I salute you kinsmen.
Kuna kasumba imekuwa kubwa taratibu sana, nahisi hali hii TCU ndio wameleta
Sikuhizi wanafunzi wamekuwa wengi na ufaulu nao umeongezeka sana
Maelfu wanamaliza form six kila mwaka na wote wanataka kwenda chuo.
Sasa TCU kama baba wa vyuo vyote na mlezi
Anaruhusu vipi vyuo.viweke strictly qualification and minimum entry?
Sikuhizi vyuo almost vyote wanataka wenye division 1 tu tena ile.kali kabisa kabisa.
Nimeshuhudia madogo wengi wakikosa vyuo mfano kwa chuo kimoja kikubwa hapa Dodoma. mtoto mwenye 1.5 Law amekosa
Sababu vyuo vingi sasa vimepandisha qualification sana na wakati wanajua serikali inazalisha wahitimu wa form six wengi kila mwaka je waende wapi??
Ni kweli vyuo viko independent kujiendesha lakini lazima vifuate sheria na procedure kutoka TCU
hapo Morogoro nako kuna chuo kikubwa tu kinapinga sana panga wanafunzi hata wenye wenye 1 nzuri tu nao wanapigwa panga.
matokeo yake hata vyuo vidogo navyo vinaiga utaratibu huu huu wa kuchuja sana wanafunzi bila sababu za mashiko
Kwa sasa form six kama mwanao ameshindwa kupata division 1 basi usitegemee kama atasoma chuo cha ndoto zake.
kwa mantiki unaelewa kwanini Wenye pesa hupeleka watoto wao nje wakasome.
Karibu wanafunzi zaidi ya elfu 10 nchi nzima wanamaliza kila mwaka na je waende wapi ikiwa kila chuo kinataka wenye 1 tu?
Na hata wenye hiyo 1 wanapigwa panga sana?
Mwanzo ilikuwa wanaangalia ufaulu wa mwaka huo lakini hii sio moja ya condition tena maana sikuhizi madogo wanafuulu sana one zipo kama uchafu .
Lakini asilimia kubwa wanakosa vyuo wanavyoomba au kozi husika na wengine kuamua kubaki nyumbani mwaka mzima
hasa hasa kozi za afya vyuo vimekuwa na kasumba hii. Kuna chuo kipo Dar kimekuwa na tabia hii kwa miaka mingi sana
Na tunapolekea sio pazuri hata kidogo.
Wenu mdau wa elimu
Its Pancho
Sababu ni kuwa