Tetesi: Wabunge kumpigia kura Spika wa Bunge kutokuwa na imani

siyo kweli na kujikwaa siyo kuanguka.

Hivi wewe hujawahi kukosea kitu huko kazini kwako? Muacheni jamani

Kweli mkuu, Mimi hukosea hapa ofisini, ila huwa najirekebisha. Sasa spika kapiga chini hoja ya mbolea, hoja ya ripoti ya CAG lakini akakubali hoja ya kumpongeza Rais Samiah. Wabunge wakapitisha azimio la kumpongeza Rais, ila kujadili mbolea inayowagusa wananchi kagoma. Wamtoe tu.
 
Huyo spika alizoea bunge lenye wapinzani, na akawa kazi yake ni kuwakomoa kwenye kila hoja yao. Matokeo yake tabia ile imegeuka kilema kwake, hivyo kila mwenye hoja kinzani na serekali kwake ni kumzuia tu. CCM vumilieni upuuzi mlioulea kugeuza bunge kuwa chombo cha kuikinga serekali, badala ya kuisimamia na kuiwajibisha.

Kweli kabisa mkuu.
 
Wabunge wa chama kipi? CCM hawa wa kupita bila kupingwa au wapi hao? Labda kama Kuna wabunge mamluki kutoka nje.
 
Kuna tetesi kuwa baadhi ya wabunge wamejipanga kuwasilisha hoja bungeni ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson baada ya kuonekana wazi kushindwa kuuongoza mhimili huo kwa manufaa ya watanzania.

Hatua ya wabunge hao inakuja baada ya Spika kuzima ajenda za wananchi ambapo baadhi ya wabunge walitaka masuala hayo yajadiliwe bungeni yeye akayazuia yote.

(i) Hoja ya kujadili Ripoti ya CAG (Mhe. Ole Sendeka)
(ii) Hoja ya kujadili uvamizi wa tembo kwa wananchi( Mhe. Bahati)
(iii)Hoja ya tatizo la mbolea na kufutiwa leseni mawakala wa mbolea( Mhe. Msambatavangu)
(iv)Hoja ya ajira kutolewa kwa upendeleo (Mh. Mwita Waitara)
Upo sawa, nadhani kuna kanuni anazisimamia Mhe.Spika. Kama kuna haja ya kujadiliwa masuala hayo ingebidi bunge libadili kanuni hizo zilizopo kwa sasa. Je, kama angeruhusu Wabunge wajadili suala hilo tofauti na kanuni zilizopo si ungesema Spika hafuati sheria/kanuni?

Hebu pitia kanuni na sheria zinasemaje kuhusu masuala ya ukaguzi wa CAG halafu uzilete humu tuzisome ili kupata uelewa.
 
Kuna tetesi kuwa baadhi ya wabunge wamejipanga kuwasilisha hoja bungeni ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson baada ya kuonekana wazi kushindwa kuuongoza mhimili huo kwa manufaa ya watanzania.

Hatua ya wabunge hao inakuja baada ya Spika kuzima ajenda za wananchi ambapo baadhi ya wabunge walitaka masuala hayo yajadiliwe bungeni yeye akayazuia yote.

(i) Hoja ya kujadili Ripoti ya CAG (Mhe. Ole Sendeka)
(ii) Hoja ya kujadili uvamizi wa tembo kwa wananchi( Mhe. Bahati)
(iii)Hoja ya tatizo la mbolea na kufutiwa leseni mawakala wa mbolea( Mhe. Msambatavangu)
(iv)Hoja ya ajira kutolewa kwa upendeleo (Mh. Mwita Waitara)
Bangi yenye mbegu Mbaya sana.
 
Huyo spika alizoea bunge lenye wapinzani, na akawa kazi yake ni kuwakomoa kwenye kila hoja yao. Matokeo yake tabia ile imegeuka kilema kwake, hivyo kila mwenye hoja kinzani na serekali kwake ni kumzuia tu. CCM vumilieni upuuzi mlioulea kugeuza bunge kuwa chombo cha kuikinga serekali, badala ya kuisimamia na kuiwajibisha.
Mchepuko wa bwana joni una stress (UH imefikia 150%) hasa baada ya joni kusepa. Spika wa bunge la chato hana uelekeo tena!
 
Back
Top Bottom