Wabongo Hawatumii Consultants vizuri ndio maana wengi wanafeli kwenye biashara

Wabongo Hawatumii Consultants vizuri ndio maana wengi wanafeli kwenye biashara

Mkuu hii ninayofanya yenyewe ni biashara mkuu,Au wewe unataka kujua biashara zote ambazo nimewahi kufanya?Huwa I share that with my clients ili kuwapa mwanga juu ya uzoefu wangu na changamoto ambazo zimenifanya niamue hasa kutoa huduma za consultancy kwa SMEs na Start ups.

Kimsingi nimeshafanya biashara tena za aina nyingi kuanzia,Kuuza Chips,Kuuza supu,Kuuza genge,Duka la reja reja,Duka la jumla,Duka la spare za Magari,Import,Network Marketing,Online business za aina tofauti and much more.Nikikutajia aina ya biashara ambazo nimewahi kufanya unaweza usiamini ili naweza nikakupa fact moja tu.(Nilizijenga zikakua,na nikaona kwamba hazilipi kadiri ya matarajio yangu nikazifunga na nikajaribu aina nyingine na nyingine.Kutokulipa kwa biashara sababu moja wapo ilikuwa na upungufu wa mtaji na profit margin ndogo na gharama kubwa za uendeshaji na too much efforts with very litle gain) Kwa ufupi biashara nimefanya mkuu.

Iwapo unataka nikupe abc za kukua kibiashara tuwasiliane kwa whatsap +255715323060 au emai:masokotz@yahoo.com and you will be amazed.

Hebu sema kidogo kuhusu network marketing business nione mtazamo wako[emoji848]
 
In Brief:
Age 30+
Work Experience:15+Years in Employment,Business and Consulting
Business Experience

First Business Started in :2003:
Second Business in 2007
Third Business in 2009
Fourth Business in 2012
Fifth Business 2014
Sixth business 2016
Seventh business 2019
Ninth business 2020

Work Experience:

First Job in 2007
Second Job in 2008
Third Job in 2009
Fourth Job in 2011
Fifth Job in 2012
Sixth Job in 2014
Seventh Job in 2016
Eighth and Current Job in 2018

Education:
1 Degree
1 Diploma
4 Certificate
12 Certifications
and I am still learning
Consulting Clients
Past number of clients:23
Pro bono Consulting 45
Current Assignements 13

For work discussion:Whatsap +255715323060 Email:masokotz@yahoo.com

Hizi biashara zote 9 bado unazo?
Kwanini umekuwa ukibadilisha badilisha biashara
Umejifunza nini wewe binafsi kupitia biashara zako
 
Kwa mtazamo wangu na uzoefu wa kufanya ujasiriamali/biashara:

1. Consultation inafanya kazi vizuri zaidi katika medium na large scale businesses ila kwa biashara ndogo kidogo ni mtihani.

2. Mifumo yetu mingi sio rasmi wakati Consultants wetu mara nyingi wanatoa ushauri ambao si mbaya bali unahitaji mifumo rasmi kuoperate.

3. Wafanyabiashara wetu kwa asilimia kubwa wana magumashi mengi kuanzia kwenye namna ya upatikanaji wa mtaji, uendeshaji, ulipaji kodi nk nk hivyo wanaoperate nje ya uhalisia ndio maana hawaoni kama consultation ni jambo lenye maana.

4. Wafanyabiashara wengi huiga anacho fanya fulani hivyo wanaona kama kulipia consultation ni kuchezea pesa.

Umeongea ukweli brother..

Kingine kinacholeta shida ni mtu kuwa consultant wa industries karibia zote kitu ambacho kidogo hakiwezekani labda awe mwenye experience na exposure kubwa mno au ana watu sahihi wa kumsaidia

Sawa na business plan tu, unakuta unaandikiwa na mtu ambaye hana uelewa wala udhoefu wa industry yako. Mwisho wa siku unaandikiwa maneno matamu yasiyo na uhalisia
 
Ni kweli mkuu, kuna baadhi ya consultants hufanyia kazi tamaa, anapokea kazi ambayo anajua hataimudu na matokeo yake anamtia hasara mteja wake na kuchafua taaluma yake pia.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Hawa wengi wanaojiita wasomi ukiwafatilia utagundua hawana 'ujiniasi' wowote zaidi walitumia muda na akili zao kwenye jambo moja (kusoma).

Unamkuta 'jiniasi' hajui kucheza mchezo wowote, hajui namna ya kuinteract na jamii, hajui hata kuapply hicho alicho kisoma....yaani alicho nacho na anachokiona cha maana ni vyeti tu.

Ndio maana sasa unawaona wanakimbia kada zao na kupigana vikumbo kwenye siasa, wameacha kuamini hata yale waliyo tumia muda mwingi kutuaminisha vyuoni, wengine wamekana hadi thesis zao ili tu wapate kutii matumbo yao...

Yule jamaa alisema, I have got a family to feed not a society to impress...watu wanafikiri kwa kutumia mioyo, wanaongozwa na tamaa zao.

Tofautisha kusoma na uwezo wa asili wa mtu.

