Wabongo wengi wanaoishi Marekani wana maisha magumu tofauti na wale wanaoishi nchi za Scandinavian

Wabongo wengi wanaoishi Marekani wana maisha magumu tofauti na wale wanaoishi nchi za Scandinavian

Ukihitaji salamu nenda pwani kwa waswahili,kwangu utaambulia chuya ukalishie kuku!

Bado sijafahamu ni kwanini watanzania wengi wanaoishi nchi za Marekani,Canada na Uk huwa wanamaisha magumu kupita kiasi tofauti kabisa na wale wanaoishi nchi za Scandinavian na Germany!.

Ninawafahamu jamaa kadhaa wanaoishi huko tangu zamani na hakuna walichofanya cha maana kwenye familia zao(Wazazi) hapa Tanzania,wengi huwa wanarudishwa kipindi cha matatizo tu lakini huwezi kuwaona wakiwa wanarudi kipindi cha furaha kuwasalimia ndugu zao.

Watanzania wengi wanaoishi nchi za Scandinavian huwa wamerekebisha makazi ya wazazi wao na pia huwa wamejenga nyumba za kifahari ili wanapokuwa wanakuja likizo basi hufikia huko,siyo nyumba tu bali huwa na usafiri mzuri!.

Hii ni tofauti kabisa na wabongo wanaoishi Marekani,Canada na UK,hawa huwa wanarudi makwao endapo Baba au Mama ni mgonjwa au amefariki kabisa,na huwa wakija hata vaa yao inatia mashaka!.

Huwa wanapenda kuvaa miwani mikubwa kama wachomelea welding na kujifanya kuishangaa Tanzania kana kwamba ni chooni!,Unakuta hata hela ya kuwatoa marafiki zake tu Out hawana zaidi ya kujiongelesha blah blah na masifa kibao!.Wengi wamechoka kimuonekano,Sura hazina nuru na mionekano yao imefubaa!.

Ukiwauliza wanabaki kusingizia Marekani Kodi ni kubwa na Ishu za Bills zinabana kila kona,Unabaki kumshangaa kana kwamba huko Marekani ni yeye tu ndiye Bills hupewa kubwa!.

Wabongo wengi wanaoishi Marekani na Canada waliofanikiwa huwa ni kuanzia Umri wa Miaka 50 - na Kuendelea,hawa ndiyo angalau huwa wamejenga makwao na hata hujitahidi kuprovide kwenye familia zao.

Ila hawa wenzangu na mie kuanzia miaka 25 - 45 huwa hawana cha maana zaidi ya blah blah na ngonjera kibao huku kila muda wakipiga simu na kusimanga serikali na kuwakashifu ndugu kana kwamba wanaishi kwenye vyoo!.

Wengine tunawafahamu wamekwenda huko miaka ya 90 lakini hadi leo ni kuzurura tu hawana paper!.

Any way:

Ukitaka kuona walivyo na hasira,wewe soma comments!
Kwa jinsi ulovyoeleza waweza kuwa sahihi kwa asilimia 80.

Mimi ni mmoja wa wale tulokwenda huko majuu miaka ya zamani na nikarudi Bongo kitambo sana kuweka sawa vitega uchumi vya kawaida sana.

Nina vibiashara vyangu vidogovidogo na nimeajiri vijana kadhaa ambao huniwekea fedha kwa akaunti yangu kila mwisho wa mwezi.

Huwa nachungulia tu mpunga kila mwisho wa mwezi.

Ukweli ni kwamba Ughaibuni kitu cha kwanza kabisa kuhakikisha umefanya ni kupata ukaazi wa kudumu na baada ya hapo wapiga kazi. mambo mengine yote watakiwa kuweka kapuni hadi hapo ukaazi utapotia timu.

Hivyo haijalishi umeenda kama mtembezi, mkimbizi au kusoma lengo ni lilelile kuhakikisha wapata ukaazi, kama si hivyo waenda kufanya nini kule?

Kinosumbua wengi ni ukaazi wa kudumu kwani ukipata ukaazi wa kudumu kwenye elimu huweza kupata mkopo wa kulipia ada ya university na pia huweza kupata hata nyumba za bei nafuu. Wengi wa wale ambao wamepoteza muda kusaka ukaazi hujikuta wakiwa na kazi za maana tayari wana familia hivyo huwa kama wameanza upya.

Ndo maana maisha yao huwa ni yale ya kujitosheleza wao na familia zao na sio "extended families". Hata wakija hapa Bongoland huonekana wamepigika khasa kutokana na kazi za kule. Kule usipokuwa mwangalifu aweza kuvunja mgongo kwa kufanya kazi zisizo na tija sana kisha kumpoteza hata manzi wako kama weye ni mwanamme.

