PostGE2025 Viongozi 10 wa Afrika waliowahi kufikishwa ICC

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
BBC.

1. Uhuru Kenyatta (Kenya)

Uhuru Kenyatta Rais mstaafu wa Kenya. Alifunguliwa mashitaka Machi 2011 kwa makosa matano ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Kenyatta alidaiwa "kulidhibiti kundi la Mungiki" na kulielekeza kufanya mauaji, uhamisho, ubakaji na aina nyingine za unyanyasaji wa kingono, mateso na vitendo vingine vya kinyama dhidi ya raia.

Mashtaka yote dhidi ya Kenyatta yalithibitishwa. Hata hivyo, kabla ya kesi kuanza, Mwendesha Mashtaka alitangaza kumuondolea bwana Kenyatta mashtaka yote.

2. Omar al‑Bashir (Sudan)

Alifunguliwa mashitaka tarehe 4 Machi 2009 kwa makosa matano ya uhalifu dhidi ya binadamu na makosa mawili ya uhalifu wa kivita kuhusiana na hali ya Darfur, Sudan.

Makosa matatu ya mauaji ya kimbari.

Alituhumiwa kutekeleza sera ya serikali iliyotumia vyombo vya dola (jeshi, polisi, usalama na vikosi vya Janjaweed) kushambulia vikundi vya Fur, Masalit, na Zaghawa ambavyo vilionekana kuasi.

Al-Bashir alituhumiwa kuamuru ubakaji, mauaji, kuangamizwa, uhamisho wa nguvu, na mateso ya raia, pamoja na uporaji wa vijiji na kambi nyingi.

Mahakama ilitoa hati mbili za kukamatwa kwa al-Bashir lakini hadi sasa hajakamatwa.

3. Jean-Pierre Bemba

Bemba alishtakiwa Mei 2008 kwa makosa mawili ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na makosa manne ya uhalifu wa kivita kuhusiana na hali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Bemba alishtakiwa kwa makosa ya jinai kwa vitendo vya ubakaji, utesaji, "ghadhabu dhidi ya utu", mauaji, na uporaji.

Bemba alidaiwa kuongoza vuguvugu la Movement for the Liberation of the Congo (MLC), kundi la waasi wa Kongo, kuingia CAR baada ya Rais wa Afrika ya Kati Ange-Félix Patassé kuomba msaada wa Bemba katika kukandamiza uasi ulioongozwa na François Bozizé.

Mahakama ilimkuta Bemba na hatia ya makosa yote matano. Mahakama ilimhukumu Bemba kifungo cha miaka 18 jela tarehe 21 Juni 2016.

Bemba alikata rufaa ya ICC. Hukumu hiyo ilibatilishwa na Jaji Christine Van den Wyngaert.

4. Bosco Ntaganda

Bosco Ntaganda alikuwa afisa wa tatu wa cheo cha juu zaidi katika Kikosi cha Patriotic for the Liberation of the Congo (FPLC).

Alishtakiwa Agosti 2006 kwa makosa matatu ya uhalifu wa kivita kuhusiana na hali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Machi 2013, Ntaganda alikimbilia Rwanda na kuingia Ubalozi wa Marekani mjini Kigali.

Aliomba Marekani kumwezesha kujisalimisha kwa Mahakama ya ICC, ICC ilimshikilia na kumhamishia The Hague. Mashtaka yote dhidi ya Ntaganda yalithibitishwa na mahakama ya awali ya kesi.

Ntaganda alipatikana na hatia kwa makosa yote ya Uhalifu dhidi ya ubinadamu na Uhalifu wa Kivita

5. William Ruto

William Ruto Rais wa sasa wa Kenya. Alishtakiwa Machi 2011 kwa makosa manne ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kuhusiana na hali katika Jamhuri ya Kenya.

