Wabunge wa Kagera wapinga Mkoa wao kumegwa na kupelekwa Chato

Wabunge wa Mkoa wa Kagera, Wamepinga kitendo cha kuendelea kuumega Mkoa wa Kagera. Hii imekuja baada ya Kuanzishwa Mchakato wa kufanya Wilaya ya Chato iliyopo Geita kuwa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule, alisema Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Geita (RCC) ilipendekeza wilaya tano, Chato na Bukombe mkoani Geita. Biharamulo na Ngara mkoani Kagera na sehemu ya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma zichukuliwe kwa ajili ya kuanzisha Mkoa mpya wa Chato.

Kwa mujibu wa takwimu za sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Chato ilihesabiwa kuwa 365,127. Chato ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya Wilaya ya Biharamulo, Mkoa wa Kagera, mwaka 2012 ikasogezwa katika mkoa mpya wa Geita.

Pia soma:

1). Madiwani Buchosa wakubali kuhamia Geita ili kutoa fursa kuanzishwa mkoa mpya wa Chato

2). Kuunda Mkoa wa Chato ni kupoteza historia ya Wahaya, Mkoa wa Chato hauna maslahi kwa urithi wa utamaduni wa Mtanzania

3). Prof. Tibaijuka: Chato haina sifa kuwa Mkoa

4). Kwanini Chato iwe Mkoa kutoka kwenye Mkoa mchanga wa Geita ulioundwa 2012?

5). Geita yakubali kuundwa Mkoa wa Chato; Kakonko, Biharamulo na Ngara kumegwa. Sengerema kwenda Geita..

6). Geita: Baraza la Madiwani laukataa Mkoa mpya wa Chato

7)). Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

8). Rais Samia anaweza kuanzisha mkoa mpya wa Chato endapo haya yatazingatiwa…

HOJA YA WABUNGE KUPINGA KUMEGA MKOA WA KAGERA.

1. UTANGULIZI
Sisi wabunge wa Mkoa wa Kagera kupitia Wilaya ya Muleba na Wilaya ya Bukoba Vijiiini, Mhe Charles John Mwijage wa Jimbo la Muleba Kasikazini, Mhe. Dkt, Oscar Ishengoma Kikoyo wa Jimbo Ia Muleba Kusini, na Mhe. Dkt. Jasson Samson Rweikiza tumepokea wito wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera cha tarehe 29/10/2021 tukiwa tayari tumerudi Dodoma kwa ajili ya vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge. barua za wito wa Kikao, zimeambatishwa na agenda za RCC. Agenda namba 4 ya kikao tajwa inahusu mapendekezo ya Wilaya za Biharamulo na Ngara kupelekwa mkoa pendekezwa wa Chato. Hoja ya kuumeumega mkoa wa Kagera, inatualika kujadili faida na hasara zake kwa mkoa wa Kagera kwa kuzingatia masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumu. Tukiongozwa na uzalendo wetu kwa mkoa wa Kagera na utaifa wetu kwa taifa letu, kwa hali yoyote ile, pendekezo la kumega mkoa wa Kagera lina athari kubwa sana kuliko faida kwa usitawi wa Mkoa wa Kagera kihistoria, kijamii, kisiasa na kiuchumi. Kwa sababu hizo, na nyingine zitakazo tolewa hapa chini, hatukubaliani na hoja ya kuumega mkoa wa Kagera.

2. CHIMBUKO LA MKOA MPYA WA CHATO
Chimbuko la kuomba mkoa wa chato halina mashiko kisiasa, kiuchumi wala kisheria. Chimbuko la mkoa wa chato linatokana na muombolezaji mmoja aitwaye Bigambo wakati wa msiba wa Hayati Magufuli. Mwombolezaji huyo alidai kusikia Hayati Magufuli akitaka Chato uwe mkoa jambo ambalo halina uthibitisho wowote kisiasa. Vigezo vya kuunda mkoa mpya hutokana na mkoa mama kutokana na ukubwa wake na/au jiografia yake kuomba kumegwa i1i kusogeza huduma kwa watu wake. Kwa ombi hili ni tofauti sana, Wilaya ndogo na changa ya Chato iliyoanzishwa mwaka 2005 inaornba kuwa mkoa ili maeneo mengine yamegwe kuisadia kutimiza adhima yake ya kuwa mkoa jambo ambalo ni kinyume na dhana na falsafa ya uundwaji wa mikoa katika historia ya taifa hili lililoasisiwa na viongozi wetu mahiri. Geita mkoa mama, nao ni mchanga ulioanzishwa mwezi Machi mwaka 2012 ukimegwa kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Kagera. Pamoja na uchanga wake, Geita ni moja ya mikoa midogo ikiwa na kilomita za rnraba 20,054. Ukichukua ukubwa wa rniina wa Geita (20,054Km2) na Kagera (35,686Km2) kwa pamoja haifikii ukubwa wa Mkoa wa Tabora wenye ukubwa wa kilomita za mraba 76,150 au Morogoro wenye ukubwa wa kilomita za mraba 70,624. Ipo mikoa mikubwa na mikongwe iliyostahili kuleta ornbi kama hili, slyo wilaya ya Chato wala mkoa wa Geita. Kwa ukumbwa wa mkoa wa Kagera na/au Geita kuenendelea kuumega, mikoa ya Kagera na Geita itakuwa mkoa mdogo sana.

