Je; Kuongezeka kwa huo ufaulu ni ule Ufaulu wa kweli au ni ufaulu wa wa kutumia mbinu batili?
Kumaliza form six sio kufaulu form six.
Ndo kazi yake. TCU wapo vizuri kwenye hilo na bado wanatakiwa waviheshimishe vyuo vyote vya hapa Tz.
Sio kijana anatoka chuo hana utofauti na yule ambaye hakuenda chuo bali alikwenda kwenye vyuo vingine.
Safi kabisa. Chuoni sio unaenda kuchukua Deg. bali unaenda kusoma masomo kiwango stahiki cha Deg.
Sawa. Kama wapo wenye 1.0 hamsini(50) na darasa linauwezo wa wanafunzi 30 sioni kwanini wahangaike na huyo wa 1.5.
Mbona pa kwenda ni pengi tuu? Vyuo vipo vingi, Taasisi za kielimu zipo nyingi hata veta nao wapo.
Sheria na procedures kutoka TCU ndo hizo - kuweka chujio kali.
Like father, like son. Mkuu; laiti ungelipita-pita huko vyuoni ukajionea yanayoendelea huko -Ungeshangaa.
Akijitahidi katika hio ndoto yake ataweza. Lakini hii ya kufuata mkumbo na kukwepa kozi ngu ndo hilo. Zamani walisema unaenda kusoma nguini (masomo ya Arts) ili upate Deg at room temperature.
Sawa lakini kama ingekuwa sio kimchongo-mchongo ; hao wanaorudi kutoka nje wakipewa ile Qualifying Exam. wengi wao wanafeli jumla.
Mbona pa kwenda ni kwingi tu broo? Hata Upolisi ???
Ni swali zuri sana esp. ukizingatia hapo juu nimesema sio wote wanaomaliza F6 wamefaulu. Huko shuleni zipo mbinu nyingi sana za udanganyifu. Kijana tangu ameanza A-level, kwenye continuous assement ni mwendo wa C,D, halafu leo ghafla bin vuu anapata A National Exam. Lazima ujiulize.
Ndo hizo Fake.
Hiyo ni hiari yake. Sio lazima kijana aende chuo.
Yes; Kongole kwao. Hakuna binadamu wa kuchezewa-chezewa Afya yake na vijana wanaoshinda huko Tiktok.
Kwa sasa unaweza kusema hivyo lakini siku likikukuta la kutokana na kupata huduma ya Wahitimi substandard (Not competent) waliotoka vyuoni utaelewa. Siku hizi Taaluma imekaa kisiasa zaidi kitu ambacho ni hatari kubwa kwa mustakabali wa Uhai na Ustawi wa jamii pia kwa Maendeleo ya Taifa letu.
Pancho; I am Sorry for the disturbing reactions
Safi sana mkuu nimependa analysis yako kisomi sana
Lakini unadhani VETA ni solution ikiwa system yetu haijaandaa mazingira rafiki kwa vijana wanaoenda huko kusoma technical skills?
Tumeshuhudia wengi wao wamesoma huko VETA lakini uwezeshwaji umekuwa duni.
Nchi za wenzetu wametengeneza system nzuri ya kuwawezesha vijana kama hao huku hakuna.
Pia.mashinikizo kutoka kwa family
Hakuna mzazi atakubali mwanaye mwenye 1.7 anende VETA mkuu sidhani.
Natambua kozi za afya zinahitaji watu competent sana maana afya ya mtu ni muhimu .
Ina maana kuwa ufaulu huu wa sasa ni feki mkuu?.
Mimi naona bado tunaforce kuishi dunia ya kale ambapo
Teaching materials zilikuwa chache
Shule zilikuwa chache zaidi
Walimu walikuwa wachache pia
Moreover online materials nazo zilikuwa chache tofauti na sasa hapo lazima wafaulu mkuu au unasemaje?
TCU wanapiga chujio kali sana kwa vyuo vya sasa lakini swali linabaki kuwa ni wote wenye 1 ni ufaulu feki?
Kama wapo waliofaulu kiuhalali wakakosa nafasi na wakapata ambao walifaulu ufaulu "fake" tunaosemea inakuwa kosa la nani?
Asante