Kuna tetesi kuwa baadhi ya wabunge wamejipanga kuwasilisha hoja bungeni ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson baada ya kuonekana wazi kushindwa kuuongoza mhimili huo kwa manufaa ya watanzania.
Hatua ya wabunge hao inakuja baada ya Spika kuzima ajenda za wananchi ambapo baadhi ya wabunge walitaka masuala hayo yajadiliwe bungeni yeye akayazuia yote.
(i) Hoja ya kujadili Ripoti ya CAG (Mhe. Ole Sendeka)
(ii) Hoja ya kujadili uvamizi wa tembo kwa wananchi( Mhe. Bahati)
(iii)Hoja ya tatizo la mbolea na kufutiwa leseni mawakala wa mbolea( Mhe. Msambatavangu)
(iv)Hoja ya ajira kutolewa kwa upendeleo (Mh. Mwita Waitara)