3. FAIDA
Kwa tathmini za kiuchumi, kijamii na kisiasa na kwa kuangalia jiografia ya mkoa wa Kagera kwa sasa na wilaya zinazolengwa kupelekwa hakuna faida yoyote kwa mkoa wa Kagera inayoweza kushawishi wananchi wa Mkoa wa Kagera kuridhia whlya za Biharamulo na Ngara kupelekwa mkoa pendekezwa.

4. ATHARI
Kwa kutumia vigezo vilivyotajwa hapo juu, athari kwa mkoa wa Kagera bila wilaya zake hizo mbili na kwa taifa zima la Tanzania ni kubwa sana.

4.1 KIJAMII:
(i) Mkoa wa Kagera ni muunganiko na mshikamano wilaya sabwa (7) za utawata zenye halmashauri nane. Pamoja na kuwa na wananchi wanaoweza kuhesabika kuwa makabila yanayojionyesha manne na koo nyingi sana, mapito ya mkoa huu katika historia ya kuwepo kwake yanaufanya mkoa huu kuwa jamii iliyoshikamana na imara kijamii, kisiasa na kiuchurni. Mkoa wa Kagera kwa kupakana na kuwa karibu na nchi nyingi umekuwa ukifikiwa na wageni wengi wa aina mbali mbali lakini wakati wote wana-Kagera walijiona wamoja na katika umoja huo wameweza kuhimiti matokeo yote hasi yaliyoletwa na wageni hao.

(ii) Kwa kuomba kuondoa wilaya za Ngara na Biharamulo kutasababisha mgawanyiko katika jamii na kufufua tofauti za kikabila na kikanda na koo zilizokwisha zikwa kwa
siku nyingi za uhai wa mkoa huu. Pamoja na sababu nyingine, hii inatokana na ukweli kuwa wananchi wa Wilaya tano zinazobaki hawakukubaliana na hawatafurahia wilaya za Biharamulo na Nsciwa kumegwa.

(iii) Kwa taifa kuna athari kubwa za kijamii, kisiasa na kiusalama kwani mpangilio wa Wilaya tatu (3) zinazopendekezwa kuunda mkoa pendekezwa, zinawingi wa watu wenye nasaba na ushawishi wa mataifa ya jirani ambayo hayajatulia kiusalama. Mshikamano wa mkoa wa Kagera uliojengeka kwa muda mrefu uliweza kudhibiti na kumaliza nguvu athari hiyo.

4.2 KIJIOGRAFIA:
(i) Kuondoa wilaya za Biharamulo na Ngara kuna itenga Kagera inayobaki na kuinyima nafasi ya "location advantage" ya mipaka ya Kabanga na Rusumo. Ustawi wa Mkoa wa Ziwa Magharibi u;itokana na hiyo "location advantage". Katika zama hizi ambazo biashara kati ya mkoa wa Kagera na nchi jirani unaendetea kukua na kuimarika, kuzimega wilaya hizo kutaunyima mkoa wa Kagera fursa hizo za kibiashara.

(ii) Mgawanyo au kumegwa huku kunapunguza eneo la mkoa wa Kagera. Mkoa wa Kagera una ukubwa wa eneo la mraba 35,686 (KM2 35,686) ikijumuisha nchi kavu na eneo la maji ya ziwa victoria. Eneo la maji ni kilomita za mraba 10,173 na eneo la nchi kavu ni kilomita za mraba 25,513. Wilaya ya Biharamulo na Ngara ambazo ni maeneo ya nchi kavu ni kilomita za mraba 9,371. Hivyo, kumega wilaya hizo mbili, Mkoa wa Kagera utakuwa umebaki na kilomita za mraba 16,142 zinazofaa kwa kilimo utalii. ikumbukwe, Kagera si mkoa
unaotawaliwa na shughuli za huduma (Service industry) hali ambayo eneo dogo linaweza kuwa na watu wengi na shughuli nyingi za kiuchunii zinazohalalisha uwepo wa eneo la kiutawala kiasi cha mkoa. Huu ni mkoa wa wakulima, wafugaji na wavuvi hivyo kupunguza eneo Iake ni kuudhohofisha kijamii, kihistoria na kiuchumi.

(iii) Katika uhai wa mkoa huu na hasa rniaka 15 mpaka leo tumepigana sana kuwa karibu k\Ara kujenga miundombinu ya barabara. Kwa kazi inayoendelea kwenye ujenzi wa barabara mzunguko wa ndani kwa ndani kwenye mkoa itakuwa si tatizo. Kimsingi suluhisho si kumega wilaya bali kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara, reli, afya, na uchumi.

