Wabunge 19 wa CHADEMA watinga Mlimani City


Kama Mrema kasema maamuzi yameshafanyika, kavuruga process nzima ya huo mchakato
 
Hawana kosa wale mbona yule mmoja wa jimboni hawamgusi
 
Kwahiyo sasa hivi mmeyakubali matokeo?? Mna tofauti gani na hao 19 ambao waliamua kukubali matokeo mapema?
Mkuu kutoyatambua matokeo ni swala lingine na KUFOJI BARUA YA KUJITEUA UBUNGE KINYEMELA KWA MSAADA WA NDUGAI ni swala jingine pia.......... USICHANGANYE

Hakuna uchafuzi ambao CDM imewahi kuyatambua matoke, sio huu uliopita tu hata chaguzi za nyuma zote haikuzitambua

CDM inautaratibu wake unao badilika badilika katika kuonyesha kwamba HAIKUBALIANI na HAITAMBUI matokeo ya chaguzi za KIHUNI
 
Nashauri wapelekwe bungeni wengine, hao wasamehewe yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
 
Sijui umeongea nini hapa? Unajua misimamo ya viongozi wengi Chadema wakati ule? Unafikiri msimamo wa Dr Slaa ungekuwa wa Mbowe na ule wa Mbowe ndio wa Dr Slaa unafikiri bado wangesimama na Dr Slaa?

Tatizo mnafikiri sisi wote ni sehemu ya propaganda za vyama. Tumesoma mchezo kitambo. Mbowe kuendesha Chadema kwa maono yake sio tatizo! Hata Nyerere amekijenga chama chake muda mrefu. Lakini pale tunapoona vitu havipo sawa. tutasema kwa kipimo kile kile tunachoisema CCM.
 
Wasamehewe tu kazi iendelee !! Hakuna asiyekosa !! Akina Halima Mdee na wenzie ni miongoni mwa wabunge machachari na mashuhuri Nchini !!
Umachachari uliishia pale aliposaliti! Ukiwa msaliti hata kama una akili za malaika wewe ni shetani tu!! Tupa kuleeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kila siku mnabadili sababu. Mwanzo kabisa chama kilisusia kila kitu kinachohusiana na serikali
Usichanganye mkuu
Chama kikisusia hakina MAMLAKA ya kumzuia mbunge wake aliyechaguliwa na wananchi asiende kuwawakilisha bunge, kikimshauri asiende na akaamua kwenda inakua sio busara kumfukuza uanachama kwa kigezo hicho

Lakini hawa wahuni akina mzee mdee walifoji barua ya chama na wakajiteua kinyemela huku wengine wakiachiwa gerezani usiku saa2 na kesho yake wanaapishwa nje ya viunga vya bunge na muhuni Ndugai

Tatizo kuu hapa ni kufoji barua ya chama na kujipendekeza kihuni kwa msaada wa mtesi wao ccm
Inamaana hamlioni hili mkuu?
 
Hakika nimeamini kifo cha marehemu hayati magufuli lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa baadhi ya watu hadi ndani ya ccm ,na sababu jinsi katiba ilivyokanyagwa awamu ya 5
 
Kila siku mnabadili sababu. Mwanzo kabisa chama kilisusia kila kitu kinachohusiana na serikali
Hiki chama huwa kipokipo tu, katika hili mimi naona hakuna cha maana wanachofanya maana wanateua wabunge wengine (wanaowaita halali😀) baada ya kuisusia serikali kwa muda wa mwaka mmoja.

Wale 19 hawakuona sababu ya kuisusia serikali kama ambavyo wao wamelitambua sasa, kwamaana nyingine wale 19 walikuwa mbele ya muda.

Kwasasa wanafanya maamzi kwakuwa njaa umekuwa ni kali, wasingeweza kususia kwa miaka mitano.
 
Kwahiyo hawa wa sasa mnaowachagua wanaingia bungeni kushirikiana na wabunge waliopita kwenye uchaguzi upi wa halali?

Maana kuanzia spika na wengine wote ni matokeo ya ule uchaguzi, nakumbuka mliwahi kusema bunge na kila kitu ni batili kwahiyo nilidhani hamtakuwa tayari kuchangamana nao.

KAZI IENDELEE😀
 
Watabadili gia kuwa adui yao alikua magufuli pekee(yaani peke yake ndie aliyeiba kura)na sio serikali ya ccm(hawa hawakuiba kura bali walifata maelekezo ya magu😂😂). Hivyo serikali ya sasa ni halali kwa upande wao
 
Sijachanganya chochote mkuu. Mbona yeye hatajwi kwa utovu wa nidhamu. Hakushauriwa bali Alizuiwa (ni ri sio ombi wala ushauri)asiende nae ajumuishwe kama msaliti na ahojiwe sababu za kugomea viongozi wake
 
Sijui kwanini hujaelewa nilichoandika, sijataka hata unilalamikie.

Hapo nilikuonesha tu, kama Dr. Slaa alikuwa anajitambua kweli angekataa kuburuzwa na mawazo ya Mbowe kama ulivyoandika kule juu, usilete hisia zako kwenye kuamua uhalisia kwa kisingizio cha "umeusoma mchezo kitambo".

Umeandika hisia zako halafu unasema wewe sio sehemu ya propaganda! kama kweli wewe sio sehemu ya propaganda nipe mifano mitatu yenye evidence kuonesha vile Mbowe anavyoiburuza Chadema kwa maamuzi yake binafsi.
 
Sijachanganya chochote mkuu. Mbona yeye hatajwi kwa utovu wa nidhamu. Hakushauriwa bali Alizuiwa (ni ri sio ombi wala ushauri)asiende nae ajumuishwe kama msaliti na ahojiwe sababu za kugomea viongozi wake
Since day one waliitwa Covid 19, Kosa lao ni kufoji barua ya uteuzi kwa msaada wa ccm.... sio covid 20. Hata siku moja hujasikia uongozi ukiongea lolote kuhusu mbunge mchaguliwa sababu wanajua sheria

Kisheria chama hakiwezi KUMZUIA mbunge aliyechanguliwa na wananchi asiende kuwawakilisha, ni kuwakosesha haki yao ya kikatiba kuwakilishwa na mbunge walio mchagua

Narudia tena KOSA hapa ni KUFOJI BARUA YA KUJITEUA na sio vinginevyo
Naona unalazimisha kosa kuhalalisha uhuni wa mzee mdee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…