Hivyo kazi ni jambo la msingi sana kuangalia ni kazi ya aina ipi itakutoa.

Nikisema kazi si kazi za "manual labour" bali ni kazi za kitaalam ambazo utakuwa na ujuzi nazo ambazo zitakupa kiasi cha kama (kwa fedha za madafu) milioni 8 kwa mwezi yaani pauni 2,900 hivi au euro 3,300 hivi au dola 3,500.

Yaani, kima cha chini cha mshahara wa mwaka baada ya kodi kwa Uingereza kiwe ni pauni 35,000, au dola 42,500 au euro 40,400.

Kwa UK mshahara wa 2900 kwa mwezi ukiwa na nyumba ya kawaida nje ya London ni wastani wa pauni 800 kwa mwezi (nyumba ya vyumba viwili), kodi ya maendeleo 110, na bills zote umeme, maji, 200, simu, chakula, na bills zingine ndogondogo.

Kwa hapa states nilipo, ni kama dola 750 kwa mwezi kwa pango na vikodi vingine ni dola 1000 hivi.

Hizo nchi za Scandinavian zina kodi kubwa sana kwenye mshahara hiyo ni lazima uwe umesoma na una kazi ya maana sana hivyo si kweli kusema watu wake wengi wageni hutoboa labda awe ni mkimbizi au kaoa/olewa na mzungu ambae ana uwezo.

Nchi kama Sweden na Finland ambazo elimu ni bure wageni wengi wana kazi nzuri khasa wasomali lakini ukifika miji kama Stockholm au Sundisvall wageni wengi wafanya kazi za kawaida sana khasa kwenye mahoteli na sehemu za public na wana mishahara midogo.

Sasa vijana wengi walokimbilia huko wa umri kati ya 25-45 kama hawakusoma basi huishia kufanya kazi zisizolipa mishahara minono na hivyo maisha yao huwa ni ya kawaida sana na kama wameingia kwenye mahusiano basi ndo huwa mwisho wa safari yao ya ahadi kwenda kwenye nchi ya asali na maziwa.

Kuna baadhi ya kazi ambazo ukizipata waweza kutoboa Ughaibuni ndani ya miaka miwili, "provided" umezisomea na una ujuzi nazo kama miezi 12 hadi 18, wazungumza kingereza safi, una uwezo wa kuzikiliza maelekezo na huna rekodi za kihalifu.
 
Oyooooooooo!!! Tajiri kaongea sasa!!!
TUKANA UONE kumbe thamani ya nyumba yako ya madale ya 280millions Kiranga anahifadhia mbwa wake 😂😂😂😂

Una lolote la kuongezea tajiri??
Hapa leo tuna matajiri wawili
Kiranga vs TUKANA UONE
Mpambano mkareee kweri kweri wadau mna maoni yoyote??? 😂😂😂😂😂
Kidumu cha petroli ezi yujo! Carleen njoo uone huku🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️
 
Kufika wapi ambako mipango imegoma? Mimi huko kwenu ntakuja kutalii mambo ikikaa sawa sio kuishi ,siwezi ishi sehemu ambayo Kila mtu ana habari zake no social cohesion kama ya Bongo.

Kiufupi sijawahi tamani kuishi Nje ya Nchi ila natamani kufika kuona kulivyo.
Weye waonekana (kama si vinasaba vya uchawa) huwa una mawazo positive sana.
 
Ukihitaji salamu nenda pwani kwa waswahili,kwangu utaambulia chuya ukalishie kuku!

Bado sijafahamu ni kwanini watanzania wengi wanaoishi nchi za Marekani,Canada na Uk huwa wanamaisha magumu kupita kiasi tofauti kabisa na wale wanaoishi nchi za Scandinavian na Germany!.

Ninawafahamu jamaa kadhaa wanaoishi huko tangu zamani na hakuna walichofanya cha maana kwenye familia zao(Wazazi) hapa Tanzania,wengi huwa wanarudishwa kipindi cha matatizo tu lakini huwezi kuwaona wakiwa wanarudi kipindi cha furaha kuwasalimia ndugu zao.

Watanzania wengi wanaoishi nchi za Scandinavian huwa wamerekebisha makazi ya wazazi wao na pia huwa wamejenga nyumba za kifahari ili wanapokuwa wanakuja likizo basi hufikia huko,siyo nyumba tu bali huwa na usafiri mzuri!.

Hii ni tofauti kabisa na wabongo wanaoishi Marekani,Canada na UK,hawa huwa wanarudi makwao endapo Baba au Mama ni mgonjwa au amefariki kabisa,na huwa wakija hata vaa yao inatia mashaka!.