4.3 KISIASA:
(i) Kagera bila Ngara na Biharamulo kisiasa siyo Kagera tunayoiona leo. Kufikia hatua hii ya kuwa na jamii tulivu na inayoelewana yenye mshikamano na mtazamo wa kimaendeleo haikuwa kazi rahisi, Wapo watu walihangaika kwa adhi na nyadhifa mbali mbali nao kwa kutambua mchango wao kwa Kagera si busara kuumega kila uchao.

(ii) Siasa ya Kagera ni zaidi ya mtazamo wa chama cha siasa na chama au vyama vingine. Tunazungumuza siasa kama hali au mtazamo wa jamii iliyoshuhudia na kuhimili kuanguka kwa uchumi baada ya kuvunjwa Chama cha Ushirika (BCU), Kuanguka kwa bei ya kahawa, jamii iliy()!itangulia taifa katika Vita dhidi ya Nduli ldd Amin Dada, jamii iliyopokea wimbi la wakimbizi toka nchi jirani, lakini pia jamii ambayo ilikuwa ya kwanza kupigwa na janga hatari la ukimwi. Pia jamii hii iliyokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi lililoaribu miundombinu na mali za watu, jamii ambayo wajasiliamali wake wengi na raia wengine walizama kwenye Mv Bukoba, ugonjwa wa Mnyauko wa r-nigomba kwa kutaja baadhi tu. Kimsingi, tafakari ya mapigo haya yaliyopata Kagera, Serikali inapaswa kuja na Mpango Maalum wa Kuikarabati Kagera (Special Economic Rehabilitation Program) ili ipone kwa ujumla wake na si kuumega vipande vipande kama inavyokusudiwa.

(iii) Athari nyingine kisiasa ni kufanya n-)aamuzi ya kumega mkoa kwa kufuata kilio cha mwombolezaji wa mkoa mwingine Bwana Bigambo alikuwa anaomboleza kama watanzania wote walivyoumia na kila mtu kusema lake kabla ya kutulizwa

View attachment 1997936View attachment 1997937View attachment 1997938View attachment 1997939View attachment 1997940View attachment 1997941
1
Upuuzi tu uliojaa wivu mikoa inagawanywa na kuongezeka kwa lengo la kusogeza na kuharakisha huduma kwa wananchi, wao ni akina nani na kwani nini wapinge, Kagera haina uspecial wowote, ilimegwa Mwanza, Arusha, Shinyanga, Mbeya, Rukwa, Iringa wao ni nani hadi wapinga huu mwendelezo wa kugawa mikoa?

Upopoma wa kindezi kabisa roho ya uchoyo, ubinafsi na kupenda kujiona bora itawaua pumbavu kbsa na mashavu yenu ya senene.

Wapende wasipende Mkoa wa Chato ushaiva kwenye hili Rais Ndugu Madam Hassan asifanye utani na ulegevu wa kuwasikiliza hawa wahaya uchwara.

Ni upumbavu kuwapa fursa ya fitina watu wenye choyo, ubinafsi, wivu kithiri usio na tija na wenye ubaguzi hasa kutopenda kuchangamana na wengine.
 
Chato ya nn wakati magu hayupo

Chato ina miradi ya kitaifa. Isipofanywa mkoa hiyo miradi itakuwa magofu.
So hakuna namna zaidi ya kupafanya mkoa ili miradi iendelee kuwa hai.
Mkoa wa Rubondo kitawekwa kituo kikubwa cha kusafisha mafuta ya Uganda..kwa ajili ya kuuza kanda ya ziwa,burundi,Congo na Rwanda
 
Wabunge wa kagera ni wanafiki na vilaza..eti ikimegwa ukubwa wa eneo utawapungukia..kwani kagera ni nchi..na ikimegwa hicho kipande kitaenda Burundi?mnataka eneo kubwa ambalo limejaa umasikini wa kutupa..anzeni kwanza kutengeneza stendi ya bukoba ambayo imewashinda ndio mnje kuleta hili pingamizi..jinga nyinyi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mka wa Ziwa Magharibi (uliopewa jina la Kager kwa heshima ya ushindi wa vita vya nduli) umekaa vizuri hapo ulipo. Kwa sababu za kiuchumi (access, critical mass, economic viability) ungebaki kama ulivyo. Sababu za kikabila hazina mshiko, sababu aliyetoa pendekezo Bigambo na Mhaya. Isitoshe, Ngara si nchi ya Wahaya ni ya Wahangaza na Biharamulo ni pori mostly la wafugaji Wasukuma. Pia naona Mbunge wa Ngara na wa Biharamulo hawajashiriki. Ukabila na mila etc etc etc hazina mshiko, sababu za kiuchumi ni muhimu zaidi. Kabila has never been a serious issue in Kagera or anywhere else in Tanzania: vimebaki vijembe vya Wahaya na Wanyambo; Baziba na Wakara; alizokuwa nazisema Nyerere kupinga ukabila.
Kwenye hili ujuaji wa kihaya ni wa kioopoma kabisa, hawa washenzi wameshiriki vikao vya kugawa mikoa mingine yote pumbavu zao wao wawe kama nani kupinga hoja walizotolea maamuzi nabkushadadia kwenye kugawa mikoa mikoa mingine.

