Wabongo wengi wanaoishi Marekani wana maisha magumu tofauti na wale wanaoishi nchi za Scandinavian

Wabongo wengi wanaoishi Marekani wana maisha magumu tofauti na wale wanaoishi nchi za Scandinavian

Mleta mada Yuko vizuri, hebu nyie mnaofikiri Marekani ni mbinguni leteni ushahidi wa mafanikio yenu.Hata hivyo maisha ya Marekani yapo juu kikubwa ukienda fanya KAZI Kwa malengo miaka kadhaa rudi nyumbani uwekeze, Kuna watu Huwa wakirudi likizo yaani mpaka unajiuliza huyu alikuwa Marekani au matombo morogoro
Wengine hivyo vizinga sasa halafu kila dakika in new york this in Miami that
 
Sikubalian na wewe, kwamba kutoboa marekani ni ngumu, Si Sahihi, watu wanaenda na Visitor Visa kama wale machalii ya R, hawarudi huwezi toboa, kazi utafanyaje mzee unaishi maisha ya "Cash Jobs" hatari

Ingia hizo nchi na vibali utatoboa asubuh kweupe sana

Mfano

Unalipwa $19(hizi ni kazi za wabeba box) kwa saa unafanya masaa 50 kwa wiki, $3800 kwa mwezi ukitoa kodi $3300 kwa mwezi unaishi chumba cha $750(included everythings) unakula $300 kwa mwezi, hivi upo peke ako unashindwaje kutoboa

ACHENI KUSAMBAZA UONGO WAZEE, hizi nchi kama unaponda bata hapa hela yao haina thaman kwao, Ukichange kwa madafu wewe TAJIRI
Brother unaongezeka mambo ya miaka mitatu iliyopita. Leo hii watu wana taaluma zao US lakini inabidi wafanye kazi mbili to get by. Mimi naongelea current situation (2023). Hadi wamarekani wanakimbilia Scandinavian country sio poa.
 
Hao unaosema wengi wao amekurupuka, mbona kuna wengi sana wanaishi maisha mazuri tu.

Ukitaka kuishi vizuri nchi hizo, wachana kabisa kuwa karibu na wabongo na magenge yasiyo na maana.

Nawashauri wanaokwenda huko, kama hawana mipango thabiti na ya uhakika basi wakaanzie maisha miji midogo midogo ambayo haina wabongo.
La kuwakwepa wabongo ukiwa nje nakupa maua ustadhati.
Unakuta mtu yuko ulaya hana rafiki mzungu hata mmoja na wabongo wa nje wengi wao majungu na kuchomana.
 
Kinachoniuma ni namna naona watanzania wenzetu ambavyo wanataabika huko nje wakati wenzao Tina maisha mazuri tu hapa nyumbani
Well said mkuu.
Mimi naamini Tz ukiwa na uhakika wa basic needs ni kuzuri kuliko popote duniani so abroad ukoenda atleast ukirudi hata usipokua tajiri uwe tu na maisha standard uta enjoy sana.
 
Brother unaongezeka mambo ya miaka mitatu iliyopita. Leo hii watu wana taaluma zao US lakini inabidi wafanye kazi mbili to get by. Mimi naongelea current situation (2023). Hadi wamarekani wanakimbilia Scandinavian country sio poa.

Unapofika nchi kama marekani/Canada/Uk kwanza unatakiwa ujue wapinzani wako ni kina nani, Usiende na kidegree chako cha UDSM na GPA yako ya 4.5 ukadhani watakushobokea mzee, USIENDE HIZO NCHI KUTAKA KUFANYA KAZI ULIYOSOMEA, UKIBAHATIKA KUIPATA "shukuru" pili ukipata jua UJIRA ni mdogo

Mtoto wa "High school" anafanya kazi bank ambazo CRDB wao wanaajiri mwenye GPA ya 4.0