Kusoma haswa elimu sahihi (course) kwa kiasi kikubwa inakurahisishia na kukupanulia wigo wa kutumia uwezo wako wa asili vizuri zaidi.. Hii hata experience ina kazi hiyo hiyo kiasi flani

Ila kusoma hakukuongezei uwezo wa asili kama kipaji mkuu.. ukipewa umepewa hata usipoingia darasa moja
 
Ni kweli mkuu, kuna baadhi ya consultants hufanyia kazi tamaa, anapokea kazi ambayo anajua hataimudu na matokeo yake anamtia hasara mteja wake na kuchafua taaluma yake pia.

Hiyo ndio ipo sana na ndio maana baadhi ya watu wanaamua kuchoma pesa kwenye business agencies ambazo yana facilities za kutosha.

Japo si kila mpango wa biashara lazma ufanikiwe ila kutumia watu binafsi wasio na track record nzuri kisa ni cheap. Ni risk zaidi
 
Bravo mkuu,
Nikiri kuwa nikikusoma naona brevity, creativity na passion uliyo nayo juu ya ulicho amua kudeal nacho (consultation). Kitu pekee kinachoweza kuleta vikwazo ni kukosa ushirikiano kwenye mifumo yetu lakini so far nakuona ukimove in a right direction.

Hivi vikwazo vichukue kama changamoto, by the time watu wengine wanazinduka kuwa you are making millions... utakuwa umejijengea msingi wa vizazi na vizazi.

Mafanikio huwa yamejificha kwenye siri, msemo huu watu hudhani kuwa kuficha namna ulivyofanikiwa ndio siri yenyewe, hell no!! Maana yake ni kuona wasiyo ona wengine.

Watu wanakuhoji mbona we hufanyi hizo biashara unazo shauri watu?

Nikusaidie kuwajibu, jamaa aliyebuni mobile transaction business (m-pesa tigo pesa etc) hakuwahi hata kumiliki kibanda cha m-pesa. Alichokiona yeye ni fursa na akatengeneza idea iliyoleta tija kwa watumiaji wake thats all.

Mkuu unajua unachokiongelea. You are the best 👏👏👏👏
 
Tofautisha kusoma na uwezo wa asili wa mtu.

Kusoma haswa elimu sahihi (course) kwa kiasi kikubwa inakurahisishia na kukupanulia wigo wa kutumia uwezo wako wa asili vizuri zaidi.. Hii hata experience ina kazi hiyo hiyo kiasi flani

Ila kusoma hakukuongezei uwezo wa asili kama kipaji mkuu.. ukipewa umepewa hata usipoingia darasa moja
Naelewa mkuu, genius ni natural gift ndio maana ukiangalia kwenye comment yangu kila nilipolitumia neno hilo nimetumia quotation ('jiniasi'), nikimaanisha kwetu 'jiniasi' ni mtu ambaye ametumia muda wake mwingi kusoma vitu/level mbalimbali na pengine ana prefix titles kama Dr, Prof, Eng etc. bila kujali anachoweza kudeliver.
 
Mshauri mzuri wa biashara unayotaka kufanya ni yule ambae anaifanya biashara hiyo, ila hii ya PDF, PPT, kama matikiti sijui

Kwa sbb yeye atakwambia faida iko hapa na hasara inapatikana hapa, sehemu za kuchukua mzigo kitonga n.k
Pili badilisha changamoto iwe biashara hii ndo ya mwisho
 
Mkuu,

Mifano unayotoa kwenye hii mada ni irrelevant.

Wewe kama ni consultant basi JUKUMU lako ni kuhakikisha unashawishi wateja waone umuhimu wako.

Si ndivyo?

Ukishindwa hilo na kuanza kulalamikia watanzania wewe ndiyo una shida kubwa.

Wafanyabiashara wa hapa Tz au nchi yoyote ile hawapo kwaajili yakukuonea wewe huruma au kwasababu eti wafanyabiashara wa America na Europe wanatumia consultation services.

Mfanyabiashara anachotaka ni results.

Kumbuka, money is attracted to value.

Kama watu hawaoni value haijalishi kiasi gani utawalaumu kamwe hawatahitaji huduma yako na hawatokupatia pesa [emoji383]

Ni rahisi tu kufahamu hili.

Hiyo ndio reality mkuu

Kwa biashara nyingi za chini yaani SME's

Value = sales

Ukienda na gear nyingine ndio bhasi tena
 
Naelewa mkuu, genius ni natural gift ndio maana ukiangalia kwenye comment yangu kila nilipolitumia neno hilo nimetumia quotation ('jiniasi'), nikimaanisha kwetu 'jiniasi' ni mtu ambaye ametumia muda wake mwingi kusoma vitu/level mbalimbali na pengine ana prefix titles kama Dr, Prof, Eng etc. bila kujali anachoweza kudeliver.

Ni misconception zilizopo kwemye jamii zetu

Umeongea ukweli na nakubali brother
 
Tatizo lipo hapa

Kutafsiri neno la kiingereza kwenda kishwahili

1)Consultant -Mshauri(Anakuelekeza baadhi ya mambo ya kitaalamu Banking, Tax, Revenue nk)

2Mentor-Mshauri (Amefanikiwa katika unachofanya)

Wachangiaji wengi wameelewa vyengine wancahanganya MENTOR na CONSULTANT.

Humu wengi wamemtafsiri CONSULTANT kama MENTOR ndio wanasema kwanini hana Biashara.

Wasomi wa kizazi hiki bwana!..
 
Back
Top Bottom