Hawa wakidekezwa kuwapa nafasi ya malumbano ni utopolo wa akili

Maudhui na dhamira iko wazi mikoa inagawanywa kukidhi haja ya huduma za kimaendeleo serikali isifanye ubaguzi wa kuwafanya wahaya special.

Mkoa wa Chato upatikane kwa haraka kwanza Kagera iko kiutopolo sana kimaendeleo imagine hata internal migration ya watz kutoka sehemu zingine kwenda kutafuta riziki kagera ni close na zero.
 
Cha ajabu hao ni wabunge wa muleba, bukoba vijijini tu... Sio wabunge wote.

Mimi sijaona point ya msingi zaidi ya ubinafsi ya kuzikatalia biharamulo na ngara kutoka kagera ambazo zina umaskini wa kutisha...

Wabunge wa ngara na biharamulo wao wanasemaje
Hoja kubwa wanasema hizo wilaya zinazotakiwa kumegwa, pamoja na Chato, wakazi wake wengi ni warundi, kiusalama, ina hatari.

Wakimbizi wa Burundi walifanikiwa kutoa Rais wa Tanzania!!
 
Ila wahaya ni kiburi, nyie....

Nimesoma maneno machache sana hasa hapo kwenye CHIMBUKO LA MKOA MPYA WA CHATO na naomba kunukuu:-

"Chimbuko la kuomba mkoa mpya wa Chato halina mashiko kisiasa, kiuchumi wala kisheria"

Naendelea kunukuu....

"Chimbuko la mkoa wa Chato linatokana na muombolezaji mmoja aitwaye Bigambo wakati wa msiba wa hayati Magufuli."

"Muombolezaji huyo alidai kusikia kwamba Magufuli alitaka Chato uwe mkoa, jambo ambalo halina uthibitisho wowote wa kisiasa"

Mwisho wa kunukuu.

My take:
Yaani hawa jamaa (Wahaya) "wameikataa" kabisa Chato na wakafika mbali zaidi kwa kusema "zilikua ni hasira tu" za kufiwa (za msiba) za bwana Bigambo.
Lakini pia wametanabaisha kwamba alichokisikia bwana Bigambo hakina uthibitisho wowote, kwahiyo huenda Bigambo alikua "anatujaza tu".
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cha ajabu hao ni wabunge wa muleba, bukoba vijijini tu... Sio wabunge wote.

Mimi sijaona point ya msingi zaidi ya ubinafsi ya kuzikatalia biharamulo na ngara kutoka kagera ambazo zina umaskini wa kutisha...

Wabunge wa ngara na biharamulo wao wanasemaje
Mimi sio wa kagera ila kugawa mkoa kwa Nia ya ubinafsi wa kiongozi mmoja ni hasara how about history ya mkoa wa kagera, hao wabunge wa ngara acha wasaidiwe kama wamelala kutetea mkoa mzima wa Kagera, hafu why chato wakati Kuna mikoa mingi mikubwa kuliko Geita na hawajapeleka hyo kugawa.
Umaskini nchi hii utaisha kwa serikali kupeleka maendeleo Hadi ngazi ya chini kabisa na sio kuongeza mikoa na wilaya ambazo zitaongeza cost of administration.
 
Naunga mkono hoja ya wilaya ya Ngara na Biharamulo Kumegwa Kwenda Mkoa Mpya Wa Chato,kwasababu Kutoka Ngara Kwenda Bukoba Kufuata Huduma Ni Umbali Mrefu Sana Pia Kuanzia Mila na desturi hata lugha ni tofauti kabisa.Ni jambo jema kuwaachia WAHAYA na Kagera yao
Vipi mkoa wa Tabora na wenyewe umegwe pia why chato?
 
Mkoa kumegwa si tatizo kubwa bali hoja ni kuwa kuanzishwa kwa mkoa kunamnufaishaje mwananchi wa kawaida.
Ni wananchi wangapi wanaohitaji huduma za kimkoa.

Wananchi wengi tunahitaji kurahisishwa/kuboreshwa kwa huduma za vitongoji, vijiji na kata.
Nakumbuka miaka ya karibuni kuna baadhi ya vitongoji viliungwa vikaongezwa ukubwa.

