Mkoa kumegwa si tatizo kubwa bali hoja ni kuwa kuanzishwa kwa mkoa kunamnufaishaje mwananchi wa kawaida.
Ni wananchi wangapi wanaohitaji huduma za kimkoa.
Wananchi wengi tunahitaji kurahisishwa/kuboreshwa kwa huduma za vitongoji, vijiji na kata.
Nakumbuka miaka ya karibuni kuna baadhi ya vitongoji viliungwa vikaongezwa ukubwa.
Tusaidieni kupunguza ukubwa wa maeneo yaliyo jirani yetu.
Wapeni posho, vyombo vya usafiri, vifaa vya kazi nk viongozi wa chini ili wawahiudumie wananchi kwenye vitongoji, vijiji na kata zao.
Kuanzisha mkoa kuna gharama kubwa mno ikiwamo majengo, magari, mishahara na mengineyo.
Kuboresha maeneo ya chini kutaharakisha maendeleo.
Naamini hitaji la wananchi si Wilaya wala mkoa mpya.
Tuleteeni wataalam wa kilimo, afya, elimu, maendeleo na ustawi wa jamii, mifugo nk huku chini.
Mungu ibariki Tanzania.
Sent from my Infinix X624 using
JamiiForums mobile app