uchumi2018
JF-Expert Member
- Mar 4, 2018
- 1,657
- 2,406
Ni kuepusha matatizo ya kuingia ndani kwa ghafla ukakuta utakachokikuta.Wengi wenu, kabla hamjafika karibu na mageti ya nyumba zenu, mnasimamisha gari na kuwa Bize na simu kwa dakika kadhaa.
Ni kipi cha muhimu mnafanya kwenye simu wakati huo? Kwani huko mlipotoka mlikosa muda wa kufanya hivyo?
Nasema haya maana hapa mtaani naona sana hayo, nyumbani ni njiani na wengi wanapita hapa wakielekea kwenye mageti yao, sasa wanasimama bila sababu, na ukipita unawaona wapo Bize na simu ndani ya gari.
Huwa mnafanya nini na hizo simu?
Wazee wa zamani walikuwa wakikaribia miji yao wanapitia nyumba ya jirani na kumtuma mtoto wa jirani
apeleke mizigo nyumbani,kama taarifa ya kuwa mwenye mji amerudi.
siku hizi tunatumia magari,mlio wa gari ukisikika kila kitu ndani kinawekwa sawa.Sasa jifanye kushtukiza uone kama hujafa kwa ugonjwa wa moyo.