Wabongo wengi wanaoishi Marekani wana maisha magumu tofauti na wale wanaoishi nchi za Scandinavian

Wabongo wengi wanaoishi Marekani wana maisha magumu tofauti na wale wanaoishi nchi za Scandinavian

Mim nilibahatika kukaa California-san Diego & Los Angeles ,huko Hadi wamarekani Wenyewe wanapakimbia Kwa gharama ya maisha ,pamoja na degree yangu kazi niliyofanya ni kuwaosha wazee wasiojiweza wenye umri mkubwa ikiwemo kuwatawaza ,kuwabadilisha nguo etc hizo kazi zinalipa sana aisee pia kufanya kazi kwenye ranch Moja iv...

Nchi za wenzetu Unakuta chumba kimoja ni Dola 1000$ Kwa mwezi hiyo hela ambayo Kwa tz ni millio 2 na ushee Sasa kama unakuta mpenda sifa anakodi vyumba vitatu Kodi zaidi ya 3500$ Kwa mwezi Sasa hapo Bado bills zingine etc ..kama una malengo na Tanzania Inabidi ghetto lako liwe na kitanda na vitu vichache Sana kuepuka unnecessary cost..kula Bata Kwa mahesabu Kila unachopata pigia calculation ya kuwekeza Tanzania,kule utaishi maisha magumu lakini Kwa kuwekeza huku tz utajikuta huku unakuwa tajiri hata kuweza kufungua pub ,guest house na hata kumiliki viwanja

Wengi wanajisahau sana na ndomana wakirudi wanakuwa wamepigika sana , kiukweli wengi wanarudi tz wanaona aibu hata kusema kama wamekuja kutoka marekani...maisha ukiwa na nidhamu nayo unatoboa ,mim nawakubali sana wanigeria wao wako makini sana aisee japo nao ndo kuaminika ni shida ..
Kiukweli fursa ni nyingi sana ila kikubwa ni mtu kujitambua ,Sasa wengi wakienda USA kazi kupiga picha maeneo ya Bata na kuringishia Facebook ila kiuhalisia unakuta Hana hata kiwanja alichonunua bongo Kwa ajili ya kujenga na unakuta kwakuwa kule ni kuzuri sana na mazingira yanavutia unajikuta miaka 10 imekatika hakuna lolote ulilofanya ukija kurudi bongo wenzako wamepiga hatua unajikuta pressure inakuandama ..Kuna kazi nyingi za kubeba mabox ,usafi wa garden ,kunyoosha nguo za watu zinalipa sana ila Sasa uwe na akili ya kuwekeza nchini kwako
 
Mchokoza mada / thread / mgongano wa diaspora na waliobaki nyumbani kuhusu mambo kadhaa na mitizamo

Professor Joseph Mbele kuhusu tofauti za maono, fikra, mawazo, kitamaduni pia mkorogano na tafrani katika dunia hii ya kijijini afafanua kupitia kitabu : Kuku Ndani Ya Bus


View: https://m.youtube.com/watch?v=Au4IbTrlWkc
Prof. Joseph Mbele kuhusu wamarekani na tamaduni kila mtu kupigana kimaisha mwenyewe hakuna kujali Shangazi, mjomba, binadamu wala wa kutoka kijiji kimoja.....

Kaka yenu yupo Marekani mwambieni awalipie ada ya shule, mchango wa harusi ... hiyo haipo katika tamaduni za Marekani na Ulaya ... Kukopeshana kwa mali kauli haipo sana Marekani kama ilivyo Tanzania au Afrika .....
Source : America Swahili News
 
Mkuu kuna mmoja juzi katoka Marekani ni mshikaji wetu kitaani yaani jamaa kachoka utadhani alikuwa gerezani,Amefika kuona nina drive Bima(BMW) anabaki kunishangaa na kunipa masifa kibao!

hiki ndo kimefanya nimeandika uzi!
Wee Ni mpumbavu SAS Ni kwamba hujawi kwenda popote uko tu hapo mbeya unajiona umefika Sasa hyo bm yako na hi mashine ipi na ipi
 

Attachments

  • IMG-20230907-WA0010.jpg
    IMG-20230907-WA0010.jpg
    163.6 KB · Views: 4
Umenikumbusha kuna siku tumeenda kunywa rafiki yangu alikuja na jamaa yake (kaka) akamtambulisha anatoka marekani!!….
Khaaah ama nilishangaa jamaa bill zote hana hata mia mbovu ya kuchangia si chakula ci vinywaji anajichekesha tu…..
Had mademu wakaanza kumtania

Naunga mkono hoja hawana hela mwili mkubwa lakin hamna hata aibu kula vya wanaume tu[emoji3][emoji3]
Dah![emoji51][emoji51][emoji51][emoji51][emoji51]
 
Mkuu kuna mmoja juzi katoka Marekani ni mshikaji wetu kitaani yaani jamaa kachoka utadhani alikuwa gerezani,Amefika kuona nina drive Bima(BMW) anabaki kunishangaa na kunipa masifa kibao!

hiki ndo kimefanya nimeandika uzi!
Kuna gari inaitwa "Bima"?