Tusaidieni kupunguza ukubwa wa maeneo yaliyo jirani yetu.
Wapeni posho, vyombo vya usafiri, vifaa vya kazi nk viongozi wa chini ili wawahiudumie wananchi kwenye vitongoji, vijiji na kata zao.

Kuanzisha mkoa kuna gharama kubwa mno ikiwamo majengo, magari, mishahara na mengineyo.
Kuboresha maeneo ya chini kutaharakisha maendeleo.

Naamini hitaji la wananchi si Wilaya wala mkoa mpya.
Tuleteeni wataalam wa kilimo, afya, elimu, maendeleo na ustawi wa jamii, mifugo nk huku chini.

Mungu ibariki Tanzania.

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Mega projects za wakati huo zilizojengwa Kwa nguvu ya mkoa zilibaki kunufaisha wahaya mfano mmojawapo ni shule. Ni kweli wahaya na wahangaza wano mwingiliano wa muda mtefu japo kuna comparative disadvantage inayojitikeza kutokana na makao makuu kuwa Kwa mhaya. Serikali ikifanya haya inayotarajia kuyafanya iwe ni Kwa lengo la ku boost hizi wilaya zilizotopea kwa imaskini japo ngara itajikomboa soon kutokana na nickel na madini mengine kadhaa .
 
Nimegundua kumbe wabunge wa kagera ndo wanazidi kupafanya kagera kuwa maskini...

Wanamawazo mgando na wako conservative.

Mimi naomba biharamulo na ngara ziundiwe mkoa wake ili ziangaliwe zaidi maana ndo maskini zaidi katika mkoa wa kagera.

Poor you wabunge
[emoji23][emoji23][emoji23] tunajua lengo lako mkuu

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Ila wahaya ni kiburi, nyie....

Nimesoma maneno machache sana hasa hapo kwenye CHIMBUKO LA MKOA MPYA WA CHATO na naomba kunukuu:-

"Chimbuko la kuomba mkoa mpya wa Chato halina mashiko kisiasa, kiuchumi wala kisheria"

Naendelea kunukuu....

"Chimbuko la mkoa wa Chato linatokana na muombolezaji mmoja aitwaye Bigambo wakati wa msiba wa hayati Magufuli."

"Muombolezaji huyo alidai kusikia kwamba Magufuli alitaka Chato uwe mkoa, jambo ambalo halina uthibitisho wowote wa kisiasa"

Mwisho wa kunukuu.

My take:
Yaani hawa jamaa (Wahaya) "wameikataa" kabisa Chato na wakafika mbali zaidi kwa kusema "zilikua ni hasira tu" za kufiwa (za msiba) za bwana Bigambo.
Lakini pia wametanabaisha kwamba alichokisikia bwana Bigambo hakina uthibitisho wowote, kwahiyo huenda Bigambo alikua "anatujaza tu".
Ila kuna mikoa NI mikubwa sana
 
Wana kagera msikubali mnaamishwa chato, huko ni kuharibu historia ya mkoa wenu ilianza kumegwa biharamulo na sasa ngara, kisa interest za kiongozi mubinfasi.

Lakini ki uhalisia ukiangalia umbali uliopo kutoka Ngara hadi Bukoba ni 280Kms,Wilaya ya Ngara ni kama imetengwa kabisa Ki Mkoa.Binafsi ni sahihi Ngara kuletwa Chato kwa maana ya huduma za Ki Mkoa.Pengine kinachogomba hapa nj jina Chato kuitwa Mkoa.
 
Wabunge wa Mkoa wa Kagera, Wamepinga kitendo cha kuendelea kuumega Mkoa wa Kagera. Hii imekuja baada ya Kuanzishwa Mchakato wa kufanya Wilaya ya Chato iliyopo Geita kuwa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule, alisema Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Geita (RCC) ilipendekeza wilaya tano, Chato na Bukombe mkoani Geita. Biharamulo na Ngara mkoani Kagera na sehemu ya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma zichukuliwe kwa ajili ya kuanzisha Mkoa mpya wa Chato.

Kwa mujibu wa takwimu za sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Chato ilihesabiwa kuwa 365,127. Chato ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya Wilaya ya Biharamulo, Mkoa wa Kagera, mwaka 2012 ikasogezwa katika mkoa mpya wa Geita.

Pia soma:

1). Madiwani Buchosa wakubali kuhamia Geita ili kutoa fursa kuanzishwa mkoa mpya wa Chato

2). Kuunda Mkoa wa Chato ni kupoteza historia ya Wahaya, Mkoa wa Chato hauna maslahi kwa urithi wa utamaduni wa Mtanzania

3). Prof. Tibaijuka: Chato haina sifa kuwa Mkoa

4). Kwanini Chato iwe Mkoa kutoka kwenye Mkoa mchanga wa Geita ulioundwa 2012?

5). Geita yakubali kuundwa Mkoa wa Chato; Kakonko, Biharamulo na Ngara kumegwa. Sengerema kwenda Geita..

