Wabunge wa Kagera wapinga Mkoa wao kumegwa na kupelekwa Chato

Wabunge wa Kagera wapinga Mkoa wao kumegwa na kupelekwa Chato

Solution ni Makao makuu ya mkoa wa Geita yahamishiwe Chato halafu mkoa wa Geita ubadilishwe jina uitwe CHATO.

Ombi la muombolezaji aitwae Bigambo litakuwa limeshatekelezwa bila ya kuwaathiri Wana KAGERA
We jamaa ni bonge la SOLVA.
 
Wilaya ya biharamulo ndo maskini zaidi mkoani kagera ...
Biharamulo ni ya pili nchini kwa umaskini huku zaidi ya 60% ya wakazi wake ni maskini kadri ya takwimu.

Ngara ipo top ten ya umaskini nchini zaidi ya 52% ni maskini na ni wilaya ya pili kwa umaskini kagera.


So Bora ziunganishwe na kutengenezewa mkoa wake ili ziangaliwe zaidi

Sasa huu mkoa mpya si utaitwa UMASIKINI
 
Ila wahaya ni kiburi, nyie....

Nimesoma maneno machache sana hasa hapo kwenye CHIMBUKO LA MKOA MPYA WA CHATO na naomba kunukuu:-

"Chimbuko la kuomba mkoa mpya wa Chato halina mashiko kisiasa, kiuchumi wala kisheria"

Naendelea kunukuu....

"Chimbuko la mkoa wa Chato linatokana na muombolezaji mmoja aitwaye Bigambo wakati wa msiba wa hayati Magufuli."

"Muombolezaji huyo alidai kusikia kwamba Magufuli alitaka Chato uwe mkoa, jambo ambalo halina uthibitisho wowote wa kisiasa"

Mwisho wa kunukuu.

My take:
Yaani hawa jamaa (Wahaya) "wameikataa" kabisa Chato na wakafika mbali zaidi kwa kusema "zilikua ni hasira tu" za kufiwa (za msiba) za bwana Bigambo.
Lakini pia wametanabaisha kwamba alichokisikia bwana Bigambo hakina uthibitisho wowote, kwahiyo huenda Bigambo alikua "anatujaza tu".
Sasa unachopinga ni nini. Kiburi kipo wapi hapo uliponukuu
 
Watoe hizo wilaya zinauangusha mkoa wa kagera.

Yaan biharamulo 60% wako chini ya dola
Wawapeleke wapi ndugu zenu[emoji23][emoji23] na wakiondolewa ndo mtakua matajiri ama? Mbona mnajiongopea sana? Kama ni huduma serikali ilitakiwa iwasogezee na siyo kutengeneza mkoa mpya. Hizo ni extra expenses za administration. Ujinga kbs huu. Halag kisa matakwa ya jiwe. Kumbafu kbs. Kila mahali wana haki ya kupata huduma zote. Kila mtu anastahili kupata mahitaji muhimu. Serikali iache ubabaifu. Kuunda mkoa mpya siyo solution. Kama ni huduma wasogezewe. Idiots kbs

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Wana kagera msikubali mnaamishwa chato, huko ni kuharibu historia ya mkoa wenu ilianza kumegwa biharamulo na sasa ngara, kisa interest za kiongozi mubinfasi.
Acha wajitenge maana wasubi, wahangaza, nk wamebaguliwa sana na hao akina nshomire......
Uzuri wa ubaguzi huwa hauishii kwenye "wapemba na waunguja" ndani kabisa kuna wanyambo, waziba, wahamba, wanyaihangiro, wahyoza, waendangabo, nk!
 
Jamani mi nauliza: Kama jiwe agekuwepo hao wabunge wangethubutu au hata kufikiria kupinga??
 
Sijapinga mkuu.