Alidaiwa kuwaongoza watu wa kabila la Kalenjin kuendeleza ghasia kwa niaba ya chama cha Orange Democratic Movement (ODM), cha Raila Odinga, wakati na baada ya uchaguzi wa 2007.

Ruto alidaiwa kuhusika na mauaji, uhamisho, mateso ya raia katika miji ya Kapsabet, Nandi Hills, Turbo na eneo la Eldoret.

Mashtaka yote dhidi yake yalithibitishwa lkn Mahakama ilifutilia mbali mashtaka dhidi yake kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha.

6. Laurent Gbagbo

Laurent Gbagbo alishtakiwa 2011 kwa makosa manne ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kuhusiana na hali katika Jamhuri ya Côte d'Ivoire.

Akiwa Rais wa Côte d'Ivoire, Gbagbo alidaiwa kuandaa, pamoja na watu wa ndani, mashambulizi ya kimfumo dhidi ya raia wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi ulioanza tarehe 28 Novemba 2010.

Vikosi vya usalama vya taifa, Jeshi la Kitaifa, wanamgambo, na mamluki chini ya amri ya Gbagbo wanadaiwa kuwaua, kuwabaka, kuwatesa na kuwatendea kinyama raia ambao walichukuliwa kuwa wafuasi wa Alassane Ouattara, mpinzani wa Gbagbo katika uchaguzi wa rais wa 2010.

Gbagbo alikamatwa na vikosi vinavyomtii Ouattara katika makao ya rais. Mahakama ya awali ilithibitisha mashtaka yote dhidi yake.

Gbagbo aliachiliwa huru tarehe 15 Januari 2019.

7. Muammar Gaddafi

Muammar Gaddafi alishtakiwa tarehe 27 Juni 2011 kwa makosa mawili ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kuhusiana na hali ya Libya. Kama kiongozi na Kamanda wa Majeshi ya Libya alidaiwa kupanga, kwa kushirikiana na kundi lake la ndani la washauri, sera ya ukandamizaji mkali wa maasi ya wananchi.

Vikosi vya wanamgambo waliopangwa na serikali, polisi wa kitaifa, jeshi la Libya, Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi, na vyombo vingine vya usalama, vilivyo chini ya amri ya Gaddafi, vilidaiwa kuua mamia ya raia na kufanya "vitendo vya kinyama ambavyo viliwanyima haki raia.

Gaddafi aliuawa katika mji wa Sirte nchini Libya 2011 na Mahakama ikakatisha kesi dhidi yake tarehe 22 Novemba 2011.

8. Germain Katanga

Germain Katanga alifunguliwa mashitaka tarehe 2 Julai 2007 kwa makosa matatu ya uhalifu dhidi ya binadamu na makosa sita ya uhalifu wa kivita kuhusiana na hali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)

Alidaiwa kuamuru vikosi vyake kushambulia raia katika operesheni ya kijeshi iliyoratibiwa na Nationalist and Integrationist Front (FNI).

Mahakama ya ICC ilitoa hati ya kukamatwa alipatikana na hatia ya makosa manne ya uhalifu wa kivita na shtaka moja la uhalifu dhidi ya binadamu, alihukumiwa kifungo cha miaka 12. Alikata rufaa akapunguziwa kifungo cha miaka 12 hadi miaka 3 na miezi 8. Katanga alikamilisha kifungo chake tarehe 18 Januari 2016.

9. Joseph Kony

Joseph Kony alifunguliwa mashitaka Julai 2005 kwa makosa 12 ya uhalifu dhidi ya binadamu na makosa 21 ya uhalifu wa kivita kuhusiana na hali nchini Uganda.

Anadaiwa kuwa mwenyekiti na kamanda mkuu wa Lord's Resistance Army (LRA), kundi lenye silaha ambalo limekuwa likiendesha kampeni ya msituni tangu 1987 dhidi ya serikali ya Uganda.

Kony bado anasakwa lakini hajulikani aliko, ingawa anashukiwa kuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati au nchi jirani.

