Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...

Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...

Dah mkuu Pascal Mayalla umeongea ukweli mchungu.

sisi Watanzania sisi wengi wetu ni mafisi (cowards) wa kupindukia, kujiita makondoo (dociles) ni kujipa sifa tusizostahili!
 
Daaaaaaa

Umenikumbusha rafiki yangu Isango

Siku chache kabla ya kifo chake tulikuwa tumenunua nyama tukakaanga na ndizi na vinywaji tukafurahi na marafiki zangu.

Siku chache baadae naona mitandaoni kafariki.

RIP Josephat!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu paskali, bado tunakuhitaji sana kaka, please usitupe wosia katika kipindi hiki kigumu. Mwenye enzi Mungu akufunike kwa ulinzi wake kama alivyomfunika Mh. Tundu Lissu. Amen.
 
Kila nikiangalia madaktari na manesi wanavyopambana na " kirusi" cha Corona pale UK nimeanza kuamini zipo kazi zinazohatarisha maisha.

Utangazaji ukiwa fair hakuna hatari yoyote!
Haiwezekani mtangazaji uwe fair kisha ubaki salama.

Imagine unapata habari namna jamaa wanavoitafuna nchi kama mchwa,with evidence.

Huku kuna kundi linalaumu hawa jamaa ni mchwa kwenye keki ya taifa.

Niambie a fair stori hapo itakuwaje ili huyu jamaa abakie salama.

Sent using iphone pro max
 
Mkuu we cheza na alama za nyakati , ukiona mkuu anapenda kusifiwa basi we andika makala za kumsifia, wanasema ukitaka kula na kipofu usimshke mkono .. maana na wewe ushaitwa kuhojiwa bungeni na hatujui ulihojiwa nn , kama vp unga juhudi mkuu
 
haukutakiwa kuzungumzia walio potea tu zungumzia na akina kabendera na wenzake waliyotendewa mpaka leo
Mkuu Hufi Leo bali kesho, kwa vile ni kuwahusu waandishi wa habari waliopotea au kutangulia mbele ya haki kwa vifo vya kutatanisha, wewe unaweza kuanzisha bandiko la waandishi waliotendwa, tutachagia
P
 
Duh...!. Mkuu Retired, unaamini kweli mimi nilitaka Twitter ifungwe?!.
Nisikilize

P

Nimesikiliza, dakika ya 1.37 to 1.47 unawaita TCRA ukisema "hawawezi", where are we, tuhamasishane tusisome twitter... Pascal ulipoiomba TCRA ukisema hawawezi, I have no speak of doubt kuwa ulimaanisha hawawezi kuiingilia kati katika haya yanayoendelea Twitter! Swali: Wanaingiliaje? the only option available to them ni kuiblock Twitter maana si rahisi kuzima card ambazo zitaonekana zina akaunti twitter!

Unajua fika kuwa wanaosoma twitter ni waelewa, very understanding people, kusema nitahamassha wasiingie twitter si kweli! Truly ulitafuta njia ya to awaken TCRA to do something about Twitter and the only irresistible conclusion to the action that can be taken by TCRA ni kuizima Twitter! Uliogopa kuweka wazi kuwa TCRA waifungie Twitter!
SEcondly unajua hali mbaya ya sheria ya magazeti, etc.....

soma link hiyo ambayo nimetoa excerpt hii chini

Govt tightens noose on social media
1591974378024.png
 
https://www.jamiiforums.com/data/attachment-files/2019/02/1994639_Instagram_media_-_Bt2Krycj3b7.jpg

Wanabodi,

Humu jukwaani tuko watu wa fani mbalimbali na miongoni mwao ni sisi watu wa fani ya habari.

Leo nimewakumbuka waandishi wa habari na kupotea/vifo vya kutatanisha, toka kwa Stan Katabalo, Ben Saanane, Azory Gwanda, Daudi Mwangosi, Josephat Isango, maajaliwa ya hatma za maisha yao, ni ama tuombe Mungu atunusuru na dhahama hizo, ama...

Ukiwa mwandishi wa habari wa kawaida tuu au mtangazaji wa kawaida tuu ni kazi kama kazi nyingine zozote, lakini ukiwa ni mwandishi wa habari za uchunguzi au mtangazaji machachari unayehoji maswali magumu, kiukweli wasomaji wako na watazamaji wako watakusifu sana kwa kazi nzuri, ila majaaliwa ya maisha yako na familia yako ni ya mashaka sana na wengi huwa na mwisho mbaya ambao hauzungumziki.

Tukianzia kwa mwandishi wa kwanza wa habari za uchunguzi nchini Tanzania, Stan Katabalo wa gazeti la Mfanyakazi aliyeibua kashfa ya Loliondo, alikufa kifo cha ghafla, japo alisifiwa sana kwa ushujaa na mpaka kesho jina lake bado linavuma kwenye list ya mashujaa wa habari Tanzania, lakini sijui kama kuna waandishi au vyama vya habari wanajua chanzo cha kifo chake, au kaburi lake linafanana vipi au majaaliwa ya familia yake baada ya kifo cha baba mwenye nyumba.

