Wabunge 7 wanaotajwa kuwa na michango yenye mashiko Bunge la 13, 2025

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
435
Reaction score
733
Wabunge wenye michango yenye mashiko katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wapo wengi. Lakini hapa wanatajwa wabunge 7 tu ambao wakipewa nafasi ya kuongea, michango yao au hoja zao hutikisa bunge lenyewe na kuvuka mipaka hadi mitandaoni, wakati mwingine mpaka kurasa za mbele za magazeti nchini.

Wakati mwingine, hoja zao uhofiwa kuitwa kwenye kamati ya maadili kuhojiwa lakini hulindwa na sheria za Bunge ambapo mbunge anapotoa mchango bungeni hakosei ili mradi hamtaji mtu kwa jina.
Wabunge hao siyo kutoka vyama vya upinzani tu bali hata chama tawala ambapo kimeshika dola, yaani Chama cha Mapinduzi (CCM).

Michango ya wabunge hao siyo ya kuikosoa serikali bali ni kwa ajili ya kuisaidia nchi kufikia maendeleo ya kweli na uwajibikaji kwa viongozi wenye dhamana.

Pia michango yao huungwa mkono na sehemu kubwa ya jamii kwa sababu ina mwelekeo wa kuwatetea wanyonge na kudumisha utendaji wa serikali katika kuleta maendeleo.

Kihistoria na hivi karibuni, wabunge hao wamechangia mijadala yenye kushutumu wizi, ubadhirifu, ufujaji wa pesa za serikali, ufisadi wa kutopea na utendaji mbovu wa baadhi ya watumishi wa umma.
Aidha, bila kuacha 'kuililia' serikali kuhusu matatizo ya kwenye majimbo yao, wabunge hao wamekuwa wakishauri namna ambavyo serikali inaweza kukomesha ufisadi huo au uzembe wa watendaji.
Majina ya wabunge hao na vyama vyao katika mabano ni kama ifuatavyo;

1. Ahmed Mabukhut Shabiby (CCM-hoja zake zinalenga ufisadi, wizi).
2. Revocatus Chiponda 'Baba Levo' (CCM-hoja zake zinalenga ushauri).
3. Joseph Kasheku Musukuma (CCM-hoja zake zinalenga utendaji mbovu).
4. Kangi Alphaxard Lugola (CCM-hoja zake zinalenga ufisadi, wizi)
5. Ado Shaibu Ado (ACT- Wazalendo-hoja zake zinalenga ukosoaji).
6. Pascal Lucas Lutandula (CCM-hoja zake zinalenga mabadiliko).
7. Livingstone Joseph Lusinde (CCM-hoja zake zinalenga uadilifu).

Kwa ujumla, wabunge hao bila kusita au kumung'unya maneno, wanaelezwa kwamba wamekuwa wakichangia kwa kuyakemea mambo ambayo yanaonekana kuchelewesha au kusumbua maendeleo ya nchi, kama ilivyoelezwa hapo juu.

Wabunge hao katika michango yao, hawana rangi ya 'damu ya mzee' bali nyekundu. Hawana rangi ya 'machungwa', ila njano. Hawana rangi ya 'bluu bahari' isipokuwa bluu. Hawana rangi ya 'kijani kibichi', zaidi ya kijani.

Hivi karibuni kumekuwa na mijadala kutoka kwa baadhi ya wananchi, wakiwemo watu maarufu, wanaodai kuwa, bunge limekosa mwelekeo. Wananchi hao wanadai kwamba, wabunge hawajadili mambo ya maana zaidi ya porojo huku wakishutumiwa kuwaona Watanzania ni wajinga.

Lakini ukweli ni kwamba, wapo waheshimiwa wabunge wanaotoa michango yenye mashiko na spika (au mwenyekiti) huwaruhusu waongee hadi mwisho (bila kuwazimia maiki) jambo linaloonesha uhai uliyopo ndani ya Bunge hilo la 13 tangu uhuru.

Screenshot_20260518_220833_Google.jpg
Screenshot_20260518_221138_Google.jpg
Screenshot_20260518_220526_Google.jpg
Screenshot_20260518_220625_Google.jpg
 
Mapampula toka lini wakawa na michango ya kueleweka?
 
Hivi kuna watanzania wanafuatilia bunge !.
 
View attachment 3590892View attachment 3590893View attachment 3590894View attachment 3590895
Bunge la kipumbavu!
 
Mashtaka yote dhidi yake yalithibitishwa lkn Mahakama ilifutilia mbali mashtaka dhidi yake kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha

Kutengeneza Satellite uplinks and down links ni rahisi sana

kambi ya upinzani itakuwa angalau angalau.

Hawa wagalatia wana chuki za kipumbavu sana,lengo kuu la mleta mada ni hiyo namba 2

Usiseme mkuu wa nchi sema mtu haramu anae jifanya ni rais

Tukishalikomboa hili Taifa, Jeshi la Polisi tutalifumua lote

Hii ni tofauti ya aliyesoma na asiye na elimu. Katoliki ni Intellectuals hawana vinyongo na wahuni

Wanajua hakuna kitu tutafanya

kizazi gani hicho kisichokuwa na hekima hata kwa watu wazima

Hata mimi siwaamini policcm. Ukiona wamefanya uchunguzi wa ishu ya mauaji au utekaji na kuwabaini wahusika, basi tambua fika hawajashiriki kwenye hayo matukio

Ahmed Mabukhut Shabiby (CCM-hoja zake zinalenga ufisadi, wizi).
2. Revocatus Chiponda 'Baba Levo' (CCM-hoja zake zinalenga ushauri).
3. Joseph Kasheku Musukuma (CCM-hoja zake zinalenga utendaji mbovu).
4. Kangi Alphaxard Lugola (CCM-hoja zake zinalenga ufisadi, wizi)
5. Ado Shaibu Ado (ACT- Wazalendo-hoja zake zinalenga ukosoaji).
6. Pascal Lucas Lutandula (CCM-hoja zake zinalenga mabadiliko).
7. Livingstone Joseph Lusinde (CCM-hoja zake zinaleng
Hamna kitu , wote takataka.
Kama mtu haja sukuma agenda from the cause root, kuwa bungeni huo wote ni ubatili.
Ado shahibu unaingia kwenye uchaguzi ambao hakuna Tume huru , lakini kwa vile unaona unaweza kupenya kwenye tundu la sindsno ya CCM ukapata mlo wako, then unakuja kudanyanya wajinga kusema sema ndani ya so called bunge unadhani wenye akili watakuthamini! NEVER!
 
Wabunge wanapenda kuongea ukweli ila vyama vinawabana sana ,ukitoa BOKO lazima utaletewa HEKAHEKA za kufukuzwa hivyo lazima "Huume" na kupuliza ,sasa wakianza kupuliza ndipo hapo wanapoboa.
 
Hapo hakuna Bunge! Bunge ni rubber stamp ya kupitisha miswada ya serikali isiyo na tija kwa wananchi.
Hao ni Waropokaji tu ambao mwisho wanaishia kupiga madawati na Kuunga mkono hoja.
 
Hamna kitu , wote takataka.
Kama mtu haja sukuma agenda from the cause root, kuwa bungeni huo wote ni ubatili.
Ado shahibu unaingia kwenye uchaguzi ambao hakuna Tume huru , lakini kwa vile unaona unaweza kupenya kwenye tundu la sindsno ya CCM ukapata mlo wako, then unakuja kudanyanya wajinga kusema sema ndani ya so called bunge unadhani wenye akili watakuthamini! NEVER!
Wenye akili ni wakina nani?

Amandla...
 
Back
Top Bottom