Huwa wanapenda kuvaa miwani mikubwa kama wachomelea welding na kujifanya kuishangaa Tanzania kana kwamba ni chooni!,Unakuta hata hela ya kuwatoa marafiki zake tu Out hawana zaidi ya kujiongelesha blah blah na masifa kibao!.Wengi wamechoka kimuonekano,Sura hazina nuru na mionekano yao imefubaa!.

Ukiwauliza wanabaki kusingizia Marekani Kodi ni kubwa na Ishu za Bills zinabana kila kona,Unabaki kumshangaa kana kwamba huko Marekani ni yeye tu ndiye Bills hupewa kubwa!.

Wabongo wengi wanaoishi Marekani na Canada waliofanikiwa huwa ni kuanzia Umri wa Miaka 50 - na Kuendelea,hawa ndiyo angalau huwa wamejenga makwao na hata hujitahidi kuprovide kwenye familia zao.

Ila hawa wenzangu na mie kuanzia miaka 25 - 45 huwa hawana cha maana zaidi ya blah blah na ngonjera kibao huku kila muda wakipiga simu na kusimanga serikali na kuwakashifu ndugu kana kwamba wanaishi kwenye vyoo!.

Wengine tunawafahamu wamekwenda huko miaka ya 90 lakini hadi leo ni kuzurura tu hawana paper!.

Any way:

Ukitaka kuona walivyo na hasira,wewe soma comments!
Mtu wa miaka 25 sio mwanafunzi huyo? Ugenini ni ugenini tu sio kwao na kama ulivyosema wengine hawana uhalali wa kuishi huko, basi hata kujikimu itakuwa ni kwa kuunga unga.
Na mipango ya mtu huwezi ijua, kama ameamua maisha yake yote yawe huko, Tz atakuja kuwekeza nini? Itamlazimu awekeze sehemu mbili, na hapo maisha yatakuwa magumu.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Una exposure ndogo sana ndio maana unabwabwaja vitu usivyojua. Kwa kifupi manual skills job kama mechanic, plumbing, carpenter nk zinalipa sana tu kuliko hata baadhi ya white color job.
Ni kweli, lakini mimi nimefanya kazi kwenye construction industry nimeona ni wazungu na wahindi ndo wenye nafasi kubwa ya kushinda tender za kazi kuliko kampuni ya mtu mweusi.

Kampuni za wazawa weusi zipo lakini ni chache sana kulinganisha na makampuni ya wazungu ambao wana connections na hupeana kazi.

Ila uko sawa hizo kazi hulipa sana ila hutegemea na kushinda contracts na ni lazima uwe na kampuni la sivyo hutoboi.
 
Kwa hali ilivyo sasa kutoboa Marekani ni vigumu sana. Haki za mfanyakazi ni ndogo na pia mfumo wa bima ya afya ni mbovu. Ujerumani ni nchi nzuri sana lakini mpaka uje ujiseti inabidi upate cheti cha huku huku na ujue lugha. Huku malipo yako poa na mfanyakazi unalindwa sana.

Kwa kumalizia mimi naona ukishafanya kazi kwa miaka mitano ukawa na experience ya kutosha kwenye field yako Bora urudi Bongo. Maana kama una mtaji unaweza hata ukaanzisha biashara yako.
Biashara gani Tz utafanya kwa mafanikio? Watu wanakuja kuwekeza, wanaishia kila siku kuandamwa na kodi, ushuru na ada zisizoeleweka, bado hujaingelea rushwa na wizi. Taratibu, mikataba, haiheshimiwi, haifuatwi, ila kauli ya ccm. WaTz wa Scandinavia waliwekeza Bagamoyo, kwa kukaribishwa na awamu ya 4, imekuja ya 5, hawatakiwi tena.
Kila siku kuchomeana moto biashara, mara pesa zinashiliwa benki, umeswekwa ndani, bado hujapigwa marufuku usiuze mazao nje, yaliyokutoa jasho na pesa kipinfi chote cha kilimo.
Ni biashara gani utaifanya kwa uhakika Tz?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Ukihitaji salamu nenda pwani kwa waswahili,kwangu utaambulia chuya ukalishie kuku!

Bado sijafahamu ni kwanini watanzania wengi wanaoishi nchi za Marekani,Canada na Uk huwa wanamaisha magumu kupita kiasi tofauti kabisa na wale wanaoishi nchi za Scandinavian na Germany!.

Ninawafahamu jamaa kadhaa wanaoishi huko tangu zamani na hakuna walichofanya cha maana kwenye familia zao(Wazazi) hapa Tanzania,wengi huwa wanarudishwa kipindi cha matatizo tu lakini huwezi kuwaona wakiwa wanarudi kipindi cha furaha kuwasalimia ndugu zao.

