Wabunge wa CHADEMA wamekengeuka, wanajifanya hawaoni kazi nzuri ya uletaji maendeleo ndani ya miaka minne

Mmesahau miaka ile watu walikuwa wanazipiga na hakuna kulichokuwa kinafanyika?
Hata sasa zinapigwa na nyongeza ya kurushiwa maburungutu ya pesa barabarani. Ninaishi Dar tena mjini, hakuna serikali huku serikali iko kwenye barabara kuu tu kwani mitaa yetu haifanyiwi matengenezo yoyote toka Uhuru huku kodi tunalipa na hatuna tofauti na vijijini.
 
Dar kubwa, usigeneralise sababu kuna sehemu miradi ya Dmdp imefanyika na kuna mabaliko makubwa. Kama unakaa kimara golani pole!
 
Kwa hiyo figure ya usd 7.5 bil ilipelekwa bungeni kama fungu la bajeti? Na kwanini kama zilipitishwa na bunge mradi haukuanza?
Kwani CAG anakagua mradi wa Sgr wakati kuna Consultant? Au anakagua matumizi ya pesa za wizara ya ujenzi uchukuzi na masaliano?
 

Mradi ulipelekwa bungeni kujadiliwa kama ilivyo miradi mingine, mradi ulijadiliwa na bunge ili kupata uhalali wa kuanza. Ukajadiliwa na kupitishwa, ikawa iko kwenye hatua ya utekelezaji huku JK akiwa muda wake wa kukaa ofisini umeisha. Alipoingia Magufuli tu akausimamisha. Mkopo wa ujenzi ulikuwa bado haujatoka hivyo bunge lisingeweza kujadili hela ambayo haijatoka na mradi bado kuanza.

CAG hakagui mradi, bali anakagua matumizi ya fedha za umma. Hata huo mradi wa SGR unajengwa kwa fedha za umma, hivyo CAG kisheria anapaswa kukagua.
 
K
Kwa hiyo bunge lilipitisha Usd 7.5 bil zitumike? Na kama lilipitisha kwa uhalali ilikuwaje sasa haukutekekezwa?
 
K

Kwa hiyo bunge lilipitisha Usd 7.5 bil zitumike? Na kama lilipitisha kwa uhalali ilikuwaje sasa haukutekekezwa?
Hayo unayoyasema ni uongo mtupu. Mradi wa Sgr umeanza kutekelezwa wakati wa awamu ya tano na ni bajeti ya 2016-2017 ndio ulijadiliwa. Na kuna kampuni moja ya china iliomba tenda ila ikawa na utata. Ndipo Yapi merkez na Mota Engil walipata tenda. Exim china walifanya mazungumzo na serikali juu ya kutoa mkopo kama hiyo kampuni ya china ingepata tenda.
Ila kwa sababu huna nondo na ni mbulula wa kukariri ndio maana unakurupuka.
 
Hii awamu ni sawa tu na timu wanapiga tachi nyingi mwisho wanafungwa wao kila mechi halafu bado wanalazimisha mashabiki wawasifu. Very hopeless.
 
K

Kwa hiyo bunge lilipitisha Usd 7.5 bil zitumike? Na kama lilipitisha kwa uhalali ilikuwaje sasa haukutekekezwa?

Rais atataka kitu nchi hii bunge liache kupitisha? Haukutekelezwa kwakuwa rais aliyekuwa amesimamia hilo alitoka madarakani. Rais aliyefuata alikuja na mitazamo yake. Ndio maana huwa tunasema nchi hii haina bunge, bali lina wala pesa za wananchi kisheria huko kwenye jengo la bunge.
 
Naona umekuwa msemaji wa wabunge wa Chadema,,we waache watajua Cha kusema. Ukifanya mazuri husingoje kusifiwa na ukiona mtu anahesabu mambo mazuri aliyoyafanya Basi hujue ni mpenda sifa.Hacha mazuri yenyewe yaongee 🏃🏃
 
Hopeless, alafu eti ndio unajifanya una nondo za kutosha.
Sababu hata ile habari ya Tanzania kupata mkopo toka Exim bank China wa usd 7.6 bil kwa ajili ya Sgr ni mwaka 2016 mwezi wa sita sasa huo uongo wako uongo wako ndio unauconnect na hiyo habari. Mmetepeta sana hamna hoja ya kumkamata JPM.
 
Naona umekuwa msemaji wa wabunge wa Chadema,,we waache watajua Cha kusema. Ukifanya mazuri husingoje kusifiwa na ukiona mtu anahesabu mambo mazuri aliyoyafanya Basi hujue ni mpenda sifa.Hacha mazuri yenyewe yaongee 🏃🏃
Kama labda hivyo vituo vya afya vingekuwa havijajengwa hawa jamaa unawajua? Kama kungekuwa na ubadhirifu Tamisemi unawajua hawa?
 