Usijilinganishe na mzawa wa hizo nchi hata siku moja

Kazi zenye malipo zipo nyingi sana, ambazo haziitaji elimu
 
Wewe utakuwa mchawi , wewe amba hata umeme na maji shida umamuonea huruma mtu aliyeko marekani?
Wewe ambae ukistaafu unakaa siku chache unapata depression unakufa halafu unasema unamuonea huruma mtu aliyeko marekani kuwa serious bwana, mimi nipo bongo ila nitakuwa mnafki nikisema sitaki kwenda marekani nikipata fursa au channel ya maisha, napenda watoto wangu wapate elimu bora sio kutongozwa na malecture wetu vyuo vya bongo halafi mtoto akimaliza chuo anatangatanga tu ,
Hajasema watu wasiende marekani.bali.ameshauri mtu ukienda usijisahau miaka ikaenda huna la maana umefanya mkuu.

Halafu mtoa mada nina uhakika kaishi Scandnavia.Kuna neno katumia wanalitumia watu wa huko
 
Unapofika nchi kama marekani/Canada/Uk kwanza unatakiwa ujue wapinzani wako ni kina nani, Usiende na kidegree chako cha UDSM na GPA yako ya 4.5 ukadhani watakushobokea mzee, USIENDE HIZO NCHI KUTAKA KUFANYA KAZI ULIYOSOMEA, UKIBAHATIKA KUIPATA "shukuru" pili ukipata jua UJIRA ni mdogo

Mtoto wa "High school" anafanya kazi bank ambazo CRDB wao wanaajiri mwenye GPA ya 4.0

Usijilinganishe na mzawa wa hizo nchi hata siku moja

Kazi zenye malipo zipo nyingi sana, ambazo haziitaji elimu
Sasa Brother kama ni hivyo si bora mtu ukaja Ujerumani. Maana huku ukija na cheti chako ufanyiwa training ya wiki sita then unaanza kazi. Na kuna uhaba wa skilled labour. Changamoto ni lugha tu.
 
Hata hapa nilipo ni popote,sijui unazingumzia popote ipi Binti Maringo
We jamaa mshari sana! Wenzako wanaongea kwa fact! Sehemu huijui! Hujawahi kufika! Hali ya kiuchumi, fedha, tamaduni na maisha mengine huijui zaidi ya kusoma na kusikia alafu unaambiwa unaleta matusi... ukubwa huambatana na ustaarab, hekma na busara.

Eti nauli za kuja zinawashinda... HAHAHA! dahh!... kweli nauamini ule msemo usemao "Usikizungumze usicho na elimu wala ujuzi nacho"

Hupajui Marekani wala Canada, kaa kimya wacha kelele... jidanganye hivyohivyo walio huko hawana hela na wana maisha magumu 😀
 
Hajasema watu wasiende marekani.bali.ameshauri mtu ukienda usijisahau miaka ikaenda huna la maana umefanya mkuu.

Halafu mtoa mada nina uhakika kaishi Scandnavia.Kuna neno katumia wanalitumia watu wa huko
Nchi yoyote ukienda bila ya makaratasi utateseka, lakini watu naowafahamu walioenda marekani they are doing very good , ukiacha wachache ambao labda kwa namna moja au nyingine hawana discipline na huwezi kulinganisha mtu wa scandinavia na usa kwa kipato , marekani wapo juu kwenye malipo na living standards
 
Sasa Brother kama ni hivyo si bora mtu ukaja Ujerumani. Maana huku ukija na cheti chako ufanyiwe training ya wiki sita then unaanza kazi. Na kuna uhaba wa skilled labour. Changamoto ni lugha tu.

Hata America ishu ni lugha, kingereza tunachoongea sio kingereza, ndio maana profesa yalimshinda

Pili, pathways za PR za nchi nyingine ni ngumu sana, kwenda kuishi kwa ujanja ujanja si vizuri
 
Brother unaongezeka mambo ya miaka mitatu iliyopita. Leo hii watu wana taaluma zao US lakini inabidi wafanye kazi mbili to get by. Mimi naongelea current situation (2023). Hadi wamarekani wanakimbilia Scandinavian country sio poa.
Mmarekani akimbilie Scandinavian labda mmarekani wa USA River Arusha

Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom