Vyuo vikuu vyote jirekebisheni kuna namna mmepotoka kidogo.

Vyuo vikuu vyote jirekebisheni kuna namna mmepotoka kidogo.

Mkuu, hapo US kaangalie idadi ya vyuo vyao na uwezo wake. Mfano chuo kikuu cha jimbo la Arizona kina uwezo wa kuchukua wanafunzi wa vyuo vingapi hapa Tanzania?.
Kwa maana hiyo miundombinu ya vyuo vingi ni imezidiwa au kupitwa na idadi ya sasa na hawajaboresha

Imagine course moja wanachukua wanafunzi 10
 
Angalia kozi za afya hapo nilipotolea mfano mkuu

Wapi utapata kwa division 3?
Hata hiyo 1.5 wanakosa sembuse 3?

Je binti huyo aliomba nini hasa?
Kozi za afya mfano Muhas kuna kozi wanachukua wenye división one ya 3 pekee maana unakuta hiyo kozi chuo kina uwezo wa kufundisha wanafunzi 20 pekee. Wakizidisha hiyo idadi,TCU watawapiga rungu.
 
waziri alichomaanisha ni kuwa vijana waache kukimbilia vyuoni tu

Badala yake waende VETA
Sasa wewe tunajua hujamaliza chuo siku nyingi ni hapo majuzi kati miaka hii hapa ya kati

Hivyo ulitakiwa kwenda VETA tu na sio ku apply chuo hapo UD🤣
😂😂😂 nimeshamaliza mda sana.
Waambie ukweli madogo waende VETA, kuhusu chuo kwa mlolongo huo watakaa sana home.
😂😂😂
 
Suluhisho hapo ni serikali iboreshe vyuo vyetu vya umma kwa kupanua miundombinu ya vyuoni na kuongeza idadi ya Lecturers and other staffs ili kuweza kuaccommodate nyomi la wanafunzi wanaomaliza form six kwa sasa

Ila tatizo pia watoto wanataka kusoma vyuo vyenye majina makubwa wakati vyuo kama SAUT,RUCU etc..... vina uhitaji mkubwa wa wanafunzi
😂😂😂 hili nalo muhimu.
 
Kozi za afya mfano Muhas kuna kozi wanachukua wenye división one ya 3 pekee maana unakuta hiyo kozi chuo kina uwezo wa kufundisha wanafunzi 20 pekee. Wakizidisha hiyo idadi,TCU watawapiga rungu.
Kwa maana hiyo miundombinu yao michache kufundisha zaidi ya hao 20?
 
Kwa maana hiyo miundombinu ya vyuo vingi ni imezidiwa au kupitwa na idadi ya sasa na hawajaboresha

Imagine course moja wanachukua wanafunzi 10
Ndo uwezo wao ulipofikia mkuu, wafanyeje?. Mfano pale Muhas main campus( kama ushawahi kufika) pale ni padogo sana, hawawezi kuchukua wanafunzi wengi. Sasahivi ndio maana wameenda kujenga campus nyingine Kigoma huko.
 
Si kweli, kuna binti wa rafiki yangu, amepata div 3, HGE na vyuo vyote 5 alivyoomba alipata; Ardhi, IFM, SAUT,MUCO, Mwenge.
​
Unaelewa maana ya competition? Course alzioomba hazina ushindani ndo maana yani div 3 serious wakati mwaka juzi tu hapo 2 kupata chuo ni mtiti labda ukasome beekeeping
 
Suluhisho hapo ni serikali iboreshe vyuo vyetu vya umma kwa kupanua miundombinu ya vyuoni na kuongeza idadi ya Lecturers and other staffs ili kuweza kuaccommodate nyomi la wanafunzi wanaomaliza form six kwa sasa

Ila tatizo pia watoto wanataka kusoma vyuo vyenye majina makubwa wakati vyuo kama SAUT,RUCU etc..... vina uhitaji mkubwa wa wanafunzi
Shida ndio hiyo

Lakini pia vyuo vingi vimeshazidiwa uwezo wa kupokea wanafunzi bado wanaishi enzi za miaka ya nyuma ambapo wasomi walikuwa wachache
 
Angalia kozi za afya hapo nilipotolea mfano mkuu

Wapi utapata kwa division 3?
Hata hiyo 1.5 wanakosa sembuse 3?

