Wabunge 19 waliofukuzwa CHADEMA ni wahujumu pale Bungeni

Wabunge 19 waliofukuzwa CHADEMA ni wahujumu pale Bungeni

Siasa zetu ni nafasi za ulaji tu,
Waacheni watu wajipatie kipato.

Wakiondoka hiyo pesa wanayopata mtachakua nyinyi.?
Si itatafunwa tu na wajanja.

Acheni wivu fanyeni kazi.
 
Baada ya miaka 100 hakuna atakaekuwepo. Labda wayafungulie kesi makaburi yao. Halafu futa wazo la chama kingine kuingia madarakani hivi karibuni. CCM bado ipo sana.
Nimesema hata miaka 100....HATA..
 
Kesi ipo mahakamani sawa, lakini ujue zinapewa maelekezo kutoka juu ya kutosoma hukumu mapema mpaka 2025 au unajifanya hujui.
Covid hakuna jina lolote linaloweza kutamkwa dhidi yao.

Ni covid 19 tu
 
Hao wanachama walioandamana hawajitambui. Hakuna uhujumu wowote kwasababu hata kama kina mdee wasingewazidi akili lazima michepuko, ndugu, na wake za vigogo wa CHADEMA wangechukua hizo nafasi. Kwanza hata katika hilo kundi la Covid19 kuna mke wa Kigaila ambaye ni kiongozi mkubwa wa CHADEMA.
Bado hujaeleweka naomba tulia andika vizuri
 
Siasa zetu ni nafasi za ulaji tu,
Waacheni watu wajipatie kipato.

Wakiondoka hiyo pesa wanayopata mtachakua nyinyi.?
Si itatafunwa tu na wajanja.

Acheni wivu fanyeni kazi.
Haya uliyo andika ndiyo tunaitaga mawazo ya vijiwe samri au vijiwe vya wavua chaza.
 
Kiukweli tuna wanachama wenye akili za ajabu sana humu kwenye vyama vyetu, wale ni wabunge 19 wa viti maalum Chadema, ni wabunge halali kabisa kwa mujibu wa taratibu zote za kibunge!. Wanawake hawa wanaoandamana sasa, ningewashauri wasubiri kwanza matokeo ya kesi iliyopo Mahakamani!, ndipo waandamane.

P
Wewe Pascal Mayalla nguli wa masuala ya kisheria nini kimekupata siku hizi?
Namna walivyoingia hawa wabunge 19 mgogoro na chama chao cha Chadema unajua kabisa ila unajifanya hujui!
 
Hao wanachama walioandamana hawajitambui. Hakuna uhujumu wowote kwasababu hata kama kina mdee wasingewazidi akili lazima michepuko, ndugu, na wake za vigogo wa CHADEMA wangechukua hizo nafasi. Kwanza hata katika hilo kundi la Covid19 kuna mke wa Kigaila ambaye ni kiongozi mkubwa wa CHADEMA.
Is your statement FACT or OPINION
 
Hayo majimbotayohongwa 2025 yatakua hayana utofauti na hao kina mdee.
 
Mkuu hawa wanajandalia kesi ya uzeeni tu maana jinai haifutiki hata baada ya miaka 100.

Siku ukiingia uongozi wa chama tofauti na ccm basi hawa lazima watalipa fedha za watanzania.
Mwenye makosa makubwa ni spika ambaye anavunja katiba kwa kutotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na katiba.
 
Yale ni maigizo yenye baraka za CCM kificho! Chadema wanaingia kwenye maigizo ya aibu.
 
Yale ni maigizo yenye baraka za CCM kificho! Chadema wanaingia kwenye maigizo ya aibu.
Kama kuna watu akili zao aliondoka nazo Jiwe basi ni uvccm ukiwepo na wewe
 
Back
Top Bottom