6). Geita: Baraza la Madiwani laukataa Mkoa mpya wa Chato

7)). Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

8). Rais Samia anaweza kuanzisha mkoa mpya wa Chato endapo haya yatazingatiwa…

HOJA YA WABUNGE KUPINGA KUMEGA MKOA WA KAGERA.

1. UTANGULIZI
Sisi wabunge wa Mkoa wa Kagera kupitia Wilaya ya Muleba na Wilaya ya Bukoba Vijiiini, Mhe Charles John Mwijage wa Jimbo la Muleba Kasikazini, Mhe. Dkt, Oscar Ishengoma Kikoyo wa Jimbo Ia Muleba Kusini, na Mhe. Dkt. Jasson Samson Rweikiza tumepokea wito wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera cha tarehe 29/10/2021 tukiwa tayari tumerudi Dodoma kwa ajili ya vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge. barua za wito wa Kikao, zimeambatishwa na agenda za RCC. Agenda namba 4 ya kikao tajwa inahusu mapendekezo ya Wilaya za Biharamulo na Ngara kupelekwa mkoa pendekezwa wa Chato. Hoja ya kuumeumega mkoa wa Kagera, inatualika kujadili faida na hasara zake kwa mkoa wa Kagera kwa kuzingatia masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumu. Tukiongozwa na uzalendo wetu kwa mkoa wa Kagera na utaifa wetu kwa taifa letu, kwa hali yoyote ile, pendekezo la kumega mkoa wa Kagera lina athari kubwa sana kuliko faida kwa usitawi wa Mkoa wa Kagera kihistoria, kijamii, kisiasa na kiuchumi. Kwa sababu hizo, na nyingine zitakazo tolewa hapa chini, hatukubaliani na hoja ya kuumega mkoa wa Kagera.

2. CHIMBUKO LA MKOA MPYA WA CHATO
Chimbuko la kuomba mkoa wa chato halina mashiko kisiasa, kiuchumi wala kisheria. Chimbuko la mkoa wa chato linatokana na muombolezaji mmoja aitwaye Bigambo wakati wa msiba wa Hayati Magufuli. Mwombolezaji huyo alidai kusikia Hayati Magufuli akitaka Chato uwe mkoa jambo ambalo halina uthibitisho wowote kisiasa. Vigezo vya kuunda mkoa mpya hutokana na mkoa mama kutokana na ukubwa wake na/au jiografia yake kuomba kumegwa i1i kusogeza huduma kwa watu wake. Kwa ombi hili ni tofauti sana, Wilaya ndogo na changa ya Chato iliyoanzishwa mwaka 2005 inaornba kuwa mkoa ili maeneo mengine yamegwe kuisadia kutimiza adhima yake ya kuwa mkoa jambo ambalo ni kinyume na dhana na falsafa ya uundwaji wa mikoa katika historia ya taifa hili lililoasisiwa na viongozi wetu mahiri. Geita mkoa mama, nao ni mchanga ulioanzishwa mwezi Machi mwaka 2012 ukimegwa kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Kagera. Pamoja na uchanga wake, Geita ni moja ya mikoa midogo ikiwa na kilomita za rnraba 20,054. Ukichukua ukubwa wa rniina wa Geita (20,054Km2) na Kagera (35,686Km2) kwa pamoja haifikii ukubwa wa Mkoa wa Tabora wenye ukubwa wa kilomita za mraba 76,150 au Morogoro wenye ukubwa wa kilomita za mraba 70,624. Ipo mikoa mikubwa na mikongwe iliyostahili kuleta ornbi kama hili, slyo wilaya ya Chato wala mkoa wa Geita. Kwa ukumbwa wa mkoa wa Kagera na/au Geita kuenendelea kuumega, mikoa ya Kagera na Geita itakuwa mkoa mdogo sana.

3. FAIDA
Kwa tathmini za kiuchumi, kijamii na kisiasa na kwa kuangalia jiografia ya mkoa wa Kagera kwa sasa na wilaya zinazolengwa kupelekwa hakuna faida yoyote kwa mkoa wa Kagera inayoweza kushawishi wananchi wa Mkoa wa Kagera kuridhia whlya za Biharamulo na Ngara kupelekwa mkoa pendekezwa.

4. ATHARI
Kwa kutumia vigezo vilivyotajwa hapo juu, athari kwa mkoa wa Kagera bila wilaya zake hizo mbili na kwa taifa zima la Tanzania ni kubwa sana.

4.1 KIJAMII:
(i) Mkoa wa Kagera ni muunganiko na mshikamano wilaya sabwa (7) za utawata zenye halmashauri nane. Pamoja na kuwa na wananchi wanaoweza kuhesabika kuwa makabila yanayojionyesha manne na koo nyingi sana, mapito ya mkoa huu katika historia ya kuwepo kwake yanaufanya mkoa huu kuwa jamii iliyoshikamana na imara kijamii, kisiasa na kiuchurni. Mkoa wa Kagera kwa kupakana na kuwa karibu na nchi nyingi umekuwa ukifikiwa na wageni wengi wa aina mbali mbali lakini wakati wote wana-Kagera walijiona wamoja na katika umoja huo wameweza kuhimiti matokeo yote hasi yaliyoletwa na wageni hao.

