Wanabodi,
Humu jukwaani tuko watu wa fani mbalimbali na miongoni mwao ni sisi watu wa fani ya habari.
Leo nimewakumbuka waandishi wa habari na kupotea/vifo vya kutatanisha, toka kwa Stan Katabalo, Ben Saanane, Azory Gwanda, Daudi Mwangosi, Josephat Isango, maajaliwa ya hatma za maisha yao, ni ama tuombe Mungu atunusuru na dhahama hizo, ama...
Ukiwa mwandishi wa habari wa kawaida tuu au mtangazaji wa kawaida tuu ni kazi kama kazi nyingine zozote, lakini ukiwa ni mwandishi wa habari za uchunguzi au mtangazaji machachari unayehoji maswali magumu, kiukweli wasomaji wako na watazamaji wako watakusifu sana kwa kazi nzuri, ila majaaliwa ya maisha yako na familia yako ni ya mashaka sana na wengi huwa na mwisho mbaya ambao hauzungumziki.
Tukianzia kwa mwandishi wa kwanza wa habari za uchunguzi nchini Tanzania, Stan Katabalo wa gazeti la Mfanyakazi aliyeibua kashfa ya Loliondo, alikufa kifo cha ghafla, japo alisifiwa sana kwa ushujaa na mpaka kesho jina lake bado linavuma kwenye list ya mashujaa wa habari Tanzania, lakini sijui kama kuna waandishi au vyama vya habari wanajua chanzo cha kifo chake, au kaburi lake linafanana vipi au majaaliwa ya familia yake baada ya kifo cha baba mwenye nyumba.
The same applies to Azory Gwanda na Ben Saanane wetu humu JF, yamebaki majina na mabandiko tu humu hakuna ajuaye hatima yao nini kiliwakuta, lakini sisi wanajamii vikiwemo vyama vya habari, japo tuliwasifu sana wakati wakileta habari za moto moto, lakini baada ya kutoweka, hakuna tena anayejali wala kujua tuu majaaliwa ya familia zao.
Nimelileta bandiko hili baada ya kumkumbuka mwandishi wa habari machachari Josephat Isango aliyefariki tarehe ya jana mwaka 2018, baada ya kuugua ghafla, hakuna media wala chama cha habari kilicho jishughulisha kubaini chanzo cha kuugua ghafla kwake na baada tuu ya maziko, sifa na pongezi zake zinaishia hapo makaburini kwa waandishi, vyama vya habari na vyama vya siasa kuweka mashada makubwa ya maua, kisha kusoma risala nzuri ya jinsi marehemu alivyokuwa mwandishi shujaa, then all ends up there and then.
Mimi nilifahamiana na Josephat Isango kwa kuunganishwa nae na mtangazaji nguli Angalieni Mpendu kupitia kipindi cha Jicho Letu Ndani Ya Habari mwaka 2015.
Kisha tukaja kukutana Siku ya Uhuru wa Habari Morogoro then Mwanza na kote akihadithia jinsi anavyo windwa na wenye mamlaka.
Hadi kifo chake, sikupata kusikia alikufa kwa nini au chanzo cha kifo chake kama ilivyo kwa Stan Katabalo, ila kiukweli sisi waandishi wa habari za uchunguzi na watangazaji wa maswali magumu, tuna wakati mgumu sana kwenye maisha yetu.
Hivyo wanabodi, tunaposifina humu kwa maswali magumu kama yale ya Ben Saanane, tusiishie kusifiana tuu humu bali tuangalie na hatma za maisha yetu na familia zetu, hivyo ikitokea mtu aliyekuwa very critical on the status quo, ghafla akageuka na kuanza kuunga mkono juhudi, nawaombeni sana muwaelewe watu wa aina hii ambao hawaangalii leo au sasa bali wanaangalia kesho na kuangalia mbali.
Tuombeni sisi watu wa media tumalize salama hatma za maisha yetu na ikitokea yakakatishwa ghafla, wale ambao ni rafiki zetu wa kweli wa kufa na kuzikana, tuushie kwenye mashada na risala za wasifu, bali angalau fuatilieni na majaaliwa ya familia zetu.
RIP Wanahabari wote waliotangulia mbele ya haki na Mungu uwanusuru wale waliopotea bila sisi kujua hatma zao, na utajaalie moyo wa ufuatiliaji kujua majaaliwa ya familia zao.
Paskali
Baadhi ya mada za Isango
Naomba mjadala wa wazi na Zitto kuhusu usaliti ndani ya chama - JamiiForums
Je, ni sahihi kwa CHADEMA kumzika Josephat Isango kwa taratibu za chama? - JamiiForums
Waandishi wa habari kuvaa sare za vyama kama huyu Gerson? - JamiiForums
TANZIA: Mwandishi wa habari, Josephat Isango afariki dunia; Azikwa Kisasida, Singida - JamiiForumsé
Josephat Isango (Tanzania Daima) ashtakiwa, adaiwa mil.500 - JamiiForums
Josephat Isango, Mhariri wa Habari Tanzania Daima akamatwa na Polisi - JamiiForums
Josephat Isango: Natoa Shukrani kwa wote - JamiiForums
Tanzia: Josephat Issango afiwa na baba yake. - JamiiForums