10. Thomas Lubanga

Thomas Lubanga Dyilo alishtakiwa Februari 2006 kwa makosa matatu ya uhalifu wa kivita kuhusiana na hali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Alidaiwa kuwa kiongozi mwanzilishi wa Union of Congolese Patriots (UCP), vuguvugu la waasi kaskazini mashariki mwa DRC, pamoja na kamanda mkuu mwanzilishi wa mrengo wa kijeshi wa UCP, Patriotic Force for the Liberation of the Congo (FPLC).

Lubanga anashutumiwa kwa kuwaandikisha watoto kwa FPLC na kuwatumia "kushiriki kikamilifu katika uhasama".

Kiongozi huyo wa waasi alikamatwa tarehe Machi 2005 na mamlaka ya Congo baada ya kudaiwa kuamuru kushambuliwa kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Julai 2012 alihukumiwa kifungo cha miaka 14 hadi leo bado anatumikia kifungo chake.
 
Huyo no 9 ina maana kajificha wapi asijulikane aliko? Sasa km ni nchi jirani au JAC mbna wanaweza kumsaka na kumpata kiwepesii.

Nweiiii mbona Case nyingi wahusika hawajapewa stahiki zao??
Mmmmh
 
Hata Mimi mwenyewe inatia shaka so huo umuhimu wa hiyo mahakama uko wapi Sasa !?
 
Kwa takwim hizo hapo juu maana yale ni kwamba ICC ni chombo cha kuwa petipeti waharifu na au kuwapunguzia hukumu au kuwaachia kabisa waharifu baada ya upepo kutulia. Ndio maana Samuya alisema waje wamchukue tu.. ataenda..kumbe utendaji kazi wa ICC anaufahamu
 
Huyo no 9 ina maana kajificha wapi asijulikane aliko? Sasa km ni nchi jirani au JAC mbna wanaweza kumsaka na kumpata kiwepesii.

Nweiiii mbona Case nyingi wahusika hawajapewa stahiki zao??
Mmmmh

Mahakama gani haina Jeshi, Haina polisi, Inategemea Polisi wa nchi nyingine wawakamatie waarifu wao.

Ni upumbavu tuu.
 
Huku kwetu matarajio yetu bwana huyu wa kwetu atanyongwa na hio mahakama!

Hii mahakama imekaa kimkakati , impact yake ni ndogo mno.

Na kamwe samia atamaliza maisha yake hapa duniani bila kusimama kwenye hio mahakama.
 
Kwa takwim hizo hapo juu maana yale ni kwamba ICC ni chombo cha kuwa petipeti waharifu na au kuwapunguzia hukumu au kuwaachia kabisa waharifu baada ya upepo kutulia. Ndio maana Samuya alisema waje wamchukue tu.. ataenda..kumbe utendaji kazi wa ICC anaufahamu
Inategemea na uhusika juzi waziri Mkuu wa Bangladesh kahukumiwa kunyongwa.
 
NIMEONA ORODHA NI YA WA AFRIKA TU.INAONEKANA NI MAHAKAMA YA KIHUNI TU.
 
Huyo no 9 ina maana kajificha wapi asijulikane aliko? Sasa km ni nchi jirani au JAC mbna wanaweza kumsaka na kumpata kiwepesii.

Nweiiii mbona Case nyingi wahusika hawajapewa stahiki zao??
Mmmmh
Haki haiko mahakamani.
Iwe Icc au hapa hapa Bongo, haki utaipata Kwa mtutu wa bunduki
 
Kitendo cha kuchunguzwa na kushtakiwa na kusimamishwa kizimbani kwa Samia itakuwa ushindi mkubwa kwa wapigania haki, ila mabadiliko ya kweli ni sisi wenyewe hakuna wa kutusaidia, migomo na maandamano ni silaha kubwa sana
 
Back
Top Bottom