu wanamaliza form six kila mwaka na wote wanataka kwenda chuo.

Sasa TCU kama baba wa vyuo vyote na mlezi
Anaruhusu vipi vyuo.viweke strictly qualification and minimum entry?

Sikuhizi vyuo almost vyote wanataka wenye division 1 tu tena ile.kali kabisa kabisa.

Nimeshuhudia madogo wengi wakikosa vyuo mfano kwa chuo kimoja kikubwa hapa Dodoma. mtoto mwenye 1.5 Law amekosa

Sababu vyuo vingi sasa vimepandisha qualification sana na wakati wanajua serikali inazalisha wahitimu wa form six wengi kila mwaka je waende wapi??

Ni kweli vyuo viko independent kujiendesha lakini lazima vifuate sheria na procedure kutoka TCU

hapo Morogoro nako kuna chuo kikubwa tu kinapinga sana panga wanafunzi hata wenye wenye 1 nzuri tu nao wanapigwa panga.

matokeo yake hata vyuo vidogo navyo vinaiga utaratibu huu huu wa kuchuja sana wanafunzi bila sababu za mashiko

Kwa sasa form six kama mwanao ameshindwa kupata division 1 basi usitegemee kama atasoma chuo cha ndoto zake.

kwa mantiki unaelewa kwanini Wenye pesa hupeleka watoto wao nje wakasome.

Karibu wanafunzi zaidi ya elfu 10 nchi nzima wanamaliza kila mwaka na je waende wapi ikiwa kila chuo kinataka wenye 1 tu?

Na hata wenye hiyo 1 wanapigwa panga sana?

Mwanzo ilikuwa wanaangalia ufaulu wa mwaka huo lakini hii sio moja ya condition tena maana sikuhizi madogo wanafuulu sana one zipo kama uchafu .

Lakini asilimia kubwa wanakosa vyuo wanavyoomba au kozi husika na wengine kuamua kubaki nyumbani mwaka mzima

hasa hasa kozi za afya vyuo vimekuwa na kasumba hii. Kuna chuo kipo Dar kimekuwa na tabia hii kwa miaka mingi sana

Na tunapolekea sio pazuri hata kidogo.

Wenu mdau wa elimu
Its Pancho

Sababu ni kuwa
 
Nadhani sababu ni competition tu Mkuu

Kila chuo kina capacity yake ya idadi ya wanafunzi wanaoweza kupokea na kuwahandle kwa kila kozi so ni kawaida hata kwa huyo mwenye 1.5 kukosa hapo ikiwa walioomba wengi wana vijiti vya point 3 na 4

Kuna Madogo wamegusa division 2 nawafahamu na wamepata nafasi pale Mlimani vizuri tu mwaka huu
 
Unaogopa nini kutaja UDOM, SUA, na MUHAS?
hadi unazunguka sana hivyo? Shida ni hiyo 1 kuwa nyingi, si mnaona sifa kufaulisha hovyo, matokeo yake ndio hayo.
Elewa vizuri hata kama hawafaulishi bado wangefaulu tu

Elimu ya sasa tofauti na zamani ambapo kitabu kimoja shule wanafunzi 10

Sikuhizi shule zina teaching and learning materials za kutosha na technology kubwa zaidi material online mengi sasa kwanini wasipate one?

Zaidi ni kuwa population imeongezeka sio kama kama miaka ile so huwezi kuzuia hilo

Shida je hawa wenye hizi one wanaenda wapi? Na vyuo vinachuja sana?
 
Nadhani sababu ni competition tu Mkuu

Kila chuo kina capacity yake ya idadi ya wanafunzi wanaoweza kupokea na kuwahandle kwa kila kozi so ni kawaida hata kwa huyo mwenye 1.5 kukosa hapo ikiwa walioomba wengi wana vijiti vya point 3 na 4

Kuna Madogo wamegusa division 2 nawafahamu na wamepata nafasi pale Mlimani vizuri tu mwaka huu
Sasa hujanipa solution ya tatizo ni nini?