The same applies to Azory Gwanda na Ben Saanane wetu humu JF, yamebaki majina na mabandiko tu humu hakuna ajuaye hatima yao nini kiliwakuta, lakini sisi wanajamii vikiwemo vyama vya habari, japo tuliwasifu sana wakati wakileta habari za moto moto, lakini baada ya kutoweka, hakuna tena anayejali wala kujua tuu majaaliwa ya familia zao.

Nimelileta bandiko hili baada ya kumkumbuka mwandishi wa habari machachari Josephat Isango aliyefariki tarehe ya jana mwaka 2018, baada ya kuugua ghafla, hakuna media wala chama cha habari kilicho jishughulisha kubaini chanzo cha kuugua ghafla kwake na baada tuu ya maziko, sifa na pongezi zake zinaishia hapo makaburini kwa waandishi, vyama vya habari na vyama vya siasa kuweka mashada makubwa ya maua, kisha kusoma risala nzuri ya jinsi marehemu alivyokuwa mwandishi shujaa, then all ends up there and then.

Mimi nilifahamiana na Josephat Isango kwa kuunganishwa nae na mtangazaji nguli Angalieni Mpendu kupitia kipindi cha Jicho Letu Ndani Ya Habari mwaka 2015.


Kisha tukaja kukutana Siku ya Uhuru wa Habari Morogoro then Mwanza na kote akihadithia jinsi anavyo windwa na wenye mamlaka.

Hadi kifo chake, sikupata kusikia alikufa kwa nini au chanzo cha kifo chake kama ilivyo kwa Stan Katabalo, ila kiukweli sisi waandishi wa habari za uchunguzi na watangazaji wa maswali magumu, tuna wakati mgumu sana kwenye maisha yetu.

Hivyo wanabodi, tunaposifina humu kwa maswali magumu kama yale ya Ben Saanane, tusiishie kusifiana tuu humu bali tuangalie na hatma za maisha yetu na familia zetu, hivyo ikitokea mtu aliyekuwa very critical on the status quo, ghafla akageuka na kuanza kuunga mkono juhudi, nawaombeni sana muwaelewe watu wa aina hii ambao hawaangalii leo au sasa bali wanaangalia kesho na kuangalia mbali.

Tuombeni sisi watu wa media tumalize salama hatma za maisha yetu na ikitokea yakakatishwa ghafla, wale ambao ni rafiki zetu wa kweli wa kufa na kuzikana, tuushie kwenye mashada na risala za wasifu, bali angalau fuatilieni na majaaliwa ya familia zetu.

RIP Wanahabari wote waliotangulia mbele ya haki na Mungu uwanusuru wale waliopotea bila sisi kujua hatma zao, na utajaalie moyo wa ufuatiliaji kujua majaaliwa ya familia zao.

Paskali
Baadhi ya mada za Isango
Naomba mjadala wa wazi na Zitto kuhusu usaliti ndani ya chama - JamiiForums

Je, ni sahihi kwa CHADEMA kumzika Josephat Isango kwa taratibu za chama? - JamiiForums

Waandishi wa habari kuvaa sare za vyama kama huyu Gerson? - JamiiForums

TANZIA: Mwandishi wa habari, Josephat Isango afariki dunia; Azikwa Kisasida, Singida - JamiiForumsé

Josephat Isango (Tanzania Daima) ashtakiwa, adaiwa mil.500 - JamiiForums

Josephat Isango, Mhariri wa Habari Tanzania Daima akamatwa na Polisi - JamiiForums

Josephat Isango: Natoa Shukrani kwa wote - JamiiForums

Tanzia: Josephat Issango afiwa na baba yake. - JamiiForums
 
Nimesikiliza, dakika ya 1.37 to 1.47 unawaita TCRA ukisema "hawawezi", where are we, tuhamasishane tusisome twitter... Pascal ulipoiomba TCRA ukisema hawawezi, I have no speak of doubt kuwa ulimaanisha hawawezi kuiingilia kati katika haya yanayoendelea Twitter! Swali: Wanaingiliaje? the only option available to them ni kuiblock Twitter maana si rahisi kuzima card ambazo zitaonekana zina akaunti twitte..
Mkuu Retired, huku sasa kutakuwa ni kulishana maneno!. Hivi huwezi kufanya ukosoaji bila kutukana, kudhalilisha na lugha za kuudhi?.
Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli
P
 
Bahati mbaya mmeshindwa kuwaita mashirika ya kimataifa ya kutetea uhuru wenu.Umenikumbusha yangu Isango daah,hata kipind mnahojiwa na Angalien Mpendu niliwaona.
 
Back
Top Bottom