Watanzania wengi wanaoishi nchi za Scandinavian huwa wamerekebisha makazi ya wazazi wao na pia huwa wamejenga nyumba za kifahari ili wanapokuwa wanakuja likizo basi hufikia huko,siyo nyumba tu bali huwa na usafiri mzuri!.

Hii ni tofauti kabisa na wabongo wanaoishi Marekani,Canada na UK,hawa huwa wanarudi makwao endapo Baba au Mama ni mgonjwa au amefariki kabisa,na huwa wakija hata vaa yao inatia mashaka!.

Huwa wanapenda kuvaa miwani mikubwa kama wachomelea welding na kujifanya kuishangaa Tanzania kana kwamba ni chooni!,Unakuta hata hela ya kuwatoa marafiki zake tu Out hawana zaidi ya kujiongelesha blah blah na masifa kibao!.Wengi wamechoka kimuonekano,Sura hazina nuru na mionekano yao imefubaa!.

Ukiwauliza wanabaki kusingizia Marekani Kodi ni kubwa na Ishu za Bills zinabana kila kona,Unabaki kumshangaa kana kwamba huko Marekani ni yeye tu ndiye Bills hupewa kubwa!.

Wabongo wengi wanaoishi Marekani na Canada waliofanikiwa huwa ni kuanzia Umri wa Miaka 50 - na Kuendelea,hawa ndiyo angalau huwa wamejenga makwao na hata hujitahidi kuprovide kwenye familia zao.

Ila hawa wenzangu na mie kuanzia miaka 25 - 45 huwa hawana cha maana zaidi ya blah blah na ngonjera kibao huku kila muda wakipiga simu na kusimanga serikali na kuwakashifu ndugu kana kwamba wanaishi kwenye vyoo!.

Wengine tunawafahamu wamekwenda huko miaka ya 90 lakini hadi leo ni kuzurura tu hawana paper!.

Any way:

Ukitaka kuona walivyo na hasira,wewe soma comments!
Mbona mizinga haiishi?
 
Wewe una matatizo,maisha Yako ya Daraja 3 Kwa Kila Nchi ,Sasa ukifika Marekani utaishia Daraja lipi? Hata Tanzania hapa wapo wa Maisha ya Juu,ya kati na chini kama kwingine Sasa unaposena viongozi

Nimefika Nchi za Africa kadhaa ila Nje ya Nchi Bado na Africa yote Kwa sehemu kubwa inafanana.

Huko Ulaya nk nakuona kwenye picha,video nk na pia nasoma Hali ya maisha, biashara na Uchumi lakini siwezi kutamani.kuishi huko ila kufika na ntafika before 2030 nikiwa mzima.

Nitapata exposure na experience Mpya ila siwezi tamani kuishi Kwa sababu tayari ntakuwa nimejiwekeza Afrika.
Sawa
 
Wewe una matatizo,maisha Yako ya Daraja 3 Kwa Kila Nchi ,Sasa ukifika Marekani utaishia Daraja lipi? Hata Tanzania hapa wapo wa Maisha ya Juu,ya kati na chini kama kwingine Sasa unaposena viongozi tuu ndio wanaishi maisha mazuri kisa viongozi sio kweli,hao viongozi ni wachache kuliko wengine.

Kinachonikera hapa Tanzania ni kwamba Ukiwa na vihela Ili uwe salama inatakiwa uwe Chana tawala hata kama hutaki hii ndio kero kubwa Sasa kiasi kwamba huna uhuru wa Mali Yako.
👍
 
Huu ujinga ndio Huwa naukataa,Nchi hizo ziko very exhausted kwenye Kila nyanja ya uchumi.

Afrika ndio Kuna fursa ingawa Changamoto ya Afrika ni mtaji na sio fursa.Binafsi uniambie nichague kazi Ulaya na Afrika nachagua Afrika
Afrika ukikomaa hauchelewi kupata mtaji wa kuwa na boda boda tuu Nje kuna mitaji na unakuja kuwekeza Afrika mtu mwenye Njaa ya mafanikio Nchi zilizoendelea ni sahihi kwake kwa kuchanga...
 
Ushindwe kutoboa Marekani wewe utakuwa mwehu , unless uwe na matatizo ya kiafya au huna Status ya ukazi WA kudumu .
Nchi yenye upward social mobility kama ile ukilinganisha na huu upuuzi wa hapa Bongo , utakuwa fala .watu toka kila pembe ya dunia unayoijua wewe wako pale na wanazidi kuja kuanzisha life hapo ,na kila siku wanazalisha mamilionea na mabilionea .
 
Back
Top Bottom