Waandishi Wa Habari Mmetia Aibu Kwenye Press Baada Ya Mchezo Wa Young Africans Na Mamelod Sundowns

Rahi❌
Rai✅
 
Sio waandishi wa habari tu sector zote... Mbona madaktari wanapasua wagonjwa vichwa baada ya miguu🙄🙄. Afu kiingereza sio lugha mama yetu. Hatuitaki asee.
Wekeni basi wakalimani kama wanavyofanya ulaya. Mchezaji kama Messi hajui kingereza ila anahojiwa kila siku na utakuta kuna mkalimani anatafsiri.

Niliona press ya benchikha baada ya mechi unamuona kabisa kuna vitu anataka kuvieleza watu wamuelewe ila kingereza chake si kizuri. Kwanini wasimuwekee mkalimani ili aongee kifaransa au kiarabu ili watu wamuelewe vizuri?
 
Hata hao watangazaji wa Azam Tv ni vichwa maji vilevile mfano ni patrick Nyembera na mwenzake Gift Macha unaona kabisa wanaunga unga lugha ya kingereza na maswali yao hayana mantiki ndio maana wanashindwa kumuhoji benchikha baada ya game za simba kwenye ligi
 
......mbona malalamiko, kwani wameulizaje, wengine hatujafuatilia mahojiano, tuwekeeni video tushee hiyo fedhea, au lugha imekuwa changamoto hadi wametukana, anyway kingereza wengi wetu kinatushinda hata tuliobahatika kwenda shule.......
Yale Yale ya uvivu wa mtanzania,nenda YouTube utayakuta mahojiano
 
Heheheee! Hakuna watu vilaza kwenye tasnia ya habari kama waandishi wa habari za michezo, ingawa tasnia nzima ina vilaza wengi ila wa michezo wamezidi sana
 
Mimi nilikuwa nasikia aibu kila swali la hovyo likulizwa, mpaka ikabidi kubadili channel
 
waandishi wengi bongo ni wapenzi wa vilabu vya Simba na Yanga, na mara nyingi huwa wana panga vikosi vyao na kulinganisha na kikosi cha kocha 🐒

na saa zingine wanakasirika kabisaaaa akipangwa fulani na fulani akaachwa bench, na ghadhabu zao ndio hua msingi wa maswali yao baada ya mechi 🐒
 
Ukisemacho ni kweli,nadhani pia paangaliwe wanakopikwa ( vyuoni) maana ni wengi wanaogubikwa na tatizo hili.
Nadhani hawatambui km ni kazi bali wanaona km ni njia ya kuwapeleka kwenye teuzi za u DC.
 
Waandishi wenyewe kina PASCHAL MAYALA natania tu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nilikuwa najiandaa kuleta uzi wenye maudhui sawa na yako,Kwa kweli ni aibu tupu mpaka Gamondi anamshangaa muandishi wa habari Kwa aina ya swali alilouliza
Na kwenye kimombo sasa...
Mzize ni mzigo sana, hili swali lilikuwa valid.
 
Si ndio hao hao walio mleta mtoto feki wa lulu diva hakuna kitu hapo!
 
duh sijaona aliuliza swali gani to get Gamond scorched kumuuliza mwandishi?
Mwandishi wa habari aliuliza kwanini amemuazisha kijana Mdogo Mzize na kumuacha Joseph Guede mkomavu na mwenye uzoefu na Michuano mikubwa, wakati wa mkutano wa Waandishi wa habari baada ya mchezo.

"Mzize ni 'Future' ya Tanzania sio Yanga tu, sasa atapataje uzoefu kama hapati nafasi ya kucheza, mbona kacheza vizuri sana, katengeneza nafasi nyingi, kukosa ni kawaida kwa washambuliaji, au hujaona alichokifanya, wewe ni mwandishi wa habari nadhana una uelewa wa mambo kuliko shabiki, sasa unaulizaje swali kama shabiki, aya nami nikuulize yule Peter Shelulile wa Mamelod Sundowns katengeneza nafasi ngapi?" - Gamondi.
 
Elimu ndio shida tutalaumiana sana ila kuwa na elimu duni Kuna waumiza sana watanzania Nina uhakika hata wewe kazi Yako japo sijui lakini unaifanya kwa kiwango Cha chini sana shida ni elimu na mazingira ya kazi
Kweli mkuu, ni muhimu tujiendeleze kutafuta maarifa sahihi.
 
Nilivyoona mwandishi wa kike anajitambulisha NI kutoka Manara TV kabla ya kujibiwa nikaona palepale press yenyewe yote haina maana yoyote kama waandishi wenyewe ndio hao.

Nimemkumbuka Abdullah Majura na Ndolanga, jana Ndolanga angekuwa ndio kocha angewatukana hawa waandishi.

Mimi nadhani level zao ni kuwahoji kina Ahmed Ally ili wapewe Majibu ya comedy kama Al Sahaf au Masau Bwire ndio wanaendana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…