Je binti huyo aliomba nini hasa?
Kwa baadhi ya vyuo ushindani ni mkubwa sana, na hii inatokana na ukubwa wa miundombinu kwa chuo husika kuchukua wanafunzi.
Mfano; Chuo x kina uwezo wa kuchukua wanafunzi 500, hakitaweza kuzidisha ata mmoja, kama waombaji ni wengi, watakachofanya ni kuchukua wale 500 wenye ufaulu mkubwa kuliko wengine.
Kama ndoto yako ni kusoma fani fulani, si lazima hiyo fani ukasomee chuo fulani tu, unaweza pia kuipata chuo kingine.​
 
Shida ndio hiyo

Lakini pia vyuo vingi vimeshazidiwa uwezo wa kupokea wanafunzi bado wanaishi enzi za miaka ya nyuma ambapo wasomi walikuwa wachache
Hilo ni jukumu la wizara maana wana takwimu za idadi ya wanafunzi wanaohitimu kila mwaka na idadi ya vyuo .
 
Sasa nani hataki kusoma chuo chenye jina jamani😂😂😂. Nani hataki kwenda chuo cha Dar??.
Nimekumbuka class letu advance, kila mtu anataja UDSM, na kweli wanafunzi karibu robo 3 waliingia UDSM, wachache sana wakaenda DIT na MUST.
😂😂😂😂
 
Unaelewa maana ya competition? Course alzioomba hazina ushindani ndo maana yani div 3 serious wakati mwaka juzi tu hapo 2 kupata chuo ni mtiti labda ukasome beekeeping
Maisha ni sanaa, kuna wengine ni viongozi ata mlango wa chuo kikuu hawajakanyaga. Muhimu hapa, ni kutafuta fani isiyo na ushindani, kama unataka fani yenye ushindani tafuta vyuo mbalimbali na si kutegemea kwenye chuo kimoja unachokitaka wewe.
Vinginevyo, utajikuta miaka yako yote ni kulalamika huku umri ukikimbia.
 
Haya mambo tangu hapo yalikuwepo. Mfano wakati ninajiunga Udsm cutting point ya Sheria ilikuwa ni division 1.7 na course nyingine kwa ujumla wake ilikuwa mwisho ni division II.12
 
Sasa nani hataki kusoma chuo chenye jina jamani😂😂😂. Nani hataki kwenda chuo cha Dar??.
Badala yake eti waende VETA wakati yeye mwenyewe hapo majuzi kati kamaliza UD

Kweli uchawi muombee mwenzako🤣
 
I salute you kinsmen.

Kuna kasumba imekuwa kubwa taratibu sana, nahisi hali hii TCU ndio wameleta

Sikuhizi wanafunzi wamekuwa wengi na ufaulu nao umeongezeka sana
Je; Kuongezeka kwa huo ufaulu ni ule Ufaulu wa kweli au ni ufaulu wa wa kutumia mbinu batili?
Maelfu wanamaliza form six kila mwaka na wote wanataka kwenda chuo.
Kumaliza form six sio kufaulu form six.

Sasa TCU kama baba wa vyuo vyote na mlezi
Anaruhusu vipi vyuo.viweke strictly qualification and minimum entry?
Ndo kazi yake. TCU wapo vizuri kwenye hilo na bado wanatakiwa waviheshimishe vyuo vyote vya hapa Tz.
Sio kijana anatoka chuo hana utofauti na yule ambaye hakuenda chuo bali alikwenda kwenye vyuo vingine.
Sikuhizi vyuo almost vyote wanataka wenye division 1 tu tena ile.kali kabisa kabisa.
Safi kabisa. Chuoni sio unaenda kuchukua Deg. bali unaenda kusoma masomo kiwango stahiki cha Deg.
Nimeshuhudia madogo wengi wakikosa vyuo mfano kwa chuo kimoja kikubwa hapa Dodoma. mtoto mwenye 1.5 Law amekosa
Sawa. Kama wapo wenye 1.0 hamsini(50) na darasa linauwezo wa wanafunzi 30 sioni kwanini wahangaike na huyo wa 1.5.
Sababu vyuo vingi sasa vimepandisha qualification sana na wakati wanajua serikali inazalisha wahitimu wa form six wengi kila mwaka je waende wapi??
Mbona pa kwenda ni pengi tuu? Vyuo vipo vingi, Taasisi za kielimu zipo nyingi hata veta nao wapo.
Ni kweli vyuo viko independent kujiendesha lakini lazima vifuate sheria na procedure kutoka TCU
Sheria na procedures kutoka TCU ndo hizo - kuweka chujio kali.
hapo Morogoro nako kuna chuo kikubwa tu kinapinga sana panga wanafunzi hata wenye wenye 1 nzuri tu nao wanapigwa panga.