Cha msingi ni wamemaanisha kwamba Kagera is not for Charity. Na hii ndio kibri ya kihaya.
Sio kiburi. Mkoa huu ushatengwa hapo kabla sasa unatengwa tena kisa kuna marehemu alijenga International Airport porini na miundombinu isiyo ya lazima kusiko na uhitaji. Mikoa mikubwa Tanzania hutoweza kuikuta Kagera, kwanini isivunjwe hiyo ili kurahisisha huduma. Kwahiyo kila rais akifa wilaya yake tunaifanya mkoa?

Huyohuyo ndio alitaka Dar ivunjwe mjini ianzie wapi sijui. Ethiopia na Nigeria walianza hivi hivi kila anayechaguliwa anaangalia kwao
 
Wabunge wa Mkoa wa Kagera, Wamepinga kitendo cha kuendelea kuumega Mkoa wa Kagera. Hii imekuja baada ya Kuanzishwa Mchakato wa kufanya Wilaya ya Chato iliyopo Geita kuwa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule, alisema Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Geita (RCC) ilipendekeza wilaya tano, Chato na Bukombe
1.Kwa hiyo mkoa wa Kagera una wabunge watatu???
2. Lini hao wabunge watatu wakawa wasemaji wa wananchi wa mkoa mzima??
3. Kama vikao vya halmashauri husika za biharamulo na ngara zilipitisha wao wanatoka wapi??
4. Katika madai yao mbona hatuoni hata mbunge mmoja wa hizo wilaya??
5. Unaanzaje kusema biharamulo ndo nguzo ya uchumi wa Kagera wakati ndo wilaya maskini zaidi Tanzania???
6. Unaanzaje kusema eti biharamulo ikiondoka Kagera aanakag
 
Hawana ubavu wa kuigomea CCM kama itaamua kuipa Chato hadhi ya kuwa Mkoa (Manispaa) , kwa hiyo hata kama hoja zao zina mashiko ila chama ndicho kinaongoza Serikali na ndicho kitamuua.
 
1.Kwa hiyo mkoa wa Kagera una wabunge watatu???
2. Lini hao wabunge watatu wakawa wasemaji wa wananchi wa mkoa mzima??
3. Kama vikao vya halmashauri husika za biharamulo na ngara zilipitisha wao wanatoka wapi??
4. Katika madai yao mbona hatuoni hata mbunge mmoja wa hizo wilaya??
5. Unaanzaje kusema biharamulo ndo nguzo ya uchumi wa Kagera wakati ndo wilaya maskini zaidi Tanzania???
6. Unaanzaje kusema eti biharamulo ikiondoka Kagera aanakag
Madini na hasa dhahabu inayochimbwa Biharamulo, nk .....wanasiasa huwa wanaangalia matumbo yao tu!
 
Upuuzi tu uliojaa wivu mikoa inagawanywa na kuongezeka kwa lengo la kusogeza na kuharakisha huduma kwa wananchi, wao ni akina nani na kwani nini wapinge, Kagera haina uspecial wowote, ilimegwa Mwanza, Arusha, Shinyanga, Mbeya, Rukwa, Iringa wao ni nani hadi wapinga huu mwendelezo wa kugawa mikoa?

Upopoma wa kindezi kabisa roho ya uchoyo, ubinafsi na kupenda kujiona bora itawaua pumbavu kbsa na mashavu yenu ya senene.

Wapende wasipende Mkoa wa Chato ushaiva kwenye hili Rais Ndugu Madam Hassan asifanye utani na ulegevu wa kuwasikiliza hawa wahaya uchwara.

Ni upumbavu kuwapa fursa ya fitina watu wenye choyo, ubinafsi, wivu kithiri usio na tija na wenye ubaguzi hasa kutopenda kuchangamana na wengine.
Mkoa ukigawanywa makao makuu yawe Lusahunga ili hizo huduma ziwe karibu na wananchi wote, Chato, Kakonko na Ngara. Kuweka makao makuu Chato ni kuwaonea wengine na mantiki ya kusogeza huduma kwa wananchi inakuwa haipo.
 
