Waasi wa M23 sasa waelekea mji wa Bukavu

Waasi wa M23 sasa waelekea mji wa Bukavu

Kagame katili mno.

ICC haitamuacha salama huyu Mzee.
Kagame alikomesha mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 mauaji ya kikatili sana sasa iweje yeye ndie asingiziwe ukatili?!
 

Prof. James Ker-Lindsay anachambua uwezekano wa Nchi Ya Kongo Kuingia ktk Vita Kamili?


View: https://m.youtube.com/watch?v=kAVJSlUAxy0
Mchambuzi bobezi nguli wa masuala ya ulinzi, usalama, utatuzi wa migogoro na ujenzi wa utaifa - anaangalia mazingira ya sasa eneo la Maziwa Makuu yaani Afrika ya Kati

Je, Afrika ya Kati inaelekea kwenye vita vingine vya uharibifu?

Mvutano kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umefikia hatua mbaya, huku hofu ikiongezeka kuwa mataifa hayo mawili yako ukingoni mwa vita kamili.

Mwishoni mwa Januari 2025, kundi la waasi la M23 ambalo linaaminika kuungwa mkono na Rwanda lilianzisha mashambulizi makubwa, na kuteka maeneo muhimu mashariki mwa Kongo, ikiwa ni pamoja na sehemu za jimbo la Kivu Kaskazini.

Kuongezeka huko kumewalazimu mamia kwa maelfu kukimbia, huku kukiwa na ripoti ya mapigano makali kati ya M23 na vikosi vya serikali ya Kongo FARDC.

Huku Umoja wa Mataifa ukiitaka Rwanda kujiondoa na shinikizo la kimataifa kuongezeka, Rais wa DR Kongo mheshimiwa Felix Tshisekedi ametangaza kuwa iwapo Rwanda haitasitisha kujihusisha kwake, vita haviwezi kuepukika.

Mgogoro huu umekita mizizi katika historia, unatokana na matokeo ya mauaji ya halaiki ya Rwanda ya 1994 na miongo kadhaa ya ukosefu wa utulivu mashariki mwa Kongo.

Rwanda inahoji kuwa hatua zake zinalenga kuangamiza makundi ya wapiganaji wa Kihutu, hasa Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (DFLR), ambayo inaona kuwa tishio la moja kwa moja kwa usalama wake.

Hata hivyo, wachambuzi wengi wanadokeza kwamba uingiliaji kati wa Rwanda unaweza pia kuchochewa na malengo ya kiuchumi na kimaeneo, huku ripoti zikionyesha kuwa Rwanda imekuwa ikinufaika kinyume cha sheria na utajiri mkubwa wa madini wa Kongo.

Wakati mataifa yenye nguvu ya kikanda na kimataifa, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, Marekani, na Umoja wa Mataifa, yanapojaribu kupatanisha, hatari ya mzozo wa muda mrefu na mbaya bado iko juu.

Je, hii inaweza kuwa vita kuu ijayo ya Afrika, au bado kuna matumaini ya azimio la kidiplomasia?
Source : Prof. James Ker-Lindsay
 
Anafeli sana sana, na hiki kinatufanya wengi tumuone mpumbavu asiye na akili.
Hiv kwa Rais wa DR congo, ni kitu gani kwake kilipaswa kuwa kipaumbele kama sio suala la Eastern congo??
Hii ilipaswa kuwa agenda yake number 1 from day 1 anaingia ikulu.
Mpumbavu huyu kila siku kushindia vikao visivyo na mbele wa nyuma hajui hata anataka nini.

Tunamlaumu sana Kagame ila baada ya kusikia hotuba yake katika mkutano wa EAC jamaa nimemuona ana akili sana. NA ninkama amekua akiwafokea maraisi wenzie na 100% ya alichokiongea ni kweli...
Fuc.k them all eac presidents!!.
Kaka,sisi watanzania tuna uelewa mdogo sana na mambo ya kimataifa,kama haya DRC,ukifuatilia vizuri,M23 wanajitetea dhidi serikali dhalimu ya kabila,natamani wamuondoe madarakani
 
Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (DFLR)
Sijui sisi Waafrika tunatatizo gani upstairs, inakuwaje mtu unajiita" Democratic Forces"wakati umebeba arms violently killing another ethnic group?!

Tulirogwa na nani?
 
Maongezi hapo m23(rpf)
M23 ni Congolese Tutsis sidhani kama RPF bado iko bali ni Rwanda Defence Forces kama sikosei.

FDLR former Interahamwe imetengezwa kipindi cha Hayati Kabila snr.
Bado wana ile ideology ya kumaliza Watutsi labda waweke silaha chini kwanza.
 
Msemaji wa M23 : Bandundu, Kasai, Katanga wanatupigia simu tuje kuwakomboa na sisi M23 tunasema tupo njia


View: https://m.youtube.com/watch?v=Eo9d5qy78vg

Lawrence Kanyuka msemaji mojawapo wa M23 akijibu maswali ya mwandishi kuhusu vuguvugu linavyovutia wakongomani wote ... mfano magharibi ya DR Congo jimbo la Kwilu mji wa Bandundu kuelekea Kinshasa wanapiga simu kuuliza lini ukombozi utafikia fasi (eneo) hiyo ...

Ramani ya DR Congo huku jimbo la Bandundu (Kwilu) katika rangi nyekundu linalopakana na jimbo Kinshasa na la Bas Kongo
1738362692334.png


More info:
Huku raia wa waliopo Goma wabeba mabango yenye ujumbe kuwa wamechoka utawala wa Kinshasa wa rais Felix Tshisekedi. Raia wasema M23 hainashinda na watu tofauti na majeshi ya Mgambo vikaragosi vya Kinshasa wanaojiita WAZALENDO na jeshi la serikali la FARDC ambao walikuwa wanapora matelefoni ya raia, pesa, chakula n.k lakini M23 imezimisha uhalifu wote wa FARDC na mgambo vikaragosi Wazalendo ..


View: https://m.youtube.com/watch?v=VJ7UNb6FC_c
 
Kagame alikomesha mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 mauaji ya kikatili sana sasa iweje yeye ndie asingiziwe ukatili?!
Hicho anachowafanyia wacongo toka mwaka 1996 ni zaidi ya ukatili.
 
M23 ni Congolese Tutsis sidhani kama RPF bado iko bali ni Rwanda Defence Forces kama sikosei.

FDLR former Interahamwe imetengezwa kipindi cha Hayati Kabila snr.
Bado wana ile ideology ya kumaliza Watutsi labda waweke silaha chini kwanza.
Uwongo,fdlr hawana hiyo ideology,nyinyi watutsi mnawalisha maneno,fdlr waingizwe RDF,ni wanyarwanda
 
Back
Top Bottom