(ii) Kwa kuomba kuondoa wilaya za Ngara na Biharamulo kutasababisha mgawanyiko katika jamii na kufufua tofauti za kikabila na kikanda na koo zilizokwisha zikwa kwa
siku nyingi za uhai wa mkoa huu. Pamoja na sababu nyingine, hii inatokana na ukweli kuwa wananchi wa Wilaya tano zinazobaki hawakukubaliana na hawatafurahia wilaya za Biharamulo na Nsciwa kumegwa.

(iii) Kwa taifa kuna athari kubwa za kijamii, kisiasa na kiusalama kwani mpangilio wa Wilaya tatu (3) zinazopendekezwa kuunda mkoa pendekezwa, zinawingi wa watu wenye nasaba na ushawishi wa mataifa ya jirani ambayo hayajatulia kiusalama. Mshikamano wa mkoa wa Kagera uliojengeka kwa muda mrefu uliweza kudhibiti na kumaliza nguvu athari hiyo.

4.2 KIJIOGRAFIA:
(i) Kuondoa wilaya za Biharamulo na Ngara kuna itenga Kagera inayobaki na kuinyima nafasi ya "location advantage" ya mipaka ya Kabanga na Rusumo. Ustawi wa Mkoa wa Ziwa Magharibi u;itokana na hiyo "location advantage". Katika zama hizi ambazo biashara kati ya mkoa wa Kagera na nchi jirani unaendetea kukua na kuimarika, kuzimega wilaya hizo kutaunyima mkoa wa Kagera fursa hizo za kibiashara.

(ii) Mgawanyo au kumegwa huku kunapunguza eneo la mkoa wa Kagera. Mkoa wa Kagera una ukubwa wa eneo la mraba 35,686 (KM2 35,686) ikijumuisha nchi kavu na eneo la maji ya ziwa victoria. Eneo la maji ni kilomita za mraba 10,173 na eneo la nchi kavu ni kilomita za mraba 25,513. Wilaya ya Biharamulo na Ngara ambazo ni maeneo ya nchi kavu ni kilomita za mraba 9,371. Hivyo, kumega wilaya hizo mbili, Mkoa wa Kagera utakuwa umebaki na kilomita za mraba 16,142 zinazofaa kwa kilimo utalii. ikumbukwe, Kagera si mkoa
unaotawaliwa na shughuli za huduma (Service industry) hali ambayo eneo dogo linaweza kuwa na watu wengi na shughuli nyingi za kiuchunii zinazohalalisha uwepo wa eneo la kiutawala kiasi cha mkoa. Huu ni mkoa wa wakulima, wafugaji na wavuvi hivyo kupunguza eneo Iake ni kuudhohofisha kijamii, kihistoria na kiuchumi.

(iii) Katika uhai wa mkoa huu na hasa rniaka 15 mpaka leo tumepigana sana kuwa karibu k\Ara kujenga miundombinu ya barabara. Kwa kazi inayoendelea kwenye ujenzi wa barabara mzunguko wa ndani kwa ndani kwenye mkoa itakuwa si tatizo. Kimsingi suluhisho si kumega wilaya bali kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara, reli, afya, na uchumi.

4.3 KISIASA:
(i) Kagera bila Ngara na Biharamulo kisiasa siyo Kagera tunayoiona leo. Kufikia hatua hii ya kuwa na jamii tulivu na inayoelewana yenye mshikamano na mtazamo wa kimaendeleo haikuwa kazi rahisi, Wapo watu walihangaika kwa adhi na nyadhifa mbali mbali nao kwa kutambua mchango wao kwa Kagera si busara kuumega kila uchao.

(ii) Siasa ya Kagera ni zaidi ya mtazamo wa chama cha siasa na chama au vyama vingine. Tunazungumuza siasa kama hali au mtazamo wa jamii iliyoshuhudia na kuhimili kuanguka kwa uchumi baada ya kuvunjwa Chama cha Ushirika (BCU), Kuanguka kwa bei ya kahawa, jamii iliy()!itangulia taifa katika Vita dhidi ya Nduli ldd Amin Dada, jamii iliyopokea wimbi la wakimbizi toka nchi jirani, lakini pia jamii ambayo ilikuwa ya kwanza kupigwa na janga hatari la ukimwi. Pia jamii hii iliyokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi lililoaribu miundombinu na mali za watu, jamii ambayo wajasiliamali wake wengi na raia wengine walizama kwenye Mv Bukoba, ugonjwa wa Mnyauko wa r-nigomba kwa kutaja baadhi tu. Kimsingi, tafakari ya mapigo haya yaliyopata Kagera, Serikali inapaswa kuja na Mpango Maalum wa Kuikarabati Kagera (Special Economic Rehabilitation Program) ili ipone kwa ujumla wake na si kuumega vipande vipande kama inavyokusudiwa.