Nakuambia hivi ulianza kujua mambo ya siasa mwaka 2015 na ndio hapo ukajiunga jf. Huna unalojua nje ya hapo zaidi ya kupiga siasa mfu huku jukwaani.
 
Nakuambia hivi ulianza kujua mambo ya siasa mwaka 2015 na ndio hapo ukajiunga jf. Huna unalojua nje ya hapo zaidi ya kupiga siasa mfu huku jukwaani.
Kujiunga Jf hakuna unusiano na kujua mambo. Wewe ni muongo na unakarishwa mambo. Kuna watu wamejiunga Jf jana au juzi wanakupita wewe kujua mambo mengi tu.
Unalazimisha uongo uwe ukweli. Yaani Usd bil 7.5 zijenge Sgr toka Dar mpaka Mwanza? Kilometa 1400+! Alafu unataka kutumia hii hoja kuonyesha JPM hafai? Bado unatetea wabunge wa Chadema kubeza kazi nzuri anayoifanya JPM na chama chake CCM. Na unashindwa kuelewa kabisa kurekebisha miundo mbinu ya reli na kujenga Sgr ni jambo ambalo liliwekwa kwenye ilani ya Chama cha Ccm ya 2020-2015. Sio suala la mtu mmoja kujiamulia.
 
Maendeleo yapi unayozungumzia kwa miaka 59?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiwe ataiacha nchi pabaya kuliko hata Nyerere
 
Dar kubwa, usigeneralise sababu kuna sehemu miradi ya Dmdp imefanyika na kuna mabaliko makubwa. Kama unakaa kimara golani pole!
DMDP ni miradi ya nani? Nijuavyo ni pesa toka nje siyo kodi zetu, zinasimamiwa na wanaozileta. Ninataka unipe kinachotekelezwa kwa kodi zetu. Mvua kidogo ikinyesha barabara zetu huongezeka urefu kwani zinakua zigzag toka nusu kilomita kuwa robotatu ya kilomita! Maeneo mengi barabara zimegeuka makorongo na kutishia nyumba kubomoka, baadhi ya nyumba zimefukiwa na udongo unaomomonyoka barabarani kiasi nyingine milango ya mbele imefungwa na nyingine unaweza ukakaa juu ya paa kwa jinsi zilivyozama. Mwisho mbaya zaidi ni wananchi wengi kuhamia kwenye maombi ya manabii baada ya kushindwa gharama za hospitali, kwanini ulipe kumuona dakitari wakati hulipi kumuona hakimu.
 

Ninapokuambua umejua siasa mwaka 2015, kisha ndio ukaamua ujiunge jf sijakosea. Hiyo $7.5b kwa rate ya wakati huo 2,200 ni sawa 15t tshs. Huenda nikiisema hiyo figure kwa fedha za kitanzania unaweza kujua mamaanisha nini. Nchi hii haijawahi kuwa na mradi mmoja wa 10t+ toka tupate uhuru. Kama unaona hiyo 15t ya wakati huo ilikuwa ni ndogo, basi unamaanisha Magufuli atajenga hiyo reli kwa zaidi ya 15t hizo km 1,450. Sasa kama atajenga km hizo kwa zaidi ya 15t, atakuwa ameokoa nini?

Halafu naona naona ni kama mjadala umekuwa mrefu mpaka umekata pumzi. Kwani ubora wa Magufuli unapatikana kwa ujenzi wa hiyo reli? Na hata kama ni ujenzi wa hiyo reli kwani ameikamilisha kama lengo lilivyo? Kumbuka ana mradi mwingine wa umeme wa 7t, na kote huko asilimia kubwa ni pesa za mkopo. Ni wapi anaweza kukopeshwa zaidi ya 10 ndani ya hiyo miaka yake mitano iliyosalia madarakani iwapo atashinda?

Hilo unalong'ang'ania kuwa wabunge wa cdm wamebeza kazi nzuri za Magufuli, nimekuambia sema wamesema nini unaleta porojo tu. Hilo bunge limejaa wanaccm na wanasifia chochote cha serikali, je hutosheki na hao mpaka wabunge wa cdm nao wasifie?
 
I Inakopa China sembuse Tz. Kwani hao waliobeza hujasikia walichosema? Wanasema ni kama kazi ndogo ati sababu kuna kata nyingi Tz. Sasa hiyo ni akili au matope. Tangu tupate uhuru kulikuwa na vituo vingapi vya afya kabla ya 2015?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…