matokeo yake hata vyuo vidogo navyo vinaiga utaratibu huu huu wa kuchuja sana wanafunzi bila sababu za mashiko
Like father, like son. Mkuu; laiti ungelipita-pita huko vyuoni ukajionea yanayoendelea huko -Ungeshangaa.
Kwa sasa form six kama mwanao ameshindwa kupata division 1 basi usitegemee kama atasoma chuo cha ndoto zake.
Akijitahidi katika hio ndoto yake ataweza. Lakini hii ya kufuata mkumbo na kukwepa kozi ngu ndo hilo. Zamani walisema unaenda kusoma nguini (masomo ya Arts) ili upate Deg at room temperature.
kwa mantiki unaelewa kwanini Wenye pesa hupeleka watoto wao nje wakasome.
Sawa lakini kama ingekuwa sio kimchongo-mchongo ; hao wanaorudi kutoka nje wakipewa ile Qualifying Exam. wengi wao wanafeli jumla.
Karibu wanafunzi zaidi ya elfu 10 nchi nzima wanamaliza kila mwaka na je waende wapi ikiwa kila chuo kinataka wenye 1 tu?
Mbona pa kwenda ni kwingi tu broo? Hata Upolisi ???
Na hata wenye hiyo 1 wanapigwa panga sana?
Ni swali zuri sana esp. ukizingatia hapo juu nimesema sio wote wanaomaliza F6 wamefaulu. Huko shuleni zipo mbinu nyingi sana za udanganyifu. Kijana tangu ameanza A-level, kwenye continuous assement ni mwendo wa C,D, halafu leo ghafla bin vuu anapata A National Exam. Lazima ujiulize.
Mwanzo ilikuwa wanaangalia ufaulu wa mwaka huo lakini hii sio moja ya condition tena maana sikuhizi madogo wanafuulu sana one zipo kama uchafu .
Ndo hizo Fake.
Lakini asilimia kubwa wanakosa vyuo wanavyoomba au kozi husika na wengine kuamua kubaki nyumbani mwaka mzima
Hiyo ni hiari yake. Sio lazima kijana aende chuo.
hasa hasa kozi za afya vyuo vimekuwa na kasumba hii. Kuna chuo kipo Dar kimekuwa na tabia hii kwa miaka mingi sana
Yes; Kongole kwao. Hakuna binadamu wa kuchezewa-chezewa Afya yake na vijana wanaoshinda huko Tiktok.
Na tunapolekea sio pazuri hata kidogo.
Kwa sasa unaweza kusema hivyo lakini siku likikukuta la kutokana na kupata huduma ya Wahitimi substandard (Not competent) waliotoka vyuoni utaelewa. Siku hizi Taaluma imekaa kisiasa zaidi kitu ambacho ni hatari kubwa kwa mustakabali wa Uhai na Ustawi wa jamii pia kwa Maendeleo ya Taifa letu.
Wenu mdau wa elimu
Its Pancho

Sababu ni kuwa
Pancho; I am Sorry for the disturbing reactions
 
Haya mambo tangu hapo yalikuwepo. Mfano wakati ninajiunga Udsm cutting point ya Sheria ilikuwa ni division 1.7 na course nyingine kwa ujumla wake ilikuwa mwisho ni division II.12
Lakini mbaya zaidi now wanafunzi wameshakuwa wengi sana na bado cutting points ni hizo hizo tu
 
Nimekumbuka class letu advance, kila mtu anataja UDSM, na kweli wanafunzi karibu robo 3 waliingia UDSM, wachache sana wakaenda DIT na MUST.
😂😂😂😂
Umeona ee, wote mkaenda vyuo vyenye majina. Halafu sasahivi umwambie kijana eti aende TEKU kwa sababu hata TEKU ni chuo😂😂😂
 
Back
Top Bottom