Ufaulu mkubwa? Au nini?

Nimeeleza wazi kuhusu competition haipaswi kuwa kigezo tena miaka hii maana kama 1.3 zimejaa sana na bado wanakosa tu madogo unadhani kuwe na procedure zipi ili kuhakikisha vijana wengi waliomaliza hawakai nyumbani?
 
Elewa vizuri hata kama hawafaulishi bado wangefaulu tu

Elimu ya sasa tofauti na zamani ambapo kitabu kimoja shule wanafunzi 10

Sikuhizi shule zina teaching and learning materials za kutosha na technology kubwa zaidi material online mengi sasa kwanini wasipate one?

Zaidi ni kuwa population imeongezeka sio kama kama miaka ile so huwezi kuzuia hilo

Shida je hawa wenye hizi one wanaenda wapi? Na vyuo vinachuja sana?
Waende VETA, kwani hawakusikia Waziri mkuu mstaafu alisema wazi wazi.
 
Mie sikukataliwa wala kuchujwa kwenye kujiunga na chuo kikuu, ndio maana sikwenda VETA.
😂😂😂
waziri alichomaanisha ni kuwa vijana waache kukimbilia vyuoni tu

Badala yake waende VETA
Sasa wewe tunajua hujamaliza chuo siku nyingi ni hapo majuzi kati miaka hii hapa ya kati

Hivyo ulitakiwa kwenda VETA tu na sio ku apply chuo hapo UD🤣
 
Sasa hujanipa solution ya tatizo ni nini?

Ufaulu mkubwa? Au nini?

Nimeeleza wazi kuhusu competition haipaswi kuwa kigezo tena miaka hii maana kama 1.3 zimejaa sana na bado wanakosa tu madogo unadhani kuwe na procedure zipi ili kuhakikisha vijana wengi waliomaliza hawakai nyumbani?
Suluhisho hapo ni serikali iboreshe vyuo vyetu vya umma kwa kupanua miundombinu ya vyuoni na kuongeza idadi ya Lecturers and other staffs ili kuweza kuaccommodate nyomi la wanafunzi wanaomaliza form six kwa sasa

Ila tatizo pia watoto wanataka kusoma vyuo vyenye majina makubwa wakati vyuo kama SAUT,RUCU etc..... vina uhitaji mkubwa wa wanafunzi
 
Sasa hujanipa solution ya tatizo ni nini?

Ufaulu mkubwa? Au nini?

Nimeeleza wazi kuhusu competition haipaswi kuwa kigezo tena miaka hii maana kama 1.3 zimejaa sana na bado wanakosa tu madogo unadhani kuwe na procedure zipi ili kuhakikisha vijana wengi waliomaliza hawakai nyumbani?
Suluhisho ni serikali kuongeza idadi ya vyuo kukidhi mahitaji. Tanzania tunazaliana mnoo na vyuo vilivyopo havikidhi idadi yetu. Kila mwaka la saba wanaomaliza wako 1M+. Kati ya hawa 1M+, wale watakaofanikiwa kumaliza form six, je kuna vyuo vya kutosheleza idadi yao??
 
Mkuu,chuo kinachukua wanafunzi kulingana na uwezo ( capacity). Mfano kozi fulani chuo kina uwezo wa kuchukua wanafunzi 10, wanaomba waombaji 1000 , chuo lazima kichukue wale wenye one za 3 pekee kati ya hao maana ndo itakuwa haki imetendeka. Au unataka chuo kichukue wanafunzi idadi kubwa kuliko uwezo wa chuo??
Twende taratibu mkuu
Kuhusu competition nimeongelea hapo wazi kabisa.

Zaidi ni kuwa sio chuo kimoja tu almost vyote huwa wanafanya hivyo now fuatilia.