Mimi sioni mantiki ya kuanzisha mikoa mipya na wilaya mpya. Kwenye technologia ya kisasa ya e-government, e-banking, e-farming, e-courts nk. hoja ya ukubwa wa eneo haina mashiko kabisa. Haya sasa kama hoja ni ukbwa basi Tabora igawanywe iwe mikoa mitatu!
Mbona Marehemu Ben Mkapa (RIP) aliwahi kusema nchi hii ni kubwa sana - mbona hamkufikiria kuigawanya mkaanzisha nchi nyingine ndani ya nchi hii kubwa?.

Hoja ya Chato kuwa mkoa haina mashiko - je makao makuu yatakuwa wapi? Utasikia wana Chato wanasema tunao uwanja wa ndege, tunayo hospitali inajengwa kubwa, kwa hiyo makao makuu yawe Chato. Huyu wa Kakonko umemsaidiaje? Umbali kati ya Geita na Chato ni kiasi gani?

Rais Samia achana na watu wa aina hiyo, hizo gharama za kuanzisha mkoa mpya zitumie kujenga barabara za vijijini kwa kiwango cha lami ili mazao yasafafirishwe kwa urahisi.

Hata hii hoja ya kujenga maghorofa makubwa ya mawizara huko Dodoma, wakati vijijini barabara ni mbovu, haina mashiko. Eti mnajenga ofisi ya ghorofa sijui 6 kwa wizara - mnataka kupangisha?
 
Mm naona watu wa humu wanaotetea mkoa mpya wa CHATO kuanzishwa ni Zero brain kama wazo hili lilikuwepo muasisi alishindwa nn kuiimarisha Kagera kwanza katika miundombinu ikijumuisha stand ya mabasi ya kisasa, barabara, uwanja wa ndege na taasisi za serikali ziwe za kisasa ndio aanze program ya mkoa mpya!

Ubaguzi kwa hapo naona mhaya hana ila watu wana chuki binafsi na wahaya ila kiuhalisia mkoa wao umechoka sana. Si busara kuanza kipya cha zamani ukakitupilia mbali. Mbaguzi ni yule aliyeelekeza hela za rambirambi za tetemeko la ardhi la mkoa huo sehemu nyingine, kama angewekeza hela yote iliyopatikana kwa mkoa husika hawa watani zangu wasingekuwa wanalalama hadi sasa mana wanaonekana bado wana kinyongo sana na kuhisi kutengwa.

Pia kiusalama wana hoja hapo Kuna vinasaba vya aina mbili vitatengwa yaani warundi na waganda ule mchanganyo uliokuwepo ulikuwa na mantiki sana katika kupata taarifa sahihi ya wakazi asili wa maeneo husika.
 
Nimefika Chato. Ile wilaya JPM aliijaza miradi mikubwa sana ya kitaifa.
Uwanja wa ndege.
Miradi kibao ya NHC.
MABANKA MAKUBWA.
IKO MIRADI MINGI SANAAAAAA.

HII MIRADI ISIPOTENGENEZEWA MIKAKATI YA KUITUMIA ITAKUFA NA SERIKALI ITAPATA HASARA.
KUIGEUZA MKOA NI SOLUTION ILIYOPO.

SABABU ZA WAHAYA KUUKATAA MKOA WA RUBONDO ZIMEKAA KIHUNI TU.
Mkuu hebu ziangalie na pesa zilizopotea kwenye mchakato wa katiba mpya,mbona huzioni au ziliokotwa,au zilitoka kwenye mifuko ya watawala?
Hiyo miradi nayo ife tu,ndipo mtaona umuhimu wa katiba mpya.
Nchi inapelekwa kokote anakotaka mtawala.

Subirini,baada ya miaka mitatu mtaiona zenji ikipaa kimaendeleo

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Si alisema atahamia Kagera, ndo wajue mwenzao aliishachora ramani

Wakiamua wafute Kagera iwe Chato tu.
 
Back
Top Bottom