Wababa wenye magari, kwanini mnasimama kwa dakika kadhaa kabla ya kuingia majumbani mwenu?

Usalama wa chombo au usalama wa mtu binafsi? Fafanua mkuu
Usalama wa mtu binafsi na mazingira. Unaweza kunyooka mojakwamoja kumbe wasiojulikana wamekutangulia. Kusimama nje ya eneo lako kwa muda mfupi kunaweza kukusaidia kunotice utofauti wa mazingira kwa siku hiyo.
 
Wewe inaelekea siyo mtu mzuri. Kwanini umekuwa ukifuatilia watu namna hiyo!!! Jitafakari ndugu.
 

Wazungu husema "Mind your own business!
1. Sasa mtu akisimama getini kwake, pengine anasubiri afunguliwe inakuhusu nini?
2. Wengine husimama kumalizia kuongea na simu ILI akiingia ndani aendelee na mambo ya familia
3. Wengine husimama kuangalia mazingira kama yapo sawa kabla ya kufunguliwa geti....
4. Wengine hupunguza mwendo kupiga simu ili akifika getini, akute tayari mtu wa kufungua amefika

Najua mawazo negative ni kuwa, Wanasimama kufuta meseji kitu ambacho sio kweli kabisa; kwani wameshindwa kufuta huko walikotoka?

Tumieni akili zenu vizuri kuwazia mambo ya maendeleo (positive).
 
Kitaalamu haishauriwi kuzima gari ghafla baada ya kutoka masafa, lazima utumie muda kadhaa kusubiri ndiyo unaweza kuizima.
Kwahiyo simu hutumika kupoteza muda tu kabla ya gari kuzimwa.
Mleta mada punguza kuwaza ujinga
 
gari inapotoka mwendo mrefu....unaiacha sailensa kwa mda kama dk 5 mpaka 10 waanasema oil ishuke then unaizima... na hivyo hivyo kuwasha unawasha unasikilizia kidogo...
 
Wewe ni me au Ke?
 
Binafsi Sina gari Wala pikipiki ila kabla sijaingia ndani Huwa na clear simu yangu hasa kutoka kwa Vimeo.
 
gari inapotoka mwendo mrefu....unaiacha sailensa kwa mda kama dk 5 mpaka 10 waanasema oil ishuke then unaizima... na hivyo hivyo kuwasha unawasha unasikilizia kidogo...
Hiyo ni kweli, lakini mimi nimesemea wale wanao simamisha magari katikati ya barabara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…