Hapo UDOM wanafunzi wamekuwa wakitumia ujanja huu
Mfano aliomba law akachaguliwa course nyingine anaconfirm akifika chuo wakati wa registration kuna dirisha la kuomba kuhama kozi

Analipa 50k anahama anaenda tena huko law ambako wanasema pamejaa na anakubaliwa .

Unadhani hiyo imekaaje
 
Suluhisho ni serikali kuongeza idadi ya vyuo kukidhi mahitaji. Tanzania tunazaliana mnoo na vyuo vilivyopo havikidhi idadi yetu. Kila mwaka la saba wanaomaliza wako 1M+. Kati ya hawa 1M+, wale watakaofanikiwa kumaliza form six, je kuna vyuo vya kutosheleza idadi yao??
Sawa lakini ukweli ni kuwa population nayo imeongezeka na unajua wazi watu ndio labour power popote pale

Population yetu sidhani kama inafikia ya USA lakini wote wanasoma tu wanapotaka kulingana na qualification zao

Hapa ina maana kuwa ni moja

Vyuo vingi miundombinu imezidiwa kuliko uhalisia wake halisi! Sindio?

Na vingine havitaki kukubali hilo na kujiupdate badala yake wanajificha kwenye kichaka cha minimum entry
 
Twende taratibu mkuu
Kuhusu competition nimeongelea hapo wazi kabisa.

Zaidi ni kuwa sio chuo kimoja tu almost vyote huwa wanafanya hivyo now fuatilia.

Hapo UDOM wanafunzi wamekuwa wakitumia ujanja huu
Mfano aliomba law akachaguliwa course nyingine anaconfirm akifika chuo wakati wa registration kuna dirisha la kuomba kuhama kozi

Analipa 50k anahama anaenda tena huko law ambako wanasema pamejaa na anakubaliwa .

Unadhani hiyo imekaaje
Hapo siwezi kuongelea mkuu, mimi chuo nilichosoma watu hawakukubaliwa kuhamia au kubadili kozi hata iweje kama maksi zako ziko chini ya maksi ambazo wanafunzi wengine waliochaguliwa hiyo kozi walifikisha. Mfano kama umepata one ya 8 ila unataka kuhamia kozi ambayo walichaguliwa watu wenye one ya 3-6, chuo kiligoma kata kata,watu walitumia kila mbinu ila ilishindikana. Huo utaratibu wa UDOM siwezi kuongelea.
 
Sawa lakini ukweli ni kuwa population nayo imeongezeka na unajua wazi watu ndio labour power popote pale

Population yetu sidhani kama inafikia ya USA lakini wote wanasoma tu wanapotaka kulingana na qualification zao

Hapa ina maana kuwa ni moja

Vyuo vingi miundombinu imezidiwa kuliko uhalisia wake halisi! Sindio?

Na vingine havitaki kukubali hilo na kujiupdate badala yake wanajificha kwenye kichaka cha minimum entry
Mkuu, hapo US kaangalie idadi ya vyuo vyao na uwezo wake. Mfano chuo kikuu cha jimbo la Arizona kina uwezo wa kuchukua wanafunzi wa vyuo vingapi hapa Tanzania?.
 
Hapo siwezi kuongelea mkuu, mimi chuo nilichosoma watu hawakukubaliwa kuhamia au kubadili kozi hata iweje kama maksi zako ziko chini ya maksi ambazo wanafunzi wengine waliochaguliwa hiyo kozi walifikisha. Mfano kama umepata one ya 8 ila unataka kuhamia kozi ambayo walichaguliwa watu wenye one ya 3-6, chuo kiligoma kata kata,watu walitumia kila mbinu ila ilishindikana. Huo utaratibu wa UDOM siwezi kuongelea.
Hata UDOM pia ni hivyo huwezi kubadili kama huna proper entry qualification

Ila wenye vigezo ndjo huwa wanabadili na wanapata ingawa panasemwa kuwa pamejaa mkuu
 
Back
Top Bottom