Napata shaka kama kweli hata gari unayo kweli.
 
Ukihitaji salamu nenda pwani kwa waswahili,kwangu utaambulia chuya ukalishie kuku!

Bado sijafahamu ni kwanini watanzania wengi wanaoishi nchi za Marekani,Canada na Uk huwa wanamaisha magumu kupita kiasi tofauti kabisa na wale wanaoishi nchi za Scandinavian na Germany!.

Ninawafahamu jamaa kadhaa wanaoishi huko tangu zamani na hakuna walichofanya cha maana kwenye familia zao(Wazazi) hapa Tanzania,wengi huwa wanarudishwa kipindi cha matatizo tu lakini huwezi kuwaona wakiwa wanarudi kipindi cha furaha kuwasalimia ndugu zao.

Watanzania wengi wanaoishi nchi za Scandinavian huwa wamerekebisha makazi ya wazazi wao na pia huwa wamejenga nyumba za kifahari ili wanapokuwa wanakuja likizo basi hufikia huko,siyo nyumba tu bali huwa na usafiri mzuri!.

Hii ni tofauti kabisa na wabongo wanaoishi Marekani,Canada na UK,hawa huwa wanarudi makwao endapo Baba au Mama ni mgonjwa au amefariki kabisa,na huwa wakija hata vaa yao inatia mashaka!.

Huwa wanapenda kuvaa miwani mikubwa kama wachomelea welding na kujifanya kuishangaa Tanzania kana kwamba ni chooni!,Unakuta hata hela ya kuwatoa marafiki zake tu Out hawana zaidi ya kujiongelesha blah blah na masifa kibao!.Wengi wamechoka kimuonekano,Sura hazina nuru na mionekano yao imefubaa!.

Ukiwauliza wanabaki kusingizia Marekani Kodi ni kubwa na Ishu za Bills zinabana kila kona,Unabaki kumshangaa kana kwamba huko Marekani ni yeye tu ndiye Bills hupewa kubwa!.

Wabongo wengi wanaoishi Marekani na Canada waliofanikiwa huwa ni kuanzia Umri wa Miaka 50 - na Kuendelea,hawa ndiyo angalau huwa wamejenga makwao na hata hujitahidi kuprovide kwenye familia zao.

Ila hawa wenzangu na mie kuanzia miaka 25 - 45 huwa hawana cha maana zaidi ya blah blah na ngonjera kibao huku kila muda wakipiga simu na kusimanga serikali na kuwakashifu ndugu kana kwamba wanaishi kwenye vyoo!.


Wengine tunawafahamu wamekwenda huko miaka ya 90 lakini hadi leo ni kuzurura tu hawana paper!.

Any way:

Ukitaka kuona walivyo na hasira,wewe soma comments!
Acha uongo na mjumlisho. Kwani umeongea na au unawajua wote? Mbona wapo wenye maisha mazuri tu wanamilki kila kitu wazungu wanamilki? Hata huko scandinavia kwako wapo wachovu. Ni kitu cha kawaida katika maisha.
 
Hapo pia tunatofautiana maana mimi huku sikuja kwa njia za kimagumashi. Nilikuja kwa ajili ya kusoma lakini nimepata kazi, pia malipo sio mabaya. Na mazingira ya kazi pia sio mabaya. Ndo nakomaa na lugha hapa nina A2 nimeanza B1 hii October.
Endelea kujinadi uanzwe kufuatwa P.M na ombaomba wa JF na mashoga wakiwemo

Usipende kuweka wazi kila kitu kukuhusu hata kama tunajadili mada. Privacy ni muhimu.

Watu hawawezi kukiharibu wasichokijua. Behave!
 
Hivi Uzi mnausoma lakini au mnataka tu kuja kukomenti muonekani?

Nani amezungumia masuala ya Uchumi baina ya nchi na nchi?

HOJA

Ni kwanini Wabongo wengi wanaoishi Marekani,Canada na Uk wanamaisha Magumu ukilinganisha na wenzao wa Scandinavian pamoja na Germany

Hiyo ndiyo hoja lakini siyo ulichoandika wewe
Niishie kukueleza kwamba unachokijua ni kusoma tu ila kuelewa bado.
 
Back
Top Bottom