(iii) Athari nyingine kisiasa ni kufanya n-)aamuzi ya kumega mkoa kwa kufuata kilio cha mwombolezaji wa mkoa mwingine Bwana Bigambo alikuwa anaomboleza kama watanzania wote walivyoumia na kila mtu kusema lake kabla ya kutulizwa

View attachment 1997936View attachment 1997937View attachment 1997938View attachment 1997939View attachment 1997940View attachment 1997941
1
Mi naona hizo wilaya za Biharamulo na Ngara zichukuliwe tu maana ndo zinaurudisha nyuma mkoa wa Kagera kitakwimu katika kila sekta. Hao wasukuma + wasubi wa Biharamulo na wahangaza wa Ngara wapo nyuma sana. Wakwende tu.

Kwanza mkoa ukiwa mdogo si ndo safi, huduma zinakuwa nzuri kwa kuhudumia eneo dogo na watu wachache zaidi? Wanakumbatia za nini wakati wameshapata mtu wa kuwasaidia kuzichukua hizo wilaya zinazofanya vibaya kiuchumi, kielimu, kimaendeleo, n.k??

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Kwanini wapinga hoja ya kuanzishwa kwa mkoa wa chato siyo wabunge kutoka wilaya pendekezwa ya biharamulo na ngara

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Mi naona hizo wilaya za Biharamulo na Ngara zichukuliwe tu maana ndo zinaurudisha nyuma mkoa wa Kagera kitakwimu katika kila sekta. Hao wasukuma + wasubi wa Biharamulo na wahangaza wa Ngara wapo nyuma sana. Wakwende tu.

Kwanza mkoa ukiwa mdogo si ndo safi, huduma zinakuwa nzuri kwa kuhudumia eneo dogo na watu wachache zaidi? Wanakumbatia za nini wakati wameshapata mtu wa kuwasaidia kuzichukua hizo wilaya zinazofanya vibaya kiuchumi, kielimu, kimaendeleo, n.k??

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Mkoa wa kagera ni maskini in general usiwasingizie hao sijui wasubi na wengine kwa kujiona wahaya ni Bora aisee
 
Lakini ki uhalisia ukiangalia umbali uliopo kutoka Ngara hadi Bukoba ni 280Kms,Wilaya ya Ngara ni kama imetengwa kabisa Ki Mkoa.Binafsi ni sahihi Ngara kuletwa Chato kwa maana ya huduma za Ki Mkoa.Pengine kinachogomba hapa nj jina Chato kuitwa Mkoa.
Bado chato haifai kuwa mkoa ulikuwa ubinafsi tu wa jiwe aisee Yani wilaya imeze mkoa wa Geita selfish idea kabisa hyo
 
Mkoa kumegwa si tatizo kubwa bali hoja ni kuwa kuanzishwa kwa mkoa kunamnufaishaje mwananchi wa kawaida.
Ni wananchi wangapi wanaohitaji huduma za kimkoa.

Wananchi wengi tunahitaji kurahisishwa/kuboreshwa kwa huduma za vitongoji, vijiji na kata.
Nakumbuka miaka ya karibuni kuna baadhi ya vitongoji viliungwa vikaongezwa ukubwa.

Tusaidieni kupunguza ukubwa wa maeneo yaliyo jirani yetu.
Wapeni posho, vyombo vya usafiri, vifaa vya kazi nk viongozi wa chini ili wawahiudumie wananchi kwenye vitongoji, vijiji na kata zao.

Kuanzisha mkoa kuna gharama kubwa mno ikiwamo majengo, magari, mishahara na mengineyo.
Kuboresha maeneo ya chini kutaharakisha maendeleo.

Naamini hitaji la wananchi si Wilaya wala mkoa mpya.
Tuleteeni wataalam wa kilimo, afya, elimu, maendeleo na ustawi wa jamii, mifugo nk huku chini.

Mungu ibariki Tanzania.

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
Nakubaliana na hili wazo lako tatizo kubwa nchi hii sio mikoa na wilaya nyingi ila huduma kwa Raia ndio changamoto kwanini serikali isiraisishwe utendaji kazi Hadi ngazi za kijiji mtu apate huduma zote muhimu kuliko kuhangaika Hadi wilayani sijui mkoani huko huwa si ku solve tatizo, huduma za msingi zipelekwe Hadi ngazi ya chini na watendaji wawezeshwe Mimi huwa na kereka kila jambo mtu upoteze mda Hadi wilayani na ukienda wilayani wakuzingue na kukusumbua.
 
Nshomilez mkimegwa Chato bado mtabaki na unshomilez wenu nini mbaya eboo?
 
Back
Top Bottom