Wabongo mkija majuu au ughaibuni acheni unafiki, majungu na ukora mnaliabisha Taifa lenu

Basi ndio umwambie hayo ili akusaidie, mimi huwa ninapata nafasi za kazi za gulf countries na watu kadhaa nimewaunganisha huko, pia huwa napata za Canada ila gharama zake huwa kubwa.
 
kuchomeshana kisa umemzidi kipato kawaida ila kinachowagharimu watanzania ni kujuana sana kila mtanzania unayekutana nae ni ndugu
Hii kwa kiasi kikubwa inatokana na watu kuishi kwa mafungu kwa kutaka kupunguza gharama za maisha.

Watu wanaoishi kivyao ni vigumu code zao kutoka, unless wao wenyewe wawe watu wa kuongea sana.

Mimi nimeishi kivyangu miaka karibu yote, hivyo hata mtu kupata habari zangu za ndani ni tabu.

Ingawa pia hata mtu angetaka kunichimba angekuta bullet proof battle scarred Shogun.

Yani ile mpaka FBI wakifungua vifurushi wanakutana na vitabu tu!
 
Basi ndio umwambie hayo ili akusaidie, mimi huwa ninapata nafasi za kazi za gulf countries na watu kadhaa nimewaunganisha huko, pia huwa napata za Canada ila gharama zake huwa kubwa.
Sasa mtu unamuuliza qualifications, or lack of, ujue ana fit wapi, hata kukujibu hilo mgogoro.

Unaona huyu ni actor tu.

Ana pose kwa ajili ya audience tu.

Si mtu wa kazi.
 
Mkuu Kiranga mimi nina elimu ya kawaida,nilifika form 6 lakini nilifeli kwa ishu zilizosababishwa na mapenzi(Haya hayana umuhimu).

Mimi ni dereva mzuri tu na nina miliki leseni daraja C,pia nina passport,kadi ya chanjo ya korona,kadi ya chanjo ya yellow fever.

Nahitaji kufika nje kwa fursa kama udereva lakini pia fursa yeyote ya unskilled mimi napiga,ishu ya pesa ya nauli kwangu siyo ishu.

Wewe niambie nifanye nini mimi nitafanya ili niweze kufika hapo
 
Mimi ni muongo.Umesema mwenyewe. Hivyo siwezi kukusaidia.
 
Safi hapo sasa umejieleza vizuri, now tumsikie mkuu Kiranga atajibu nini, itakuwa msaada kwa wengine pia.
 
Ktk historia wazee wetu walioongoza mapigano au aina yoyote ya kukataa udhalimu kutoka kwa wakoloni walisalitiwa na baadhi ya wazee wetu mfano mdogo tu ni mfanyabiashara maarufu wa pwani BWANA HERI ambae alikua mstari wa mbele kupinga wakoloni wa kijerumani alinyongwa ktk mwembe uitwao mwembe kinyonga pale korogwe baada ya kukamatwa akiwa mafichoni huko Dodoma hivyo majungu na kusalitiana hapa bongo ni sehemu ya maisha.
 
Ebu toa hints za nini kifanyike ili uweze kutoa msaada kwa muhusika mwingine
Kwanza kabisa yeye mwenyewe ajue ana kipi, hana kipi, anataka kusaidiwa wapi.

Mfano.

Kuna watu wana degree ya kwanza, wanataka kusoma zaidi nje kwa njia ya scholarships, wanajua wamesoma field gani, wanajua wamefanya mitihani gani, au hata kama hawajui, hawa tunaweza kushauriana nao. Kuna network ya safari za mambo ya vyuo, scholarships, grants, loans etc.

Kuna watu hawana pa kufikia wala barua ya mualiko, wana safari za kijamii/kitalii wanahitaji barua ya mualiko itakayoonesha wana sehemu ya kufikia.

Kuna watu wana qualifications za kutafuta kazi zenye soko sana kimataifa, wanahitaji kujua jinsi ya kuunganishwa na makampuni ya kimataifa kufanya kazi.

Kitu muhimu ni mtu mwenyewe awe na idea ana kipi, anataka kufanya kipi, anataka msaada wapi, ana kipaji gani, mtu aanze kufanya homework yeye mwenyewe, si anataka kuja nje tu wakati hata yeye mwenyewe hajui anataka kufanya nini huko nje.
 
Siyo vizuri kuwa kisiwa. Ni vizuri kushosolaiz na kujichanganya kigumu hivyo hivyo.

Kuna nature kama kifo na kuuguwa. Japo mibongo mingi ni mitambo ya umbea hivyo hivyo tu itasaidia.

Lakini tabia zetu mtoni ni mbofumbofu na kukera.
Wabongo wa mamtoni sio wa ku socialize nao.
Mim nikiwa mamtoni ni wazungu na big brain nigerians tu.
wabongo wa nje hawana issue na vibesdei vyao vya sebuleni umbea wanaume na wanawake.
Wote wanafanya kaz za kufanana ukifanya cha tofauti lazima wakupe shida.
Wana roho mbaya hawaoni shida kukuchoma mkose wote.
 
Naona ni mchakato uanaohitaji ujitambue na ufahamu unachokitaka haswa. Kwa kunufaisha audience, ikiwa ulishaweka uzi wa mambo haya. Unaweza ku attach hapa ili tufahamu kwa undani baada ya hizi insights. Shukhurani
 
Majungu hayo utakua huna tofauti nae
 
Kutawaliwa ni matokeo ya wazee wliokuwa ma snitch, zile meli za arabs zilikuwa zikitia nanga pwani vijana wa kibantu wanaenda kuwatafuta na kuwawinda vijana wenzao kuwauza kwa arabs na whites, wanapewa fedha,hovyo kabisa.
 
Jibu yale maswali yake mkuu.
Ukiyajibu mchoro wa jinsi yakusaidiwa utapatikani.
Usiyadharau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…